Pre GE2025 Utekaji wamliza Makonda

Pre GE2025 Utekaji wamliza Makonda

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Akiwa ziarani huko shinyanga mama mmoja Kabila lake amemuomba aingilie kati swal lake kwani ameangaika na Hadi kwa mkuu wa wilaya na rpc Ila hajapata msaada

Alisema mume wake akitekwa siku ambayo aliitwa Baraza la ardhi la kata ndiko siku alikotekwa na mtu ambae anagombania nae kiwanja ambapo Hadi Sasa kiwanja kile Cha mumewe kimejengwa kiwanda Cha unga

HV Kweli kesi hii Ni ya kumpelekea makonda ?

Makonda alishia kuimba nyimbo za tenzi za rohoni na kukosa Cha kumjibu mama yule aliyetekewa mume wake Toka mwak 2021
 
Akiwa siarani huko shinyanga mama mmoja Kabila lake

Alisema mume wake akitekwa siku ambayo aliitwa Baraza la ardhi la kata ndiko siku alikotekwa na mtu ambae anagombania nae kiwanja ambapo Hadi Sasa kiwanja kile Cha mumewe kimejengwa kiwanda Cha unga

HV Kweli kesi hii Ni ya kumpelekea makonda ?

Makonda alishi kuimba nyimbo za tenzi za rohoni na kukosa Cha kumjibu mama yule aliyyetekewa mume wake Toka mwak 2021
. Siarani, 🤔🤔
 
Ofisi Ya Ombudsman Tanzania, mtu asifikirie kwamba ofisi ya ombudsman itaichukua ... Tanzania, Serikali ya nchi hiyo ilianzisha ofisi kama hii kufuatilia tuhuma za kunyimwa haki, utendaji mbovu .... za viongozi ....

1706526109435.png
 
Ofisi Tume kibao chini ya serikali ya CCM lakini matokeo ni hasi au chini ya zero

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA​

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu

UTANGULIZI​


Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ni idara huru ya Serikali, iliyoanzishwa kama taasisi ya kitaifa iliyo kitovu cha kukuza na kulinda haki za binadamu na utawala bora nchini Tanzania.
THBUB ilianzishwa chini ya Ibara ya 129(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 3 ya mwaka 2000.A
Tume ilianza kazi Julai 1, 2001 baada ya kuanza kutumika kwa Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura ya 391 na Tangazo la Serikali Na. 311 la Juni 8, 2001. Tume ilizinduliwa rasmi Machi 15, 2002 baada ya kuteuliwa na kuapishwa kwa Makamishna wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wa Tanzania Zanzibar, Tume ilianza kazi rasmi Aprili 30, 2007 baada ya Sheria ya THBUB Sura ya 391 kuridhiwa na Baraza la Wawakilishi kwa kutungiwa Sheria Na. 12 (Extension Act) ya Mwaka 2003.
Eneo la Utoaji Huduma
THBUB inatoa huduma zake katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na mitano (5) ya Zanzibar kupitia ofisi yake kuu iliyoko Dodoma na Unguja; vile vile kupitia ofisi zake za kanda zilizoko Dar es Salaam, Mwanza, Lindi na Pemba.
THBUB inaendelea kufanya jitihada ili kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi kwa kufungua ofisi nyingi zaidi za matawi nchini.
Ubia
Tunaamini katika usemi usemao: “Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.” Moja ya mambo makubwa THBUB inayojishughulisha nayo ni kuimarisha mahusiano na wadau mbalimbali. Tunaamini kuwa masuala ya haki za binadamu yaliyopo nchini Tanzania yanaweza kushughulikiwa vyema iwapo tu utakuwepo ushirikiano mzuri miongoni mwa wadau.
Hadi sasa THBUB imesaini mikataba ya makubaliano ya ushirikiano na Asasi 31 Zisizo za Kiserikali katika utoaji wa elimu ya haki za binadamu na utawala bora nchini. Uhusiano bora hauishii katika kushirikishana mawazo na uzoefu tu miongoni mwa wadau, bali pia kuwa tayari kushirikishana rasilimali muhimu zinazohitajika katika utekelezaji wa malengo ya pamoja.
Tume iko tayari kushirikishana rasilimali hizo na wadau wengine wote wanaojitahidi kufanya dunia iwe mahali bora pa kuishi. Iwapo ungependa kuwa sehemu ya mahusiano haya yanayokuwa siku hadi siku, unaweza kushirikiana nasi kwa kuwasiliana nasi kwa anwani na namba za simu zilizooneshwa hapa chini.
 

