Utetetezi wa Sabaya, haupo kisheria, na pia unavunja kanuni za Kijasusi

Binafsi sitashañgaa kuona hilo likitokea kwani kwao hiyo ilishakuwa ni sera ambayo inatekelezwa na wanajua jinsi ya kulindana.
 
Sabaya aliwahi kushitakiwa kwa kosa la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa.

Na wakati huo alikuwa mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha.

Sasa ukiniambia Sabaya ni jasusi, ninapata mashaka kwamba inakuwaje jasusi ashitakiwe kwa kujifanya jasusi?
 
Hakuna kesi ni ujinga tu, sabaya tangu mwezi wa 4 anasakamwa. Na wanajua alikuwa akipewa order kama mojawapo ya majukumu. Hawakustahili kumdhalilisha kiasi kila wakati wanajua alifanya majukumu aloagizwa

Ilibidi wamlinde maana kwa sisi tunaojua siasa kila uongozi lazima watu wachache waumie wengi wapone.
Sabaya kutumwa na rais sio dhambi ilo wazi hata ungekuwa wewe ungemtuma akusaidie kazi.kisiasa hii inaeleweka wala aliemtuma yupo sahihi.
Urais ni taasisi je hawakujua hilo? Of cause walijua sana. Sasa ndo ujuwe magufuli alikuwa akichukiwa bila yeye kutambua. Yaani sasa hivi ni kama kukomoa.
Sabaya ametaja baada ya kuona hakuna msaada.kipindi hiki chote alikuwa kimya alivyoona hakuna anaemsaidia akaongea...
Najua ataumia na wenda baabae...................

Kwa sasa hana chaguo hata mimi ningefanya hivyo.
Ni mapito tu hata awamu zilizopita hapa.mambo yalikuwepo.
 
Sio enzi ya mwendazake tu lakini si kila kitu anachoarifiwa Rais na makamo lazima aambiwe! Yako mengi sana makamo huwa hawaambiwi na sio Tanzania tu bali duniani kote.
Ni sawa mkuu lakini sio katika mambo muhimu hasa ya usalama wa nchi...Angalia Kenya kwa mfano hakuna kitu atachokifanya Kennyatta na Rutto asijue( Mambo muhimu ya nchi). Tatizo letu Tanzania tulijisahau kuwa Makamu ndiye Rais number mbili na ndio maana walikuwa wanapewa saana wale wenzetu pale jirani kama kuwatuliza kuacha kelele za kudai nchi yao. Tumekujakustukia sasa hivi.
 
Nakuambiaje acha hakuna kitu anafanya Kenyata eti Ruto asijue! Vyombo vya ulinzi na usalama vyote vinareport kwa Kenyata sio Ruto! Ruto anaweza kuambiwa ila si lazima yote anayoambiwa Kenyata.
 
hakuna kesi hapo.
kama alikuwa anatekeleza majukumu yake aliyo elekezwa na aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu ktk kuhakikisha kodi ya Serikali inalipwa. sasa huo unawezaje kuuita eti ni unyang'anyi?!!
ukiangalia hii kesi kwa jicho la tatu imejaa kisasi dhidi ya sabaya kutokana na majukumu yake aliyo kuwa akiyatekeleza, kwa vyovyote vile lazima angechukiwa sana na either;
1. wafanyabiashara au wanasiasa au wote kwa pamoja. ndicho kilicho tokea.
 
aise kweli selo mbaya
kachanganyikiwa huyu sio bure na naamini huyu sio kitengo huyu..

Jambaz
 
 
Kwamba sabaya,magufuli,na mpango waliunda genge la kijambazi la kuua kutesa na kupora watu Mali zao!!
 
Hapo kwenye special mission ndio ukweli wenyewe, beba lawama baadae utakumbukwa.

Kuna wale walimuua "jambazi" mmoja baadae ikaonekana alikuwa mkurugenzi wa taasisi nyeti. Sijui kilichotokea, lakini walipunguziwa adhabu kutoka kwa Bwana Mkapa, wakatoka wakati wa Kikwete
 
Na nusu mshahara bado inaingia kila mwezi. Akishinda kesi hela zetu za miamala zitamlipa fidia.
 
Uzuti hii kesi inaenda mbio sana tusubiri mawakili wa upande Jamhuri waki cross ....pia demand ushahidi
 
Basi maandalizi yake yalikuwa na mashaka sana.

Hakuwahi kufundishwa kwamba kuna kutolewa sadaka, na mambo yakiharibika you are on your own. Kama kweli alitumwa which is likely ni kweli, kwa nini taasisi zile zile zinamtesa? Kuna uwezekano mkubwa alikuwa anavuka mipaka na akatengeneza maadui wengi, walikuwa wanasubiri sponsor aondoke wamshushie rungu.

Either way, alikuwa mpumbavu aliyelewa power. Hii nchi kila mwenye "kazi maalum" angekuwa kama yeye, hali ingekuwa mbaya sana.
 

Katika makosa kuna kufanya kitu kinaitwa kosa kwa public interest. Kwa mfano, wakati anakamata mashine ya kutengenezea fedha haramu, ingetokea purukushani akajeruhi mtu, kujeruhi ni kosa, lakini asingekuwa pinpointed yeye mwenyewe, na Identity yake wakati wa hilo zoezi, haikuwa sabaya.

Inapotokea kwenye missiona kama hizo, amekwenda kukamata mitambo ya fedha, halafu akaanza kubaka kwa mfano, hiyo ni personal offence, na kama anageshitakiwa kwa kubaka, hapo utetezi wa kwamba alikuwa kazini ni null and void, kwa kuwa hakuwa ametumwa kwenda kubaka, na kubaka hakukuwa na uhusiano wowote wa kumsaidia akamlishie kazi yake.

Alitumwa kuwakamata waharifu, na kukamata uharifu, hiyo ndiyo JD yake. Habari za kuenda kupigia watu makele usiku kucha na kudai mamilioni ya fedha kwa wafanya biashara nako alitumwa na nani?



Ni lazima watu watambue mipaka ya kazi. Ujambazi si sehemu ya kazi na hivyo haiwezi kuwa utetezi.

Hata hivyo ninaona Sabaya anachengesha. Haongelei jinai zake, badala yake anakimbilia kusema matukio rasmi aliyokuwa anafanya kazi halali za kukamata wafua noti bandia. Lakini hakuna kesi inayohusu kosa lake la kukamata mitambo ya fedha kwa kuwa hiyo ilikuw akazi halali. Aongelee tuhuma zile zingine kama nazo alitumwa na nani?

ULEVI NA KIBURI CHA MADARAKA VINA MWISHO. HERI MTU YULE AMBAYE BWANA NI KIMBILIO LAKE. MAANA HATAONDOSHWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…