Utendaji Mbovu wa Tume ya Utumishi wa Umma; Rais Samia tupia jicho lako hapo

Utendaji Mbovu wa Tume ya Utumishi wa Umma; Rais Samia tupia jicho lako hapo

Kugosola

Senior Member
Joined
Aug 7, 2021
Posts
191
Reaction score
261
Kumekuwa na malalamiko mengi sana kutoka kwa wananchi kuhusu utendaji mbovu wa Tume ya Utumishi wa Umma ikiongozwa na ndugu Muhoji aliyezungukwa na wasaidizi vilaza wavivu kutumia akili katika kushughulikia rufaa za watumishi wa umma walioonewa na waajiri enzi zile!

Kumekuwa na biasness kubwa sana katika kushughulikia rufaa za watumishi wa umma pale Tume.

1. Tume imekuwa ikishirikiana na waajiri katika kuhujumu haki za watumishi.

2. Rufaa zimekuwa zinakaa kwa muda mrefu bila kuzitolea maamuzi. Ningefurahi sana kujua kama kuna kipengele chochote kinachoibana Tume kuhusu muda.

3. Maafisa wa Tume hawako makini katika uchambuzi wa rufaa za watumishi.

4. Maafisa wa Tume wamekosa customer service or care kwenye kazi zao na hivyo kupelekea wwtumishi wanaokwenda kuulizia rufaa kuwafanya kama maadui, they are so defensive and protective.

5. Wamekuwa wakipewa rushwa na waajiri ili watumishi wakandamizwe ktk kudai haki zao kwasababu waajiri wengi wamekuwa wakiwabambikkiza makosa watumishi wao.

Hivyo basi, tunaomba Mh. Rais Samia tupia jicho lako kwenye hiyo Tume, wanafanya kazi kwa mazoea na kuminya haki za watumishi.
 
Wapi na wapi kupata hiyo suluhu
Mama na Mkwe
 
Samia atupie jicho wakati naye matatizo aliyakuta na awamu aliyoanzia kuwa madarakani ndio mambo haya yalishamiri?

Mliaminishwa kuwa mnaye mtetezi wa wanyonge ilhali akamkabidhi mpwa wake cheo cha kuwa paymaster general !?

Kwani kulikua hakuna Senior officers zaidi ya mpwa ambao wangeipata hiyo nafasi kabla yake kutokana na ubobevu wao kwenye taasisi hiyo nyeti?
 
Kwani rufaa ikishindikana Tume ya Utumishi, waweza kwenda mahakama ya kazi?
 
Huu ndio tunaita "upotoshaji"

Tume ina maafisa wasiozidi 35

Wanashughulikia rufaa za watumishi wooote wa umma ukiondoa walimu, polisi, magereza, na wanajeshi

Unajua workload ya rufaa au unalalama tu.
===

Ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji kuhusu utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Umma

NA MWANDISHI MAALUM-PSC

Tume ya Utumishi wa Umma imeanzishwa chini ya Kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma (Sura ya 298 marejeo ya mwaka 2019), pamoja na majukumu mengine Tume ina jukumu la kupokea na kushughulikia rufaa kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Nidhamu ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa dhidi yao, kwa mujibu wa Kifungu cha 25 (1) cha Sheria hii na Kanuni ya 60 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003.

Tume ya Utumishi wa Umma inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji kuhusu utendaji kazi wa Tume iliyotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa “Jamii Forum” tarehe 12 Agosti 2021 kama ifuatavyo:-

1. Kwa mujibu wa Kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 (marejeo ya mwaka 2019), Tume inaundwa na Mwenyekiti na Wajumbe 6 ambao huteuliwa na Rais ambao pamoja na majukumu mengine wana jukumu la kisheria la kutolea uamuzi rufaa na malalamiko yanayowasilishwa mbele ya Tume. Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 14(1) na (2) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 (marejeo ya mwaka 2019), Tume ina Katibu ambaye ndiye Mtendaji Mkuu. Katibu na Wasaidizi wake (Sekretarieti) ndio watendaji wa kazi za kila siku katika Tume ya Utumishi wa Umma ambao wameteuliwa baada ya kukidhi sifa na vigezo katika nafasi walizo nazo.

