Wednesday, January 24, 2024
THBUB na Ujumbe wa EU wakutana kuzungumzia utekelezaji wa mapendekezo ya Haki Jinai

Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bwana Patience Ntwina (wa kwanza, kushoto) akiongea wakati wa mazungumzo baina ya Tume na Ujumbe wa EU ulipotembelea Makao Makuu ya Tume Kilimani jijini Dodoma, leo Januari 24, 2024.

Kiongozi wa Ujumbe wa EU, Bi. Nathalie Vandevelde akiongea wakati wa mazungumzo baina ya Ujumbe wake na viongozi wa Tume Makao Makuu ya Tume Kilimani jijini Dodoma, leo Januari 24, 2024.

Kamishna wa THBUB, Mhe. Dkt. Thomas Masanja akichangia hoja katika mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Tume Kilimani jijini Dodoma baina ya Tume na Ujumbe wa EU leo Januari 24, 2024.

Makamu Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Mohamed Khamis Hamad akifafanua jambo wakati wa mazungumzo baina ya Tume na Ujumbe wa EU leo Januari 24, 2024. Mazungumzo hayo yaliyofanyika Makao Makuu ya Tume Kilimani jijini Dodoma

Makamu Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Mohamed Khamis Hamad (katikati) na Kiongozi wa Ujumbe wa EU, Bi. Nathalie Vandevelde (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa THBUB ujumbe huo ulipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za Tume, Kilimani jijini Dodoma leo Januari 24, 2024. Wakili Clarence Kipobota (wa pili, kulia) aliambatana na Bi. Nathalie wakati wa ziara hiyo.
KIKAO KIZITO TUME THBUB
Tume ya Rais ya Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai nchini.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisi Kuu ya THBUB Kilimani jijini Dodoma
Leo Januari 24, 2024 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imekutana na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya (European Union - EU) na kufanya mazungumzo kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Rais ya Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai nchini.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisi Kuu ya THBUB Kilimani jijini Dodoma, Tume iliujulisha Ujumbe huo kuwa tayari imekwisha chukua hatua kadhaa za maandalizi ya utelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Kamati hiyo ya Mheshimiwa Rais, na kwamba ingefurahi kupata msaada wa wadau katika kutekeleza jukumu hilo.
Kwa upande wake, Ujumbe huo uliifahamisha Tume kuhusu utayari wa EU kuiwezesha Tume katika kutekeleza baadhi ya vipengele vya mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Haki Jinai.
Miongoni mwa maeneo ambavyo EU inaweza kuisaidia Tume kwa mujibu wa Ujumbe huo ni pamoja na: Uanzishaji wa Divisheni ya Haki Jinai, mafunzo kwa watumishi, kupata vitendea kazi na gharama za uendeshaji katika baadhi ya maeneo.
Mtaalamu wa masuala ya haki na utawala wa sheria, Bi. Nathalie Vandevelde aliongoza Ujumbe wa EU katika mazungumzo hayo akiambatana na Mshauri Mwelekezi, Wakili Clarence Kipobota.
Washiriki wa mazungumzo hayo yaliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Khamis Hamad kwa upande wa Tume walikuwa: Waheshimiwa Makamishna Dkt. Thomas Masanja, na Mhe. Nyanda Shuli; Katibu Mtendaji wa Tume, Bwana Patience Ntwina; Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria, Bwana Nabor Assey; na Mkurugenzi Msaidizi - Utekelezaji wa Sheria, Bwana Gabriel Lubagila.