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Wednesday, January 24, 2024​

THBUB na Ujumbe wa EU wakutana kuzungumzia utekelezaji wa mapendekezo ya Haki Jinai​



Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bwana Patience Ntwina (wa kwanza, kushoto) akiongea wakati wa mazungumzo baina ya Tume na Ujumbe wa EU ulipotembelea Makao Makuu ya Tume Kilimani jijini Dodoma, leo Januari 24, 2024.

Kiongozi wa Ujumbe wa EU, Bi. Nathalie Vandevelde akiongea wakati wa mazungumzo baina ya Ujumbe wake na viongozi wa Tume Makao Makuu ya Tume Kilimani jijini Dodoma, leo Januari 24, 2024.

Kamishna wa THBUB, Mhe. Dkt. Thomas Masanja akichangia hoja katika mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Tume Kilimani jijini Dodoma baina ya Tume na Ujumbe wa EU leo Januari 24, 2024.

Makamu Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Mohamed Khamis Hamad akifafanua jambo wakati wa mazungumzo baina ya Tume na Ujumbe wa EU leo Januari 24, 2024. Mazungumzo hayo yaliyofanyika Makao Makuu ya Tume Kilimani jijini Dodoma

Makamu Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Mohamed Khamis Hamad (katikati) na Kiongozi wa Ujumbe wa EU, Bi. Nathalie Vandevelde (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa THBUB ujumbe huo ulipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za Tume, Kilimani jijini Dodoma leo Januari 24, 2024. Wakili Clarence Kipobota (wa pili, kulia) aliambatana na Bi. Nathalie wakati wa ziara hiyo.


KIKAO KIZITO TUME THBUB
Tume ya Rais ya Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai nchini.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisi Kuu ya THBUB Kilimani jijini Dodoma


Leo Januari 24, 2024 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imekutana na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya (European Union - EU) na kufanya mazungumzo kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Rais ya Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai nchini.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisi Kuu ya THBUB Kilimani jijini Dodoma, Tume iliujulisha Ujumbe huo kuwa tayari imekwisha chukua hatua kadhaa za maandalizi ya utelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Kamati hiyo ya Mheshimiwa Rais, na kwamba ingefurahi kupata msaada wa wadau katika kutekeleza jukumu hilo.

Kwa upande wake, Ujumbe huo uliifahamisha Tume kuhusu utayari wa EU kuiwezesha Tume katika kutekeleza baadhi ya vipengele vya mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Haki Jinai.

Miongoni mwa maeneo ambavyo EU inaweza kuisaidia Tume kwa mujibu wa Ujumbe huo ni pamoja na: Uanzishaji wa Divisheni ya Haki Jinai, mafunzo kwa watumishi, kupata vitendea kazi na gharama za uendeshaji katika baadhi ya maeneo.

Mtaalamu wa masuala ya haki na utawala wa sheria, Bi. Nathalie Vandevelde aliongoza Ujumbe wa EU katika mazungumzo hayo akiambatana na Mshauri Mwelekezi, Wakili Clarence Kipobota.

Washiriki wa mazungumzo hayo yaliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Khamis Hamad kwa upande wa Tume walikuwa: Waheshimiwa Makamishna Dkt. Thomas Masanja, na Mhe. Nyanda Shuli; Katibu Mtendaji wa Tume, Bwana Patience Ntwina; Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria, Bwana Nabor Assey; na Mkurugenzi Msaidizi - Utekelezaji wa Sheria, Bwana Gabriel Lubagila.
 
Kamtisha nani? Kwani bado anateka watu?
Anawatishia wote wanaotishika. Mafisadi ya Nchi. Wazungu uchwara.

Makonda anateka mtu? ana ubavu? Anasingiziwa tu.

Walio jiteka wanajulikana. Ati anateka.

Mijamaa ilijiteka bhana.
 
Anawatishia wote wanaotishika. Mafisadi ya Nchi. Wazungu uchwara.

Makonda anateka mtu? ana ubavu? Anasingiziwa tu.

Walio jiteka wanajulikana. Ati anateka.

Mijamaa ilijiteka bhana.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Bongo raha sana,, sihami ng'o!
 
Back
Top Bottom