Mwaka huu ndio unakwenda kuisha na kuingia mwaka mpya. Ni wakati wa kujithathmini kwa mwaka huu umeweza fanya nini cha kimaendeleo cha kukuingizia kipato. Je umejifunza nini ulikosea ili ujipange upya na ufanye vitu kivingine?
Kwa ushauri tu ningemshauri yeyote anayesoma hapa kuwa tafuta elimu popote pale hata km sio kutoka kwangu jifunze lakini cha msingi zaidi ufanyie kazi hata kama ni japo kiduchu. Mwaka 2017 january labda ulisema mwaka huu ungefanya kitu fulani cha kujipatia kipato lakini imefika december sasa hujafanya chochote. K, umepanga mwaka ujao ufanye kitu basi fanya kweli ili isije tena ikafika next year december hujafanya chochote. Ni bora uanze leo ili angalau uwe na cha kuonyesha. Angalia tu usije ukawa ni mwaka wa stress kwa kukosa pesa ya matumizi
Pia kwa ushauri mwingine ni kuwa fanya shughuli au biashara kadhaa kwa wakati huo huo ili kuongeza nafasi ya kupata kipato kikubwa zaidi. Mfano ukipata haya ya sabuni huwa nawapa watu mafunzo bure ya namna ya kutengeneza bidhaa zingine ndogo ndogo bila kuwa na mtaji mkubwa mfano kutengeneza bidha km chaki, tomato na hili sosi, losheni, wine, ice cream, lamba lamba nk
Heri ya mwaka mpya