Uteketezaji huu wa vifaranga ni unyama uliopitiliza

Kupitia taarifa ya habari jana jumatatu saa mbili usiku azam tv imeripoti habari ya kiwanda kimoja cha kuzalisha vifaranga cha mjini Moshi kuteketeza mamia ya vifaranga kwa kuwatosa kwenye moto mkaili eti kisa tu vifaranga hao wamekosa soko!

Kweli japo kuku wanaliwa kila siku lakini kitendo kilichofanywa na uongozi wa kiwanda hicho ni cha kinyama tena kinyama mno,
Kwa kweli nimepigwa na butwaa baada ya kusikiliza habari ile na kumshuhudia mmoja wa wafanyakazi akitupia box moja baada ya jingine juu ya moto mkali huku vifaranga vikilia kwa uchungu!..aisee imeniuma mno.

Sababu za mkurugenzi:

Walivisafirisha vifaranga hivyo hadi Dar ili viuzwe kwa tsh 1000@..biashara ikawa ngumu kwa sababu ati kuna watu wengi sasa hivi wana ingiza vifaranga toka nje hivyo soko limetibuka..wakaamua washushe bei hadi tsh 900...bado hawakupata soko..wakaamua mzigo urudi kiwandani Moshi huko nako wakatangaza bei ya tsh 900 ikashindikana..uamuzi wao wa mwisho ukawa ni kuwateketeza kwa moto mkali!

Tuiombe serikali kitengo cha watu wa mifugo au kama bado ipo taasisi ya kutetea wanyama iwafuatilie wamiliki wa kiwanda hiki na ikibidi wachukuliwe hatua kali ili iwe onyo kwa wengine watakaofikiria kufanya upuuzi huu.maana mkurugenzi wao ameshasema kuwa vifaranga wengine laki nane na nusu wanatarajiwa hivi karibuni na hajui pa kuwapeleka.

Nimejiuliza kwanini basi hata huku Dar na Moshi wasivigawe kwa mtu yeyote atakayeweza kutunza?hata kama mtu angechukua 20 mwingine box 4,mwenye vifaranga 60 nk wangetangaza tu hadharani..au kuwatangazia hata majeshini,vyuoni pengine wangejaribu kuwakuza vifaranga hao wa nyama na mayai.

Nimalizie kwa kusema kitendo kile ni cha kishetani na hakina budi kulaaniwa na serikali ichukue hatua stahiki na hili lisijirudie.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Hiki kitu kinatakiwa kiwekewe utaratibu na Serikali; na kama utaratibu upo basi unahitji kuwa revised. Ni kitu kibaya sana hiki
 
Kupitia taarifa ya habari jana jumatatu saa mbili usiku azam tv imeripoti habari ya kiwanda kimoja cha kuzalisha vifaranga cha mjini Moshi kuteketeza mamia ya vifaranga kwa kuwatosa kwenye moto mkaili eti kisa tu vifaranga hao wamekosa soko!

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Si wangeweza hata kuchukua ption ya kuwagawia watu wengine sehemu mbali mbali za nchi ambako kuna masoko? Naamini wapo wazalishaji wengine ambao uzalishaji wao umelegalega, wengeweza kuwatangazia wakaja wakachukua vifaranga hao. Mimi kwa kweli kwa watu ambao priority yao kubwa ni pesa tu huwa sipati muda wa kuwaelewa. Unachomaje moto chakula wakati wapo majirani walio na njaa?
 
HIVI HAO VIFARANGA WANAOTENGENEZWA MAABARA BILA BABA NAO NI VIUMBE HAI???
 
Tanzania ni nchi yenye walalamikaji sana. Nimeshangaa kuona watu wengi kiasi hiki hawajui ugumu wa kufuga kuku wa kisasa hawa, mtu anadai eti wangevigawa kwa vituo vya kulea wazee wavifuge. Mtu huyo huyo ukimpa 1000 na milioni 2 ukamwambia afuge trust me hatoboi. Hao wazalishaji sio wajinga kama mnavyofikiria, ni kama nyanya tu zisipouzika unafanyaje
 
Tanzania ni nchi yenye walalamikaji sana. Nimeshangaa kuona watu wengi kiasi hiki hawajui ugumu wa kufuga kuku wa kisasa hawa, mtu anadai eti wangevigawa kwa vituo vya kulea wazee wavifuge. Mtu huyo huyo ukimpa 1000 na milioni 2 ukamwambia afuge trust me hatoboi. Hao wazalishaji sio wajinga kama mnavyofikiria, ni kama nyanya tu zisipouzika ubafanyaje
Nilifuga wangu wakapata ugonjwa sijui unaitwa Coccidiosis nilichanganyikiwa ...

Wanakufa kama hawana akili, nililia na nikakata tamaa ya kufuga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Exactly [emoji817]...
Aisee kiukweli watu wana roho mbaya sana...
Si bora utoe bure..huu ni ushetani mkubwa sana..
GMO products itakuwa zina sumu hii geresha ya kukosa soko siwezi kuiamini.
 
Kwanza naomba niseme hao siyo vifaranga original walioumbwa na Mungu or Allah, hao ni matokeo ya utundubwa mwanaadam.

Pili wangekuwa Og ambao wangeweza kujilisha wenyewe nadhani hata staff wa kiwanda wangebeba na kwenda kuwamwaga kwenye cage sababu wanatafuta na kufukua chakula popote.