2. Pamoja na Sheria zilizopo, Tume inashughulikia rufaa kwa mujibu wa Mwongozo Kuhusu Mashauri ya Nidhamu na Rufaa kwa Watumishi wa Umma wa Mwaka 2009 ambapo rufaa hupokelewa, husajiliwa, huchambuliwa na kupitiwa na Kikao cha Menejimenti na hatimaye kuwasilishwa mbele ya Tume kwa uamuzi. Hatua ya mwisho ni Mrufani na Mrufaniwa kujulishwa kwa barua juu ya uamuzi unaotolewa na Tume. Utaratibu huu umewekwa ili kuimarisha utendaji kazi, kudhibiti upendeleo, rushwa na kuimarisha utoaji wa haki. Aidha, elimu kuhusiana na utaratibu huu imekuwa ikitolewa kwa wadau kupitia majukwaa mbalimbali.

3. Tume katika kushughulikia rufaa na malalamiko haitoi uamuzi kwa shinikizo au ushawishi wa Mwajiri au Mamlaka ya Nidhamu yoyote ili kuwakandamiza watumishi wasipate haki zao. Tafsiri kuwa Tume ni chombo cha kulinda maslahi ya Waajiri na Serikali. Tume inapenda kuufahamisha umma kuwa inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo.

4. Rufaa na malalamiko yanayopokelewa Tume yenye vielelezo vilivyokamilika ndio yanayoshughulikiwa na kutolewa uamuzi kwa kadri yalivyopokelewa (First in, First Out).

5. Tume ya Utumishi wa Umma, inaomba umma kuupuuza upotoshwaji huu uliotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa “Jamii Forum” na inatoa wito kwa umma na wadau wote kuwasiliana na Tume kwa ufafanuzi, maoni au suala lolote kuhusu Tume kupitia simu namba 0738166703, 0733 005 974 na barua pepe, secretary@psc.go.tz.

Imetolewa na:

John C. Mbisso

KAIMU KATIBU

TUME YA UTUMISHI WA UMMA

DAR ES SALAAM

13 AGOSTI, 2021

Hii tume iwe makini tu. Kuna watumbuliwa na cheti feki wanafikiri hii ni enzi ya ufisadi na uzembe wanaona wanaweza geuza meza.

Ila kuna hii issue ya wahitimu wa shahada wafanyakazi wa umma kwa mikataba ya kujitolea. Tume iweke utaratibu kuwapa ajira ya kudumu kwani ni kama wanayonywa nguvu na kudhulumiwa. Unakuta mtu ana miaka mitatu wanakuja wahitimu wa juzi eti wamepita usahili.
 
Hili sio jukumu la TUU

Hata ukifanya kazi kwa mkataba wa miaka3 mara 3

Huajiriwi unapofanyia kazi.

UTUMISHI wametoa hayo maelekezo kwamba AJIRA NI ZA USHINDANI,

Hizo za mikataba mnashikana mikoni tu kwa kujuana kama una sifa nafasi zikitangazwa na SEKRETARIETI YA AJIRA peleka maombi unashindane na wenzako
 
HII tume kiukweli ni Disaster kwa watumishi wa Umma kuna jamaa namfahamu mpaka amekufa hakuna alichosaidiwa na hao vilaza, Nimeona wamejitia Kujibu kwa mihemko kwa Kuandika Press Release, Ni ukweli mtupu wanaopeleke Malalamiko ni wengi lakini hayashughulikiwi kwa wakati , inawezekanaje mtu ana madai yake yanazidi miaka miwili hadi mitatu hakuna anachojibiwa hakuna anachosaidiwa, watu wanawafuata fuata mpaka soli za viatu zinakwisha, hawatoi majibu hawapokei simu, hawana majibu mazuri kwa watumishi ambao ndio wanawafanya wawepo mjini, Wakati umefika hivi vitume vya dizaini hii vifutwe ili kama watu wana mambo yao wayapeleka MAHAKAMANI na si vinginevyo.

