Uteketezaji huu wa vifaranga ni unyama uliopitiliza

Uteketezaji huu wa vifaranga ni unyama uliopitiliza

hapo pana utata inawezekana hata wao hawajapenda ila mazingira yalikuwa ni limited kwao! Maana ilikuwa inatakiwa kuvilisha na kuvitibu kila siku, so kuliko kubiacha vife na njaa wameona bora vichomwe tu
Kwa nini wasivigawe bure
 
Kuchoma ni bad sana kwann washi we aachie majalalani wakulie huko tuu? Watakaopona haya ..wakiliwa na kunguru..sawa...ila kuchoma...duuu.
Kiwanda kifungiwe
 
Kupitia taarifa ya habari jana jumatatu saa mbili usiku azam tv imeripoti habari ya kiwanda kimoja cha kuzalisha vifaranga cha mjini Moshi kuteketeza mamia ya vifaranga kwa kuwatosa kwenye moto mkaili eti kisa tu vifaranga hao wamekosa soko!

Kweli japo kuku wanaliwa kila siku lakini kitendo kilichofanywa na uongozi wa kiwanda hicho ni cha kinyama tena kinyama mno,
Kwa kweli nimepigwa na butwaa baada ya kusikiliza habari ile na kumshuhudia mmoja wa wafanyakazi akitupia box moja baada ya jingine juu ya moto mkali huku vifaranga vikilia kwa uchungu!..aisee imeniuma mno.

Sababu za mkurugenzi:

Walivisafirisha vifaranga hivyo hadi Dar ili viuzwe kwa tsh 1000@..biashara ikawa ngumu kwa sababu ati kuna watu wengi sasa hivi wana ingiza vifaranga toka nje hivyo soko limetibuka..wakaamua washushe bei hadi tsh 900...bado hawakupata soko..wakaamua mzigo urudi kiwandani Moshi huko nako wakatangaza bei ya tsh 900 ikashindikana..uamuzi wao wa mwisho ukawa ni kuwateketeza kwa moto mkali!

Tuiombe serikali kitengo cha watu wa mifugo au kama bado ipo taasisi ya kutetea wanyama iwafuatilie wamiliki wa kiwanda hiki na ikibidi wachukuliwe hatua kali ili iwe onyo kwa wengine watakaofikiria kufanya upuuzi huu.maana mkurugenzi wao ameshasema kuwa vifaranga wengine laki nane na nusu wanatarajiwa hivi karibuni na hajui pa kuwapeleka.

Nimejiuliza kwanini basi hata huku Dar na Moshi wasivigawe kwa mtu yeyote atakayeweza kutunza?hata kama mtu angechukua 20 mwingine box 4,mwenye vifaranga 60 nk wangetangaza tu hadharani..au kuwatangazia hata majeshini,vyuoni pengine wangejaribu kuwakuza vifaranga hao wa nyama na mayai.

Nimalizie kwa kusema kitendo kile ni cha kishetani na hakina budi kulaaniwa na serikali ichukue hatua stahiki na hili lisijirudie.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Hahahahaha nadhani Rais Samia atakuwa keshapata sasa ile habari yake ya kuwaonea huruma vifaranga wanaochomwa moto. Hapo wazee wa kazi wamemuonesha kuwa yeye hajui anajua na kuvichoma vile vifaranga yalikuwa maelekezo ya hao hao wanaomlinda usiku na mchana. Ni funzo aheshimu mamlaka maana urais siyo mtu ni taasisi wakitoa maelekezo yanakuwa siyo ya rais bali ni ya taasisi maana yeye anajifanya kupinga wakati watu wamo humo humo. Ila hii dunia haiachagi kuumbua binaadamu. Pole sana Rais Dkt Samia sijui hiyo kauli yake ya kuwahurumia hao vifaranga wa bebapari Kenyata ataendelea kuwalilia.
 
Hii ni sababu ya kipumbavu eti kukosa soko wasitudanganye kuna ukweli wameficha na soon mtapata majibu lazima hivyo viwanda vya nje wapigwe zakichwa hio ni kamari ndogo sana imechezwa na mtu sasa hivi anashindua kama ni kukosa soko basi na hao wa nje wangechoma ila kiwanda ni kimoja kimechoma jiongezeni mnaotetea mnaonekana wabichi sana kwenye nchi hii
 
Huyu mkurugenzi wa kiwanda naye dishi limeyumba yaani unahojiwa unatoa maelezo comfortable kabisa.

Kama hadi 900 hawajanunuliwa si bora mngeuza 500? Ok hata kama 500 hawakununuliwa si mngetoa bure? Kuchoma na kutoa bure ipi nzuri?
 
Kuna kanuni za biashara mkuu. Yeye kama anadaiwa kwa mfano, akikosa rejesho bank watamuambia hapana uliuza, ushahidi pekee ni kuchoma and it’s a common practice. Nyie mnaojifanya kuhurumia hamjui.
 
