Mimi nimeolewa mwaka wa nne sasa. tangu nilipofunga ndoa niligundulika kuwa nina uvimbe na nikaambiwa na madaktari kuwa lazima nifanyiwe operation na kutolewa kizazi. sina mtoto hata mmoja hivyo nikakataa kufanya hiyo operation. Nimejaribu kila dawa imeshindikana. Naomba msaada wenu nifanyeje ndugu zangu. Naona maisha yanakuwa kitendawili sasa.
Last week shemeji alilazwa Aghakan kwa ku-breed mfulilizo hadi damu ikapungua mwili na akagundulika ana Uvimbe (fibroid), ushauri wa daktari bingwa anaitwa Dr Shafiq ni huu: Akamwuliza mna watoto wanagapi? shemeji akajibu wa3,kama mnataka kuongeza mwingine ni vizuri mkafanya hivyo hili tatizo la kutoka damu litasimama kwa muda kwani hakuna MP wakati wa ujauzito baadae mtakuja niondoe kizazi,shemeji na mumewe wakajadili na kukubaliana ya kuwa watoto wametosha ni bora atolewe kizazi awe na afya bora alee watoto vizuri,sasa unaposema kutopata mimba kunasababishwa na huo uvimbe sielewi maana moja ya solution ya kutuliza kwa muda ugonjwa huo ni kubeba mimba.