Jiwe lipo, tumeliona na kulitumia utotoni mwetu kwani wengine tumekulia sehenu zisizo na Hospitali wala Zahanati wala kituo cha afya. Tiba za asili zilikuwepo enzi na enzi kabla ya kuja kwa Wazungu na kuleta hii muitayo tiba za kisasa. Nyoka nao walikuwepo enzi na enzi na watu waliishi nao pia hata kung'atwa ila walitumia mawe na miti kama dawa na sio hizo za sasa
Jiwe la Nyoka lipo, lilikuwa Jeusi na lilikuwa "porous" mtu aking'atwa na Nyoka, alikuwa anachanjwa pale penye jeraha kidogo na damu nyeusi yenye madhara ya sumu inaanza kutoka kisha anawekewa hilo jiwe kwenye kidonda/alipoumwa na nyoka. Jiwe lile litakaa na kuning'inia pale alipokuwa na simu ukiisha kitaanguka. Ie porous nature na madini yaliyopo kwenye jiwe(Sijajua ni madini gani) ndiyo yanavuta na kuitoa ile sumu bila madhara kwa aliyekuwa.
Kipindi chetu, kila nyumba ilikuwa na yale mawe. Ni nimeyaona na kuyatumia.