Uteketezaji huu wa vifaranga ni unyama uliopitiliza

Uteketezaji huu wa vifaranga ni unyama uliopitiliza

Hata mie sijaelewa,nilikuwa nataka kuagiza vifaranga toka Iringa kuja hapa nilipo nikaambiwa kifanga kimoja ni 2500 na usafiri ni juu yangu.Nilikuwa ndo natafuta pesa hapa niagize.Du ningejua kn vya bei nafuu hapo Moshi ningechangamkia fursa make moshi na hapa nilipo ni karibu.Je walitangaza wapi mpk watanzania tushindwe hiyo bei wakaona soln ni kuchoma?Sijapenda,nashauri serikali iwachukulie hatua kwa ukatili dhid ya hao ndege
Inasikitisha sana. Kuna mtu alisema haya mauaji ya viumbe hai sio bure ni makafara
 
Shida yenu hamuelewi kinachoendelea mtaani, vifaranga kwa sasa wanunuzi hawavitaki hata bure kwa sababu vyakula vya kuku vimepanda bei karibu mara 10-15.

Imagine debe la pumba lililokuwa linauzwa elfu 1, kwa sasa linauzwa elfu 10, maeneo mengine mpaka elfu 15.

Hapo hata kama utapewa vifaranga bure haisaidii maana utaingia hasara tuu maana gharama za uendeshaji zitakuwa kubwa kuliko faida.

Screenshot_2022-12-14-06-21-09-352-edit_com.gbwhatsapp.jpg
 
Nimeona jana Waziri wa Mifugo katika kauli ya kwamba ile kampuni inatakiwa kufuatiliwa na vyombo vya dola kwa kosa la kuchoma vifaranga. Binafsi imeniuma sana kuona watu wanatoa uhai wa viumbe vya mwenyezi Mungu hadharani tena kwa moto. Pale kuna kitu nyuma ya pazia sio kweli kukosa wateja ndio chanzo. Si bora angevigawa bure kwa watu wengine?
 
Mkuu ukiangalia njia za kuvigawa bure zilikuwa nyingi sana, ni kama vile waliingiwa na choyo tu kuzifuata na ndiyo maana nasema sasa si bora wangewalisha samaki tu kuliko kuviua kwa kuvichoma moto
Inaonekana kwamba kuna Ombwe la Elimu.

1.Tuchukulie Jirani yako kapewa vifaranga vya Bure na wewe unavifaranga ulivyonunua kwa Tsh 1500.

Ni kitu gani kitatokea wakati wa kuuza hao kuku na soko lenu ni moja?

2.DOC-Day old Chick...huyu kifaranga anaweza kuishi bila kula kwa masa 24 wastani...baada ya hapo kila utakachofanya ili aishi ni Gharama....ikiwa hujajiandaa hakuna aliye tayari kukabiliana na Hiyo Gharama...awe Mfugaji awe mzalishaji...!

Yaani hapa kinachokosekana ni Elimu...na pengine haikupaswa kuoneshwa kwenye TV kwa Sababu yule ndege alihitaji privacy wakati wa kuuwawa....lakini ile ni normal Practice!!
 
Licha ya Rais Samia kupinga vifaranga kutoka nje kuchomwa moto ,safari hii vifaranga zaidi ya elfu 30 kutoka kwenye kiwanda cha watanzania huko mkoani Kilimanjaro wamechomwa moto baada ya kukosa soko baada ya nchi kufunguliwa na vifaranga kutoka nje ya kuingia bila kufuata utaratibu huku wakiuzwa kwa bei ya chini.
20221213_084428.jpg
 
Hahahahaha nadhani Rais Samia atakuwa keshapata sasa ile habari yake ya kuwaonea huruma vifaranga wanaochomwa moto. Hapo wazee wa kazi wamemuonesha kuwa yeye hajui anajua na kuvichoma vile vifaranga yalikuwa maelekezo ya hao hao wanaomlinda usiku na mchana. Ni funzo aheshimu mamlaka maana urais siyo mtu ni taasisi wakitoa maelekezo yanakuwa siyo ya rais bali ni ya taasisi maana yeye anajifanya kupinga wakati watu wamo humo humo. Ila hii dunia haiachagi kuumbua binaadamu. Pole sana Rais Dkt Samia sijui hiyo kauli yake ya kuwahurumia hao vifaranga wa bebapari Kenyata ataendelea kuwalilia.
Na ataumbuka sana
 
Zaidi ya vifaranga 50,000 vimechomwa moto na mwekezaji mkoani Kilimanjaro baada ya Kukosa soko

Afisa mifugo wa Wilaya bi Swai amesema Serikali ilitoa kibali cha uchomaji na kanuni zote zimefuatwa

Chadema ambao ndio chama maarufu pale Moshi hadi sasa hawajaongea chochote wala kukemea kama walivyofanya vilipochomwa vifaranga vigonjwa kutoka Kenya

Habari hii imeripotiwa Katika Taarifa ya Habari ya ITV
Wafuasi wa bi tozo na wakosoaji wa Magufuli wanazidi kuumbuka
 
Kwanza naomba niseme hao siyo vifaranga original walioumbwa na Mungu or Allah, hao ni matokeo ya utundubwa mwanaadam.

Pili wangekuwa Og ambao wangeweza kujilisha wenyewe nadhani hata staff wa kiwanda wangebeba na kwenda kuwamwaga kwenye cage sababu wanatafuta na kufukua chakula popote.

Pamoja na yote kuku wa machine hana haki wala sheria ya kumlinda, kuku gani ukimuweka stendi ya daladala aondoki wala ageuki!.

[emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka hapo mwisho
 
Mi nilifikili katili ni kiwe tu kumbe wengine wapo
 
Roho imeniuma sana kuona kiumbe hai kinachoma moto!

Kwani hakuna njia nyingine isiyokua ya mateso zaidi ya kuwachoma moto? Kwanini japo wasinge wagawa bure?
Sa100 ni dictator kabisa yani kachoma vifaranga elfu 50 huu uamuzi ni wakipumbavu kabisa.
 
Back
Top Bottom