Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hahaa bia inanoga ukishushia na paja la kuku lililobanikwa kwa moto na kuwekewa madiko dikoo hahaaaaTunyweni bia
Hii zilipendwaZaidi ya vifaranga 50,000 vimechomwa moto na mwekezaji mkoani Kilimanjaro baada ya Kukosa soko
Afisa mifugo wa Wilaya bi Swai amesema Serikali ilitoa kibali cha uchomaji na kanuni zote zimefuatwa
Chadema ambao ndio chama maarufu pale Moshi hadi sasa hawajaongea chochote wala kukemea kama walivyofanya vilipochomwa vifaranga vigonjwa kutoka Kenya
Habari hii imeripotiwa Katika Taarifa ya Habari ya ITV
Ata ili pia mkalitazame!!Kupitia taarifa ya habari jana jumatatu saa mbili usiku azam tv imeripoti habari ya kiwanda kimoja cha kuzalisha vifaranga cha mjini Moshi kuteketeza mamia ya vifaranga kwa kuwatosa kwenye moto mkaili eti kisa tu vifaranga hao wamekosa soko!
Kweli japo kuku wanaliwa kila siku lakini kitendo kilichofanywa na uongozi wa kiwanda hicho ni cha kinyama tena kinyama mno,
Kwa kweli nimepigwa na butwaa baada ya kusikiliza habari ile na kumshuhudia mmoja wa wafanyakazi akitupia box moja baada ya jingine juu ya moto mkali huku vifaranga vikilia kwa uchungu!..aisee imeniuma mno.
Sababu za mkurugenzi:
Walivisafirisha vifaranga hivyo hadi Dar ili viuzwe kwa tsh 1000@..biashara ikawa ngumu kwa sababu ati kuna watu wengi sasa hivi wana ingiza vifaranga toka nje hivyo soko limetibuka..wakaamua washushe bei hadi tsh 900...bado hawakupata soko..wakaamua mzigo urudi kiwandani Moshi huko nako wakatangaza bei ya tsh 900 ikashindikana..uamuzi wao wa mwisho ukawa ni kuwateketeza kwa moto mkali!
Tuiombe serikali kitengo cha watu wa mifugo au kama bado ipo taasisi ya kutetea wanyama iwafuatilie wamiliki wa kiwanda hiki na ikibidi wachukuliwe hatua kali ili iwe onyo kwa wengine watakaofikiria kufanya upuuzi huu.maana mkurugenzi wao ameshasema kuwa vifaranga wengine laki nane na nusu wanatarajiwa hivi karibuni na hajui pa kuwapeleka.
Nimejiuliza kwanini basi hata huku Dar na Moshi wasivigawe kwa mtu yeyote atakayeweza kutunza?hata kama mtu angechukua 20 mwingine box 4,mwenye vifaranga 60 nk wangetangaza tu hadharani..au kuwatangazia hata majeshini,vyuoni pengine wangejaribu kuwakuza vifaranga hao wa nyama na mayai.
Nimalizie kwa kusema kitendo kile ni cha kishetani na hakina budi kulaaniwa na serikali ichukue hatua stahiki na hili lisijirudie.
Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
the irony wanasema kumlisha kuku-dume ni ghali zaidi ili umle nyama na bado atakua na uzito mdogo & will take longer to mature, now. who bares the cost? kuna kampuni nilisoma waliacha kufanya culling lkn added cost wakaongeza kwenye mayai wanayouza kwa wateja wao. hivyo ni kama hamna namna hii kitu lazima iwe addressed properly in one way or another."However, some certified pasture-raised egg farms are taking steps to eliminate the practice entirely"
Huyu Samia ni muuaji mkubwa.Nchi ameifungulia kiholela na kusababisha wafugaji kukosa soko na kupelekea kuteketeza mifugo yaoSina la kuongezea
View attachment 2445628
Havijaingizwa, vimezalishiwa Moshi. Vimekosa soko baada ya vifaranga kutoka nje kuruhusiwa kuingia na hivyo vya ndani kukosa soko.Binafsi naona hao waliovichoma hivyo vifaranga, hawana akili! Sababu ya kuvichoma ni ipo? Vina magonjwa? Kwa uthibitisho upi? Huu ni ukatili uliopitiliza dhidi ya viumbe hai.
Kama tatizo ni kuingizwa nchini kinyume na utaratibu, wangevitaifisha basi! Halafu wangeenda kuvigawa kwenye taasisi zao! Mfano kwenye mashule, magereza, nk.