Uteketezaji huu wa vifaranga ni unyama uliopitiliza

Sasa unachoma Moto vifaranga kwa kukosa soko maana yake ukivifuga haviwezi kukua ? Ili watu wapate Mboga?
 
Nikikupa hao vifaranga watajifia wanahitaji huduma ya hali ya juu mno. Usifikiri hao ni kama kuku wa kienyeji ndugu.

Mfugaji ambaye hajajiandaa kimtaji hata ukimpa bure anaweza kukataa.
Kwanini asitangaze kugawa bure anaamua kuchoma Moto
Hii habari niyakupika
 
Ndo biashara zilivyo zamu kwa zamu Mungu ugawa riziki, enzi za Magu walikuwa miungu watu kupata vifaranga unaweka oda miezi minne mbele tena kwa bei ya 2200.
Wengi waliacha kufuga sababu walikosa vifaranga.
 
wewe tangaza hata bei ndogo uonee kama utakosa watejaaa yani mnafanya overproduction mpaka vifaranga 3000 na bado mnataka muendelee kuzalisha wengine... huyo mtu wa sales nae wakufukuzaa kazi.
Hata ukipewa vya bure watu hawataki maana anajua hatakuwa na uwezo wa kuwalisha
 
Yeye ndie kakosa soko na sio soko limejaa, watu wanahangaika kusaka vifaranga, hawapati
Wapi huko ambapo wewe upo umeona watu wanahangaika kutafuta vifaranga na hawapati?
 
Kwahiyo wewe mabanda yako hayana kuku ulikuwa unasubiri vifike 500 ndio ununue?

Vifaranga vimetoka 2200 hadi wanasema 900 mbona hukununua ili ujaze hayo mabanda?
 
Hiko kiwanda wamefanya hivyo kupunguza hasara. Unazalisha umuuzie mfugaji let say una stock ya vifaranga 4000 unasubiri vitoke hakuna wanunuzi utafanyaje

Wangewatangazia watu waje kuchukua bure kuliko kuwachoma
 
Sidhani kama hali iko hivyo inawezekana walikuwa hawana njia kabisa! All in all Ukiwa unatetea mambo kama haya huku unamla samaki, kuku, Ng'ombe au kiumbe chochote kile ni yale yale
hao wote hawachomwi wakiwa hai
 
Haina haja ya kuvigawa bure. Kwan wangeviuza 500 wangepata shingap?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Huyo mkurugenzi namfananisha na mkurugenzi flani hivi
 
hapo pana utata inawezekana hata wao hawajapenda ila mazingira yalikuwa ni limited kwao! Maana ilikuwa inatakiwa kuvilisha na kuvitibu kila siku, so kuliko kubiacha vife na njaa wameona bora vichomwe tu
Options nzur zilikuepo. Kwan wangeamua kuvigawa bure kwa wateja, wakaichukulia kama MARKET strategies, niamin hivo vingine vingepata pa kwenda.
 
Sidhani kama hali iko hivyo inawezekana walikuwa hawana njia kabisa! All in all Ukiwa unatetea mambo kama haya huku unamla samaki, kuku, Ng'ombe au kiumbe chochote kile ni yale yale
Wamesema sokoni walipanga wauze 1000 ikashindika wakashusha 900 hola wakaona solution ni kuchoma. Nngekua mimi nd mkurugenzi ningeshusha mpka 500 au ata zaid ya hapo kama ingeshindikan ningegawa bure unless vinamagonjwa hatarishi na yasiotibika
 
Wamesema sokoni walipanga wauze 1000 ikashindika wakashusha 900 hola wakaona solution ni kuchoma. Nngekua mimi nd mkurugenzi ningeshusha mpka 500 au ata zaid ya hapo kama ingeshindikan ningegawa bure unless vinamagonjwa hatarishi na yasiotibika
kweli hapo kuna hoja ya msingi
 

Nilishachukua kuku wa kisasa wa wiki 3 nikawabadili mazingira nikawachia nje na wakienyeji walikuwa vijogoo.
Walipata shida ila baada ya kama mwezi wakaadopt maisha ya nje. baada ya miezi 8 walianza kuwika na kupanda mitetea na kuzalisha kama kawaida,
Ilifika mahali nilikuwa na kuku wa kienyeji zaidi ya 100 weupe pyee kutokana na mbegu za hao wajogoo waliokuwa wa kisasa .
kuku wa kisasa wanaweka kuadopt maisha ya kuku wa kienyeji vijogoo vikapanda na mitetea wakataga kabisa
 
Mkuu hao unaongelea wewe sio kuku wa nyama pure, hao unaongelea wewe itakuwa ni machotara au kuku wa Mayai ambayo watu wengi sana wamefanya kuyazalisha na kuku wa kienyeji na wala haina shida

Hawa ambao wanaongelewa hapa ni kuku wa Nyama, ambao wao hawajiwezi Kwa lolote na kadri wanavyokuwa wakubwa ndio kadri wanavyozidi kuwa wavivu hapa wafugaji wa kuku wa nyama wanaelewa vizuri

Me wakati nafuga hawa kuku wa nyama nilikuwa nabakisha kuku kama 10 hivi Kwa ajili ya kitoweo cha nyumbani maana kuwala wakiwa na mwezi mmoja wanakuwa hawajakomaa na hawana Radha nzuri

Hivo me nilikuwa nawapa tu maji na chakula Kwa muda wa miezi 3-4 na kuku mmoja anafikisha kilo 5-6 na nikiamua kuuza nilikuwa nauza 35000 badala ya 6000

ila shida inakuja ni kwamba wanakuwa hawawezi ata kutembea hatua 10 analala kutokana na uzito mkubwa, hivo muda wote ni kuchafuka na vinyesi vyao tu maana yanajisaidia wakati huo huo yanalalia vinyesi vyao

Kwahiyo mkuu, kuku unaongelea wewe sio hawa wa nyama japokuwa inawezekana ikawa ni kabila lingine la kuku wa kisasa
 
Kwa hiyo mfanya biashara anaweza kuona ni heri avichime kuliko kushusha bei akauza japo 500tsh akapata nusu bei? Hivyo vifaranga vina corona.

Walete sababu nyingine ila hizo ngonjela wadangaye wajinga
Hii inchi kwasasa ina watu wa ajabu sana kwenye nyadhifa za uongozi. Hadi mtu unashindwa elewa kuwa wanatumia akili au makalio kuwaza!
 
Hiko kiwanda wamefanya hivyo kupunguza hasara. Unazalisha umuuzie mfugaji let say una stock ya vifaranga 4000 unasubiri vitoke hakuna wanunuzi utafanyaje
Walivileta hadi Dar wakarudi navyo Kilimanjaro, kwann wasingeviacha Dar waviuze hata kwa mkopo tu.
 
Hiko kiwanda wamefanya hivyo kupunguza hasara. Unazalisha umuuzie mfugaji let say una stock ya vifaranga 4000 unasubiri vitoke hakuna wanunuzi utafanyaje
Gawa mitaani, watachukuliwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…