Utengenezaji wa Sabuni za Aina Mbalimbali: Fahamu Mahitaji, Mchakato wa Uzalishaji na Masoko

Utengenezaji wa Sabuni za Aina Mbalimbali: Fahamu Mahitaji, Mchakato wa Uzalishaji na Masoko

Mku kuhusu vifungashio anayehitaji anitumie sampuli ya anayohitaji tutafanya biashara
 
Kamwene!Wakuu mimi natengeneza sabuni za maji na shampoo.Naomba kujua namna ya kupata mashine.Pia nisaidieni namna ya kufanya ili sabuni iwe nzito sana.

Aisee ni rahisi sana utakapo changanya mchanganyiko wako usisahau kuweka kitu kinaitwa ALKA hiyo ndo inafanya sabuni yako kuwa nzito na kama unataka sabuni ikae kwa muda mrefu bila kuharibika weka FOLMALIN pia.
 
Na kama hujui jinsi ya kutengeneza sabuni nafundisha kwa vitendo tena sawa na bure kupitia youtube channel yangu
nenda youtube search gawazaTV utapata video nyingi za mambo kama hayo na usisahau ku-subscribe 4 more videos
all da best good day 2 all jf users
 
Waone Gemab Enterprises wanafundisha mambo ya sabuni ya maji ya choo ,shampoo,kufulia ,batiki,mishumaa,peanut butter,mafuta ya mgando,sabuni ya unga,chachandu nk.kwa whatsup no.0713262188 tena kwa gharama nafuu sana.
 
Waone Gemab Enterprises wanafundisha mambo ya sabuni ya maji ya choo ,shampoo,kufulia ,batiki,mishumaa,peanut butter,mafuta ya mgando,sabuni ya unga,chachandu nk.kwa whatsup no.0713262188 tena kwa gharama nafuu sana.
Gharama nafuu ndo sh.ngapi?
 
Umewapigia? Acha maswali yasiyo na maana ili hali contact zipo
Ndo mazingira ya kuuza bei tofauti tofauti kulingana na mteja alivyo kuja. Katamka yoote kwenye bei kashindwa kutaja na kuweka "nafuu" acheni biashara za kimachinga hizo.....
 
JIFUNZE KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI YA KUNAIWIA MIKONO View attachment 376324

Moja kati ya mahitaji makubwa ya watu ikiwemo wafanyabiashara za mama lishe,mabucha na nyingine,ni sabuni ya kunawia.Kutokana na mahitaji makubwa waliyonayo watu na kukosekana kwa bidhaa hiyo wahitaji hujikuta wakitumia sabuni ambazo hazikutengenezwa kwa kazi hiyo kama sabuni za unga,shampoo na sabuni za vipande ambazo huwasababishia madhara bila kujijua. Leo katika somo letu tutajifunza jinsi ya kutengeneza sabuni za kunawia mikono.fuatana nami mwanza mpaka mwisho.

MAHITAJI; .
Sulphonic acid .soda ash .maji yaliyochujwa vizuri .pafyum .Rangi yoyote inayovutia .sless .Chumvi

JINSI YA KUTENGENEZA.
Andaa vizuri chombo chako kwaajili ya kutengenezea sabuni yako kama ndoo au pipa pamoja na kuandaa malighafi zako huku ukizingatia usafi. Tanguliza kumimina ssulphonic acid vijiko vitano vya chakula kwenye chombo chako. Endelea kuweka soda ash iliyochanganywa na maji vijiko vitatu vya chai. Weka maji lita tano ukifuatiwa na sless robo lita,chukua pafyum yoyote na uweke kijiko kimoja na nusu cha chai. Ongeza rangi kijiko kimoja cha chai na uanze kunyunyizia chumvi ambayo huleta uzito na kufanya sabuni yako isiharibike na kukaa muda mrefu. Koroga vyote kwa pamoja kwa muda wa dakika ishirini na sabuni yako itakuwa tayari.
Nimependa hilo somo, kwa Mimi niliye Kilimanjaro nawezaje kupata hayo mahitaji? Msaada kwa anayefahamu kunakopatikana
 
Mbona kuna mdau alishaweka kitabu humu jukwaani cha pdf kinachoelezea kutengeneza vitu vingi tu ikiwemo hiyo sabuni kiongozi.

Upo uzi unazungumzia hiyo ngoja mdau mmoja atautafuta huo uzi atatupa link na ikiwezekana atatuwekea hata na hiko kitabu hapa coz najua watu walishaki-download tayari.

Ni suala la muda tu, tusubiri kitambo kidogo walichonacho wata-share hapa jukwaani na huu ndio uzuri wa [HASHTAG]#JamiiForums[/HASHTAG] mkuu.

Karibu Sana.
 
hii ni batiki ya mishumaa,
njoo pm tuanze kufungua kiwanda.

.......................

KUTENGENEZA BATIKI

MAHITAJI:

1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali.

2.Sponji zenye urembo mbalimbali.

3.Brash kubwa/ndogo.

4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili.

5.Sufuria.

6.Vitambaa vya mpira.

7.Misumari midogo.

8.Jiko.


MADAWA:

1.Sodium hydrosulphate.

2.Caustic soda

3.Mshumaa.


KAZI ZAKE:

1. Sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje,kama itachanganywa na caustic soda.Madawa haya huwa kazi yake ni moja lakini ikikosekana moja nyingine haifanyi kazi.