Zaidi ya vifaranga 50,000 vimechomwa moto na mwekezaji mkoani Kilimanjaro baada ya Kukosa soko

Afisa mifugo wa Wilaya bi Swai amesema Serikali ilitoa kibali cha uchomaji na kanuni zote zimefuatwa

Chadema ambao ndio chama maarufu pale Moshi hadi sasa hawajaongea chochote wala kukemea kama walivyofanya vilipochomwa vifaranga vigonjwa kutoka Kenya

Habari hii imeripotiwa Katika Taarifa ya Habari ya ITV
 
Kama kuchoma ni faida, angegawa ingekuwa hasara?
 
It is a common practice kuuwa vifaranga, labda kwa vile sie watz sio deep thinkers kivile ndo tunarukia mambo kama haya
"However, some certified pasture-raised egg farms are taking steps to eliminate the practice entirely"
 
Zaidi ya vifaranga 50,000 vimechomwa moto na mwekezaji mkoani Kilimanjaro baada ya Kukosa soko

Afisa mifugo wa Wilaya bi Swai amesema Serikali ilitoa kibali cha uchomaji na kanuni zote zimefuatwa

Chadema ambao ndio chama maarufu pale Moshi hadi sasa hawajaongea chochote wala kukemea kama walivyofanya vilipochomwa vifaranga vigonjwa kutoka Kenya

Habari hii imeripotiwa Katika Taarifa ya Habari ya ITV
Mkuu CHADEMA imekuumiza sana ,katiba mpya ni sasa,halafu inaonekana CCM hawataki soko huria kama vile hawataki vyama vingi
 
Hii ni sababu ya kipumbavu eti kukosa soko wasitudanganye kuna ukweli wameficha na soon mtapata majibu lazima hivyo viwanda vya nje wapigwe zakichwa hio ni kamari ndogo sana imechezwa na mtu sasa hivi anashindua kama ni kukosa soko basi na hao wa nje wangechoma ila kiwanda ni kimoja kimechoma jiongezeni mnaotetea mnaonekana wabichi sana kwenye nchi hii
Punguzeni ujuaji kwenye vitu msivovijua, Ni kweli saiz soko la kuku wa nyama hakuna na ubaya zaidi vyakula vya kuku vimepanda sana Kwa sababu nafaka zimepanda ndomana ata unga unaona bei ni kubwa na hiyo kupelekea wafugaji wengi kuacha

Mwezi wa 10 kifaranga kimoja ilikuwa ni 2200 ilipofika mwezi wa 11 ndipo bei zikaanza kuporomoka taratibu hadi 1300, ilipofika Dec bei ikafika 1200 hadi hiyo 900 ambayo wao walitangaza kama bei ya mwisho

Mayai kwenye incubator yanakaa siku 18-21 ili kuanguliwa kifaranga, kwahiyo maana yake ni kwamba hawa walinunua mayai Kwa bei ya zamani, inawezekana hayo mayai wamenunua tangu August/October ambayo wao kifaranga wakatakiwa kuuza bei ya 2200

Na wafanya biashara wakubwa waga hawana issue za kulipa cash, kuna uwezekano wao wanakopa na baada ya mauzo ndio wanalipa, hivo walijaribu kupunguza bei hadi pale ambapo waliona basi at least turudishe tu gharama za uzalishaji ila ikishindikana

Kwahiyo kama watatoa vifaranga bure still watatakiwa kulipa madeni ya vifaranga ambavyo walizalisha, ila wanapochoma ni faida kwao kwani ata waliowapa mayai wanaona uthibitisho kuwa kweli vifaranga havikuuzwa na vikaishia kuchomwa, kuna uwezekano wa kufutiwa madeni

Na kingine hivo vifaranga unavosema wavigawe sio hao vifaranga wa kuku wa kienyeji ambae anaweza kujitafutia mahitaji, hao wanahitaji miundombinu thabiti ili kuweza Ku survive na sio kila mtu anaweza kuwafuga kwani ni gharama sana

Hao vifaranga wanakula na kunywa maji masaa 24 na hapo bado hawajaugua, na chakula chao ni ghari usidhani wanakula pumba, maana yake ni kwamba ata kama wangegawa bure kuna uwezekano wangeenda kufa vifo vya mateso ya Njaa na maradhi kuliko huo Moto wa mara moja

Na mwisho kabisa, wale wamechomwa baada ya taratibu zote kufatwa na kupatiwa vibali kwani uchomaji wa wanayama unaruhusiwa, hivo hakuna Sheria yoyote ile iliyokiukwa hapo, kuanzia za binadamu hadi za wanyama, kuliko wangeenda kuteseka na kufa na Njaa na maradhi hiyo ndio ilibakia njia yenye unafuu Kwao lakini pia Kwa hao vifaranga
 
Back
Top Bottom