Uteketezaji huu wa vifaranga ni unyama uliopitiliza

Uteketezaji huu wa vifaranga ni unyama uliopitiliza

Huu ni upumbavu kabisa!! Si wangevigawa tu bure kwani watu wasingechukua?

Ni roho mbaya ya ubinafsi tu hiyo!! Kwa nini wasingeuza bei shindani ya soko!!

Yaani mwenye kiwanda sijui mhindi huyo sijui mzungu ana roho mbaya sana!!
 
Huyu inabidi afilisike
 
Ukatili wa kiwango kisichovumilika.. kwa nini wasingegawa kwa wananchi wanaohitaji badala ya kuchoma moto viumbe hawa
 
Sababu mbalimbali, aidha ni ubora ama bei nakadhalika nakadhalika..
Ukisikiliza mazungumzo ya hao wahusika wa hio kampuni KIBO POULTRY

Ni kuwa uzalishaji wa vifaranga ni mzuri unaridhisha na walipata hamasa kutoka kwa serikali, Na ni baada ya serikali kusitisha utoaji wa vibali vya kuagiza vifaranga nje ya nchi ambapo mwisho ilikua ni tarehe 30/7 ili kuwapa nguvu wazalishaji wa ndani. Sasa hivi vifaranga awamu wa hii vinatoka wapi ? Na kama Ni waagizaji vibali wamepata wapi ?
 
Kwa kweli undani wa jambo hili sijaufahamu vizuri, inawezekana kuna sababu hazijawekwa wazi.
 
Tusikurupuke kusema ukatili ukatili...Ni sawa njia sio nzuri ya kuua vifaranga ila mzizi wa tatizo ni nini?Kuua vifaranga ni kama jani tu la mti...mzizi wa tatizo ni nini?

Tafakari.Chukua hatua
 
Huyu Samia ni muuaji mkubwa.Nchi ameifungulia kiholela na kusababisha wafugaji kukosa soko na kupelekea kuteketeza mifugo yao
RAIS WETU SAMIA HUWEZI KURUHUSU UCHOMAJI HUU WA VIUMBE HAI, WIZARA YA KILIMO NA MIFUGO IHOJIWE JUU YA HILI, NAAMINI HAYA NI MAAMUZI HOLELA, YA KIUTENDAJI, HUU NI UCHONGANISHI, NA SI SAWA NA SI HAKI KWA VIUMBE HAWA, KWANINI BAADA YA KUKAMATWA VISINGERUDISHWA VILIKOTOKEA?, POLITICAL WAR.
 
Mimi niliona kwenye taarifa habari Jana nikajisikia vibaya sana.
Hao vifanga wamewakosea nini sasa hadi wawaadhibu kiasi kile? Hakuna njia nyingine tofauti na kuwachoma moto wakiwa hai?
 
Ujasusi wa kiuchumi,wengi wanalalamika vingegawanywa nani anajua vinaugonjwa gani utakaoleta taharuki tunapaswa kujifunza kutokana na covid-19.
 
Ujue tangu niione ile kwenye taarifa ya habari moyo haujatulia

Kwanza nalaani lakini najiuliza ilishindikana vipi kugawa bure, kuvitelekeza porini au kwenye maji huko viumbe wengine wapate kitoweo? Au ilishindikana vipi kuuza hata bei ya hasara tu (mfano sh 400) ilimradi tu visiuawe?

Yaani nikikumbuka jambo hili naona maswali ni mengi kuliko majibu... au kuchafuliana tu!
 
Hivi Tanzania [emoji1241] hakuna mashirika ya kutetea haki za wanyama? Mara huyu kachoma vifaranga, mara yule kavitupa mtoni. Jamani si mngenipa mimi kwa bei nzuri?
Hata mie sijaelewa,nilikuwa nataka kuagiza vifaranga toka Iringa kuja hapa nilipo nikaambiwa kifanga kimoja ni 2500 na usafiri ni juu yangu.Nilikuwa ndo natafuta pesa hapa niagize.

Du ningejua kn vya bei nafuu hapo Moshi ningechangamkia fursa make moshi na hapa nilipo ni karibu.Je walitangaza wapi mpk watanzania tushindwe hiyo bei wakaona soln ni kuchoma?Sijapenda,nashauri serikali iwachukulie hatua kwa ukatili dhid ya hao ndege
 
Hivi Tanzania [emoji1241] hakuna mashirika ya kutetea haki za wanyama? Mara huyu kachoma vifaranga, mara yule kavitupa mtoni. Jamani si mngenipa mimi kwa bei nzuri?
Mkuu ukiangalia njia za kuvigawa bure zilikuwa nyingi sana, ni kama vile waliingiwa na choyo tu kuzifuata na ndiyo maana nasema sasa si bora wangewalisha samaki tu kuliko kuviua kwa kuvichoma moto
 
Back
Top Bottom