Pamoja na yote kuku wa machine hana haki wala sheria ya kumlinda, kuku gani ukimuweka stendi ya daladala aondoki wala ageuki!.
Wale ni viumbe hai kama wewe tu

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Kwahio wabaki hai alafu wafe kwa njaa ?

Nipe best alternative ambayo haita-involve mwenye kiwanda kufirisika na kuwa omba omba...
 
hapo pana utata inawezekana hata wao hawajapenda ila mazingira yalikuwa ni limited kwao! Maana ilikuwa inatakiwa kuvilisha na kuvitibu kila siku, so kuliko kubiacha vife na njaa wameona bora vichomwe tu
Wangewatoa bure...huu ni umagufuli mwingine
 
Vifaranga haviwezi kujileo vyenyewe viwe vifaranga vya kiswahili au vya kizungu ni sawa na mtoto mchanga hawezi kujilea mwenyewe ukishasikia kifaranga ni sawa na mtoto mchanga, vifaranga vinahitaji malezi makubwa we chunguza vifaranga vya kiswahili vikiwa na mama yao wanavyo pewa malezi usiku au wakati wabaridi mama yao uwapatia joto kwa kuwakumbatia na wakati wa chakula mama uwatafutia chakula tena hii ni kwa ndege wote, sasa itakuwa kwa vifaranga vya kizungu visivyo kuwa na Mama mtu tu wakawaida havichukue akavifuge kienyeji hata siku mbili havifiki bora ata kuku wa kiswahili wanaweza kutoboa, Kuku wa kisasa kwanza wanakula masaa 24hrs na wanatakiwa wawekewe taa na majiko ya kuwaletea joto usiku na maisha yao yote ni kuwanywesha madawa bila madawa hawa wezi kuishi na bandani kwao lazima ukiingia ujisafishe na maji ya dawa na utenge viatu vya kuingia navyo bandani mwao.
Nilishawahi kuvinunua 4 kwa ajili ya mwanangu pale tazara nikavitafutia box na chakula starter,chanjo mbona walikua wakubwa na nikawachanganya na wa kienyeji waliishi na kukua kabisa

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Kwanza naomba niseme hao siyo vifaranga original walioumbwa na Mungu or Allah, hao ni matokeo ya utundubwa mwanaadam.

Pili wangekuwa Og ambao wangeweza kujilisha wenyewe nadhani hata staff wa kiwanda wangebeba na kwenda kuwamwaga kwenye cage sababu wanatafuta na kufukua chakula popote.

Pamoja na yote kuku wa machine hana haki wala sheria ya kumlinda, kuku gani ukimuweka stendi ya daladala aondoki wala ageuki!.
🤣🤣🤣
 
yani aise ngozi nyeusii ni takatakaaaaaa....yani laaan kabisaa
 
Kupitia taarifa ya habari jana jumatatu saa mbili usiku azam tv imeripoti habari ya kiwanda kimoja cha kuzalisha vifaranga cha mjini Moshi kuteketeza mamia ya vifaranga kwa kuwatosa kwenye moto mkaili eti kisa tu vifaranga hao wamekosa soko!

Kweli japo kuku wanaliwa kila siku lakini kitendo kilichofanywa na uongozi wa kiwanda hicho ni cha kinyama tena kinyama mno,
Kwa kweli nimepigwa na butwaa baada ya kusikiliza habari ile na kumshuhudia mmoja wa wafanyakazi akitupia box moja baada ya jingine juu ya moto mkali huku vifaranga vikilia kwa uchungu!..aisee imeniuma mno.

Sababu za mkurugenzi:

Walivisafirisha vifaranga hivyo hadi Dar ili viuzwe kwa tsh 1000@..biashara ikawa ngumu kwa sababu ati kuna watu wengi sasa hivi wana ingiza vifaranga toka nje hivyo soko limetibuka..wakaamua washushe bei hadi tsh 900...bado hawakupata soko..wakaamua mzigo urudi kiwandani Moshi huko nako wakatangaza bei ya tsh 900 ikashindikana..uamuzi wao wa mwisho ukawa ni kuwateketeza kwa moto mkali!

Tuiombe serikali kitengo cha watu wa mifugo au kama bado ipo taasisi ya kutetea wanyama iwafuatilie wamiliki wa kiwanda hiki na ikibidi wachukuliwe hatua kali ili iwe onyo kwa wengine watakaofikiria kufanya upuuzi huu.maana mkurugenzi wao ameshasema kuwa vifaranga wengine laki nane na nusu wanatarajiwa hivi karibuni na hajui pa kuwapeleka.

Nimejiuliza kwanini basi hata huku Dar na Moshi wasivigawe kwa mtu yeyote atakayeweza kutunza?hata kama mtu angechukua 20 mwingine box 4,mwenye vifaranga 60 nk wangetangaza tu hadharani..au kuwatangazia hata majeshini,vyuoni pengine wangejaribu kuwakuza vifaranga hao wa nyama na mayai.

Nimalizie kwa kusema kitendo kile ni cha kishetani na hakina budi kulaaniwa na serikali ichukue hatua stahiki na hili lisijirudie.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Upuuzi ni pale tunaporuhusu nchi jirani kuingiza vifaranga wakati wafugaji wetu wa ndani wanazalisha na kutosheleza mahitaji
 
BTW wenzetu wa ulaya na marekani wanajadiliana ethics za hizi culling..wengine wakidai umri sahihi wa culling na wengine wakiadai technology bora ya kufanya na pia economic alternatives za kuacha au kufanya culling. sie bado naona tupo kizani sana
 
Back
Top Bottom