2. Kazi ya mshumaa ni kuweka urembo kwenye nguo au kwenye vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo,twiga,matunda au aina yoyote ya urembo unayotaka mtengenezaji.

JINSI YA KUTENGENEZA.

(a) JINSI YA KUGONGA MISHUMAA:

Chemsha mshumaa uchemke sawasawa kisha ipua upoe kidogo. Andaa kitambaa cha pamba (cotton) na kukitandika mezani, chovya kibao chenye picha kwenye mshumaa kisha gonga kwenye kitambaa na kuacha nafasi kidogo. Endelea kugonga picha hizo mpaka kitambaa kiishe.

(b) JINSI YA KUWEKA RANGI:

Chemsha maji ya moto yachemke sawa sawa kisha pima lita tano mpaka sita. Baada ya hapo pima caustic soda vijiko3 na sodium hydrosulphate vijiko vinne mpaka vitano. Changanya na maji ya moto,weka rangi kijiko kimoja. Baada ya hapo pima maji lita kumi na tano na changanya na mchanganyiko wa madawa ili maji yawe vuguvugu. Tumbukiza vitambaa vya vinne vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuzageuza viingie rangi kwa dakika kumi mpaka kumi na tano. Suuza kwa maji baridi na uanike kwenye kivuri ili mshumaa usiyeyuke.

(c) KUWEKA RANGI YA PILI:

Katika kuweka rangi hii kinachofanyika ni kuongeza vipimo vya ranagi tu. Ongeza vipimo vya rangi viwili na zaidi ya mala ya kwanza,maji,mudani uleule,

Weka mshumaa sehemu ambayo haina mshumaa kwa kutumia urembo uleule.Pima rangi kwa kufuata hatua zilezile. Tumbukiza vitambaa vitatu,geuza kwa mda uleule kisha anika.

(d) JINSI YA KUTOA MSHUMAA:

Chemsha maji yachemke vizuri,changanya na sabuni ya unga jikoni,tumbukiza kitambaa kimoja kimoja jikoni ili kutoa mshumaa,geuza kwa mti,suuza kwenye maji ya baridi yaliyochanganywa na maji.

PIGA PASI TAYARI KWA KUUZA.
 
Je, ulifanikiwa kupata hiki kitu rafiki?
Kama bado na unahitaji wasiliana na mimi.
 
Habari wanaJF..
Tutengeneze sabuni ya maji

MALIGHAFI
MASHINE YA KUTENGENEZEA IWE JABA AU KARAI

MAJI LITA KUMI

SULPHONIC ACID LITA MOJA

SLESS NUSU LITA

GLYCERINE VIJIKO VINNE VYA CHAKULA

SODA ASH VIJIKO VITANO VYA CHAKULA

FORMALINE VIJIKO VITATU VYA CHAKULA

MANUKATO KIJIKO KIMOJA CHA CHAI

RANGI YA SABUNI NUSU KIJIKO CHA CHAI

JINSI YA KUTENGENEZA

HAKIKISHA MASHINE YA KUTENGENEZEA NI SAFI
Weka Sulphonic acid na slees koroga vichanganyike weka soda ash koroga weka maji koroga vizuri hakikisha hakuna mabonge mabonge

Weka glycerine, formaline, perfume, rangi na chumvi kisha koroga kwa dakika 15.

Paki kauze....

ANGALIZO
SULPHONIC ACID IPO KAMA ASALI WEKA MBALI NA WATOTO MAANA NI KEMIKALI HATARI.

ASANTE

-QUEEN___
Chumvi unaweka kiasi gani?
Kuna wengine huwa naona wanauza unakuta kama Haina quality Nzuri unaona kama ni maji tu yenye rangi Huwa wanakuwa wamekosea vitu gani?
Je kama nataka kutengeneza kwa ajili ya matumizi binafsi nyumbani hiyo ratio ya mchanganyiko naweza iweka vingine ili kuongeza ubora,kwa mfano maji yawe Lita nane badala ya kumi?
 
Habari wanaJF..
Tutengeneze sabuni ya maji.

MALIGHAFI
MASHINE YA KUTENGENEZEA IWE JABA AU KARAI

MAJI LITA KUMI

SULPHONIC ACID LITA MOJA

SLESS NUSU LITA

GLYCERINE VIJIKO VINNE VYA CHAKULA

SODA ASH VIJIKO VITANO VYA CHAKULA

FORMALINE VIJIKO VITATU VYA CHAKULA

MANUKATO KIJIKO KIMOJA CHA CHAI

RANGI YA SABUNI NUSU KIJIKO CHA CHAI

JINSI YA KUTENGENEZA

HAKIKISHA MASHINE YA KUTENGENEZEA NI SAFI
Weka Sulphonic acid na slees koroga vichanganyike weka soda ash koroga weka maji koroga vizuri hakikisha hakuna mabonge mabonge

Weka glycerine, formaline, perfume, rangi na chumvi kisha koroga kwa dakika 15.

Paki kauze

ANGALIZO
SULPHONIC ACID IPO KAMA ASALI WEKA MBALI NA WATOTO MAANA NI KEMIKALI HATARI.

ASANTE

-QUEEN___
Kuifanya iwe bora kabisa kwa mahtaji binafsi na sio ya biashara unafanyaje kwa uoande wa ratio yani iwe kama ilivyo Harpic kwa mfano.
 
Back
Top Bottom