Salamu wana Jamvi!
Uvimbe katika mfuko wa uzazi ama kwa kitaalamu ndio huitwa Fibroids.
Dalili za kusumbuliwa na uvimbe katika mfuko wa uzazi ni;
Uvimbe katika kizazi cha mwanamke ukiwa mdogo unaweza usiwe na dalili zozote na dalili hutegemea sehemu ulipo kwenye mfuko wa uzazi na pia ukubwa wake.
Dalili kubwa ya ugonjwa huu mara nyingi ni kutokwa damu nyingi kwa muda mrefu wakati wa hedhi ikiambatana na mabonge mabonge isivyo kawaida, au kutokwa damu isiyo ya kawaida katikati ya mwezi au hedhi zisizokuwa na mpango.
Dalili nyingine ni kupata maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi, kutokana na ugonjwa kubana viungo vingine vya mwili (pressure symptoms). Mtu anaweza kupata maumivu makali ya tumbo, maumivu wakati wa tendo la ndoa, maumivu ya mgomgo na kukojoa mara kwa mara kwani uvimbe hukandamiza kibofu cha mkojo.
Pia fibroid inaweza kusababisha kutotunga mimba au mimba kuharibika na kutoka, na wakati mwingine ugumba.
Tatizo la uvimbe katika kizazi mara nyingi huambatana na maradhi mengine. Maradhi hayo ni kama, upungufu wa damu, kufunga choo, matatizo ya figo na mara chache huweza kuwa saratani. Pia uvimbe wa fibroid unapokua mkubwa unaweza kusababisha dalili zifuatazo, mkojo kubaki kwenye kibofu, haja kuwa ngumu, miguu kuvimba na kupungukiwa damu.
Habari njema kwa ndugu zetu wanaosumbuliwa na Uvimbe katika mfuko wa uzazi (Fibroids) ama uzazi kwa maana ya uwezekano mdogo wa kupata mtoto.
Picha kuonyesha uvimbe katika mfuko wa uzazi
Jibu ni matumizi ya mti wa “Ficus sansibarica” na uzuri ni kwamba mti huu unapatikana katika ukanda wa afrika mashariki na kati ikiwemo Tanzania.
Mti wa Ficus Sansibarica
Sehemu inayotumika kwa utabibu huu ni tini (figs) ambayo huweza kutumika kama “Tonic” kwa wanawake
Figs za Ficus Sansibarica
Itaendelea ....!