HII tume kiukweli ni Disaster kwa watumishi wa Umma kuna jamaa namfahamu mpaka amekufa hakuna alichosaidiwa na hao vilaza, Nimeona wamejitia Kujibu kwa mihemko kwa Kuandika Press Release, Ni ukweli mtupu wanaopeleke Malalamiko ni wengi lakini hayashughulikiwi kwa wakati , inawezekanaje mtu ana madai yake yanazidi miaka miwili hadi mitatu hakuna anachojibiwa hakuna anachosaidiwa, watu wanawafuata fuata mpaka soli za viatu zinakwisha, hawatoi majibu hawapokei simu, hawana majibu mazuri kwa watumishi ambao ndio wanawafanya wawepo mjini, Wakati umefika hivi vitume vya dizaini hii vifutwe ili kama watu wana mambo yao wayapeleka MAHAKAMANI na si vinginevyo.
Yaani wanalundika mashauri ya watu, hawashughulikii ukiuliza unaambiwa wanasubiri fedha , yaani kukaa vikao vya kuamua na kusaidia hatma ye wenzenu ni mpaka Mlipwe POSHO enzi za mwendazake ndio kabisaaaa hawa mchwa wala posho walikua ndio hawana kazi kabisaaaa, maana jamaa alikua anaajiri yeye anafukuza yeye anaamua yeye keshi na wao wapo tu, mavyeo makuubwa utasikia sijui Katibu, Sijui Naibu Katibu Sijui takataka gani ,na wooote wanaenda kazini na kurudi kila siku, wanachofanya hakuna.
Kuna jamaa wengi wameomba sauti ipazwe kwenye mitanmdao yote ili haki zao zipatikane ni hivi watumishi wa Tanzania njaa kali hata haki zao wanalazimika wakati mwingine kuzinunua , ingekua huku kwa wenzetu maujinga haya yasingekuwepo kabisa, Kimsingi kwa TANZANIA Utumishi wa Umma ni Utumwa na ni Balaa.