Ndugu yangu, sumu iliyopo kwenye mate yety haina effect kwa nyoka.Inawezekana,umeshajiuliza inakuwaje mdudu akiingia kwenye jicho au sikio akikutana na yale maji maji anakufa,ngoja nifanye research,siku nikikutana na Nyoka nimetemee mate nione nini kitatokea,halafu ntaleta mrejesho...
Kwamba nyoka wa bongo ni wa mchongo??
π π π π yawezekana maana mi ni mara ya pili nayapoteza mara ya kwanza nlinunua.moja nikaliweka kabatini sikuliona tena mara ya pili nikanunua mawili na sasa pia siyaoniHata Mimi sijui kipo wapi au vinarudi kwa wenyewe
Iko hivi hilo jiwe, Ukipata lenyewe lina aina ya madini na pia liko porous. Hivyo ukiliweka sehemu ambayo nyoka amekung'ata muda huo huo linaifyonza sumu yote (yaani sumu inanyonywa na kuhamia kwenye jiwe) na hivyo kumnusuru mtu. Sasa ili uweze kulitumia tena ni lazima hilo jiwe ulidumbukize kwenye chombo chenye maziwa fresh na kulianika juani. Changamoto iliyopo ni kulipata jiwe lenyewe, hasa kipindi hiki cha utapeli.Ni story Tu hakuna jiwe linatibu sumu ya nyoka
Ukweli ni kwamba % ya nyoka wa tanzania sio wa sumu
Uking'atwa na nyoka wa sumu ukaweka Hilo jiwe utakufa tu
Iko hivi hilo jiwe, Ukipata lenyewe lina aina ya madini na pia liko porous. Hivyo ukiliweka sehemu ambayo nyoka amekung'ata muda huo huo linaifyonza sumu yote (yaani sumu inanyonywa na kuhamia kwenye jiwe) na hivyo kumnusuru mtu. Sasa ili uweze kulitumia tena ni lazima hilo jiwe ulidumbukize kwenye chombo chenye maziwa fresh na kulianika juani. Changamoto iliyopo ni kulipata jiwe lenyewe, hasa kipindi hiki cha utapeli.
Sijui ni kwanini kizazi hiki kimekuwa na ujuaji mwingi na kupinga kila kitu. Huo uungaji wa mifupa bila operation hata sasa wapo wanaofanya hivyo ila serikali haizitambui tiba asili kama tiba rasmi ndio maana hao wanaofanya hivyo hawawekwi huko MOI unaposema. Ni nipo Iringa na kuna mzee anafanya hiyo tiba ya kuunganisha mifupa ya mtu aliyevunjika bila operation. Vipawa hivyo vipo na watu wa Iringa wanaweza mjua mzee............. Siwezi taja Jina lake ila anafahamika tu.Walikufa na elimu zao.
Hawa wangetusaidia Sana MOI pale kuunga mifupa ya bodaboda
Jiwe lipo, tumeliona na kulitumia utotoni mwetu kwani wengine tumekulia sehenu zisizo na Hospitali wala Zahanati wala kituo cha afya. Tiba za asili zilikuwepo enzi na enzi kabla ya kuja kwa Wazungu na kuleta hii muitayo tiba za kisasa. Nyoka nao walikuwepo enzi na enzi na watu waliishi nao pia hata kung'atwa ila walitumia mawe na miti kama dawa na sio hizo za sasaKaka sumu ya cobra unaijua? Sumu ya kifutu unaijua? Acha utani ndugu yangu
Aking'atwa na nyoka kimbia kwenda hospital
Zipo sana mkuu ila vijana wa sasa wana ujuaji mwingi na kupinga kila kitu.Broo wangu alishawai kugongwa (kung'atwa na nyoko)
Walimchanja kidogo karibu na eneo alilohongwa.
Walimuwekea hilo jiwe la sumu, likaganda na kweli lilikua linavuta sumu
Baada ya muda linadondoka, inabidi mlichemshe
Then mnaliweka tena
Hiyo process inajirudi hadi unafika muda ukiliweka linaanguka muda huo huo
Alipona, na hakupelekwa hospital
TIBA ZA ASILI ZIPO, TENA KONKI SANA
Jiwe lipo, tumeliona na kulitumia utotoni mwetu kwani wengine tumekulia sehenu zisizo na Hospitali wala Zahanati wala kituo cha afya. Tiba za asili zilikuwepo enzi na enzi kabla ya kuja kwa Wazungu na kuleta hii muitayo tiba za kisasa. Nyoka nao walikuwepo enzi na enzi na watu waliishi nao pia hata kung'atwa ila walitumia mawe na miti kama dawa na sio hizo za sasa
Jiwe la Nyoka lipo, lilikuwa Jeusi na lilikuwa "porous" mtu aking'atwa na Nyoka, alikuwa anachanjwa pale penye jeraha kidogo na damu nyeusi yenye madhara ya sumu inaanza kutoka kisha anawekewa hilo jiwe kwenye kidonda/alipoumwa na nyoka. Jiwe lile litakaa na kuning'inia pale alipokuwa na simu ukiisha kitaanguka. Ie porous nature na madini yaliyopo kwenye jiwe(Sijajua ni madini gani) ndiyo yanavuta na kuitoa ile sumu bila madhara kwa aliyekuwa.
Kipindi chetu, kila nyumba ilikuwa na yale mawe. Ni nimeyaona na kuyatumia.