Yaani wanalundika mashauri ya watu, hawashughulikii ukiuliza unaambiwa wanasubiri fedha , yaani kukaa vikao vya kuamua na kusaidia hatma ye wenzenu ni mpaka Mlipwe POSHO enzi za mwendazake ndio kabisaaaa hawa mchwa wala posho walikua ndio hawana kazi kabisaaaa, maana jamaa alikua anaajiri yeye anafukuza yeye anaamua yeye keshi na wao wapo tu, mavyeo makuubwa utasikia sijui Katibu, Sijui Naibu Katibu Sijui takataka gani ,na wooote wanaenda kazini na kurudi kila siku, wanachofanya hakuna.

Kuna jamaa wengi wameomba sauti ipazwe kwenye mitanmdao yote ili haki zao zipatikane ni hivi watumishi wa Tanzania njaa kali hata haki zao wanalazimika wakati mwingine kuzinunua , ingekua huku kwa wenzetu maujinga haya yasingekuwepo kabisa, Kimsingi kwa TANZANIA Utumishi wa Umma ni Utumwa na ni Balaa.
 
Huu ndio tunaita "upotoshaji"

Tume ina maafisa wasiozidi 35

Wanashughulikia rufaa za watumishi wooote wa umma ukiondoa walimu, polisi, magereza, na wanajeshi

Unajua workload ya rufaa au unalalama tu.

Ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji kuhusu utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Umma

Kuna ushahidi kuwa baadhi ya Waajiri ambao wamelalamikiwa na wafanyakazi waliowafukuza wanatoa RUSHWA kwa wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Umma, ili waendelee kuwakandamiza wafanyakazi.
 
Huu ndio tunaita "upotoshaji"

Tume ina maafisa wasiozidi 35

Wanashughulikia rufaa za watumishi wooote wa umma ukiondoa walimu, polisi, magereza, na wanajeshi

Unajua workload ya rufaa au unalalama tu.

Ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji kuhusu utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Umma

Majibu haya hayamjibu mtoa mada, inakuaje tume haina utaratibu wa kujua lini mtu anajibiwa rufaa yake? Na wakati ukisoma hizo kanuni zao wanasema miezi 3 baada ya kupokea rufaa alafu hapa wanasema first in, first out. Yaani hoja zipo nyingi hapo juu majibu mepesi na vitisho juu
 
First in Firs out miaka minne , na rushwa wanaomba , ooh mimi flani shauri lako nitalisogeza kwa wakubwa fanya fanya utaratibu SHAME ON THEM vilaza
 
Huu ndio tunaita "upotoshaji"

Tume ina maafisa wasiozidi 35

Wanashughulikia rufaa za watumishi wooote wa umma ukiondoa walimu, polisi, magereza, na wanajeshi

Unajua workload ya rufaa au unalalama tu.

Ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji kuhusu utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Umma

Upuuzi mtupu!! Ni aibu kubwa sana kwa Afisa Mkubwa kama wewe kutoa ufafanuzi ambao ni utopolo mkubwa!! Shame on you!! Mnacheza na haki za Watumishi kwa maelezo ya kipuuzi kama hayo!!

Eti mnafanyia kazi rufaa za watumishi kwa first in first out! Kwani Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003 zinasemaje katika kushughulikia rufaa ya mtumishi wa Umma in terms of time frame!

Mbona mara nyingi Tume inatoaga majibu rahisi tu kuwa hawawezi kuifanyia kazi rufaa kwasababu iko nje ya Muda ulioruhusiwa kisheria?

