Hii hali si ya kawaida.Nimeshashuhudia na kusikia wanawake wengi sana wakisumbuliwa na uvimbe wa tumbo pamoja na tumbo kutoa usaha pindi wakifanyiwa upasuaji.
Idadi imekuwa kubwa mno mpaka nimeona nije kuleta hii mada humu jamii forums tuweze kupata ufumbuzi.
Mfano mzuri ni huyu muigizaji wa bongo dar es salaam anayeitwa Carina amefanyiwa upasuaji mara tano na tumbo lake linatoa usaha tu na mpaka sasa bado hajapata nafuu.
Pia nilivyosikia hii hali ikiendelea kwa muda mrefu inapelekea kansa.
View attachment 1548854