Utengenezaji wa Sabuni za Aina Mbalimbali: Fahamu Mahitaji, Mchakato wa Uzalishaji na Masoko

Je inakuwa na ubora kama haya makampuni makubwa mana naona makampuni makubwa yanazidi kupeta sioni ushindani

Unajua haya wajasiriamali wadogo wanatengeneza sabuni zenye ubora sana. Tatizo ni Vifungashio wanavyotumia ni low quality haviwezi kupata soko supermarket. Ishu ukiwa na Vifungashio bora unaongeza thamani
 
Wapi napata kemikali ya Salicylic Acid kwa hapa Dar?
 
Kwa ufupi mpendwa hapo juu amesaidia sana maelezo ila mimi ningependa kama upo dsm naweza kuja kukufundisha.0717539573 ila ukipata semina ya Dr.Lunyungu ni nzuri kwani hata mimi ni zao lake.
sabuni ya unga unaweza nifundisha na kunieleza upatikanaji wa raw material??
 
number yako ya simu tafadhali
 
Kipo kitabu cha mafunzo ya hizi sabuni za miche,unga,maji na bidhaa zingine na formula zote ni softcopy unaweza kutumiwa katika email au whatsapp kwa shilingi elfu 5 tu kipo vizuri.
 
Nimepiga hizo number ya tigo nimemuuliza naongea na kampuni ya Tanzania bussiness creation? akasema sio, number ya Voda nimepiga wanasema hiyo number haipo. Air tel haipatikani, ninashida na hiyo idea nataka kuonana na watu ain hiyo ili nipate msaada wao.
 
Jaribu SIDO

[emoji252] [emoji479]
 
Imekuwa muda kidogo, labda hawapo tena mkuu

Sent from my TECNO-J8 using Tapatalk
 
Karibuni katika uzi huu mpya wa kujifunza elimu mbali mbali juu ya utengenezaji wa losheni,cream na sabuni za:

1. Kung'arisha ngozi
2. Kuondoa chunusi harara mwilini
3. Kurekebisha ngozi
4. Kunawirisha ngozi.

Huu utakua ni uzi maalum wa kupeana maujuzi juu ya kutengeneza hivyo jamani mnaojua pls nawaomba muweke maujuzi yenu hapa hii ni fursa nzuri mnoo ya kujiajiri hata kujiingizia kipato pia.

Karibuni sana.
 
Malighafi na kazi zake:

[emoji843]Sulphonics Acid -inaongeza povu
[emoji843]Soda ash-inapunguza acid
[emoji843]Sless-hupunguza povu na kun'garisha
[emoji843]Perfume-kuleta harufu nzuri
[emoji843]Glycerin-kuleta umafuta na ulaini
[emoji843]Chumvi-kuleta uzito na kufanya bidhaa yako iishi kwa muda mrefu
[emoji843]Maji
[emoji843]Rangi-kuipa muonekano mzuri bidhaa yako
[emoji843]Kifaa kama ndoo au pipa
[emoji843]Mti au mwiko mkubwa
[emoji843]Gloves
[emoji843]Buti
[emoji843]Kifaa kitakachoziba pua na mdomo

[emoji841]VIPIMO[emoji841]
[emoji843]Sulphonic Acid vijiko 4 vya chakula
[emoji843]Soda ash vijiko 2 vya chakula
[emoji843]Maji lita4
[emoji843]Sless roho
[emoji843]Glycerin vijiko3 vya chakula
[emoji843]Rangi kijiko kimoja cha chai
[emoji843]Chumvi robo kilo

[emoji841]JINSI YA KUTENGENEZA[emoji841]
[emoji842]Andaa Malighafi zako zote na uhakikishe sehemu ni safi
[emoji842]Anza na sulphoic acid weka kwenye ndoo /pipa
[emoji842]Fuatia soda ash ila kabla haujaweka kwenye ndoo/pipa hakikisha wailoweka kwenye maji kidogo pembeni ikishakua uji ndio umimine kwenye ndoo/pipa
[emoji842]Koroga na mwiko au mti vichanganyike
[emoji842]Weka maji Lita 4 na ukoroge dk 10
[emoji842]Weka glycerine
[emoji842]Weka perfume
[emoji842]Weka rangi
[emoji842]Weka chumvi kwa kunyunyiza kidogo kidogo

Endelea kukoroga hadi bidhaa yako iwe nzito kama uji kwa dk 15. Hapo shampoo yako itakua tayari.

[emoji840]waweza ongeza vipimo vya Malighafi kutokana na wingi utakao

Shampoo yako ipo tayari kwa matumizi

Naomba maswali pale ambapo hamjaelewa

Ahsanteni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…