Kwanini Tume nayo isifuate muda uliowekwa Kisheria katika kuzifanyia kazi rufaa za watumishi??

Watu kama nyie akina John Mbiso ndio mnaofanya Tume ionekane kama ni kituko! Tume imejaza vilaza na hawamsaidii Mh. Rais. Hizo tuhuma ni very serious hampaswi kutoa majibu kijumlajumla tu! Shame on you!!

Eti Tume ina Makamishina walioteuliwa na Rais, kwani hao Makamishina si ndo wanaofanya maamuzi yaliyopelekwa na nyie VILAZA?. Wazungu wanasema GARBAGE INN GARBAGE OUT!!😆😆😆

Tume ya Utumishi inatakiwa ifumuliwe, why?

1. Wako very corrupted

2. Wako very defensive

3. Wanashirikiana na Waajiri kikandamiza haki za Watumishi

4. Mara nyingi Tume haifuati Sheria na Kanuni katika kushugulikia rufaa za Watumishi

5. Wanafanya kazi kwa mazoea na customer care iko very poor. Hata namba waliyoitoa ni geresha tu kwasababu unaweza ukaipiga siku nzima na usijibiwe au ukajibiwa dry!!

Tunamuomba Mh. Rais Samia atupie jicho kwenye hiyo Tume maana inatia kinyaa. Otherwise, ikkshindikana basi Watumishi wapeleke kesi zao moja kwa moja Mahakamani badala ya kupeleka kwenye huu uchocholo!
 
Majibu haya hayamjibu mtoa mada, inakuaje tume haina utaratibu wa kujua lini mtu anajibiwa rufaa yake? Na wakati ukisoma hizo kanuni zao wanasema miezi 3 baada ya kupokea rufaa alafu hapa wanasema first in, first out. Yaani hoja zipo nyingi hapo juu majibu mepesi na vitisho juu
Hii Tume ni hovyo kabisa! Wanachezea haki za wafanyakazi kirahisirahisi tu. Sheri zinawekwa halafu wanakuwa wa kwanza kuzikiuka....pumbavu kabisa.

Afisa Mwandamizi mzima eti anajibu very simple kwamba wana workload kubwa, kwani hiyo workload inamsaidia nini mtumishi?, kwani umuhimu umuhimu wa kuweka Sheria na Kanuni ni upi?
 
Kumekuwa na malalamiko mengi sana kutoka kwa wananchi kuhusu utendaji mbovu wa Tume ya Utumishi wa Umma ikiongozwa na ndugu Muhoji aliyezungukwa na wasaidizi vilaza wavivu kutumia akili katika kushughulikia rufaa za watumishi wa umma walioonewa na waajiri enzi zile!

Kumekuwa na biaiseness kubwa sana ktk kushughulikia rufaa za watumishi wa umma pale Tume

1. Tume imekuwa ikishirikiana na waajiri katika kuhujumu haki za watumishi

2. Rufaa zimekuwa zinakaa kwa muda mrefu bila kuzitolea maamuzi. Ningefurahi sana kujua kama kuna kipengele chochote kinachoibana Tume kuhusu muda

3. Maafisa wa Tume hawako makini katika uchambuzi wa rufaa za watumishi

4. Maafisa wa Tume wamekosa customer service or care kwenye kazi zao na hivyo kupelekea wwtumishi wanaokwenda kuulizia rufaa kuwafanya kama maadui, they are so defensive and protective.

5. Wamekuwa wakipewa rushwa na waajiri ili watumishi wakandamizwe ktk kudai haki zao kwasababu waajiri wengi wamekuwa wakiwabambikkiza makosa watumishi wao

Hivyo basi, tunaomba Mh. Rais Samia tupia jicho lako kwenye hiyo Tume, wanafanya kazi kwa mazoea na kuminya haki za watumishi
Hawa si ndio walivujisha mtihani juzi hawa?
 
Back
Top Bottom