Utetetezi wa Sabaya, haupo kisheria, na pia unavunja kanuni za Kijasusi

Utetetezi wa Sabaya, haupo kisheria, na pia unavunja kanuni za Kijasusi

Walitakiwa wamshitaki kwenye mahakama ya kijeshi lakini wamefanya kosa mamlaka kumpeleka kwenye mahakama ya kiraia huku wanasiasa wakiruhusiwa kumkejeli wakati mamlaka wakijua kwamba kile alichokuwa akikitekeleza kiliidihinishwa na wao kwahiyo hapo hakuna cha kutunza siri tena. Tambua usalama wako tayari kwa lolote watakalo kabiliana nacho wakati wakitekeleza majukumu waliyotumwa siyo kwa mtindo walioamua mamlaka kumdhalilisha kisa kuwafurahisha watu fulani ambao hata hivyo hazingatii kama kuna haki yoyote inatendwe.

Mamlaka za uteuzi huwa hazifi ila mtu hufa.....shughulikeni na mamlaka ya uteuzi ambayo bado ipo pamoja na kwamba mtu kabadilika.

Rejea "Rais Hakosei"-SSH ila mtumwa ndio hukosea!!!! Maajabu ya DUNIA ya SABA


Sasa hatambuliki Kama yeye ni TISS au Mwanajeshi atapelekwaje huko??
 
Kwamba sabaya,magufuli,na mpango waliunda genge la kijambazi la kuua kutesa na kupora watu Mali zao!!
Sabaya was a typical crook,blackmailer hata kabla ya kupewa u DC.
Huko nyuma alikuwa anawatishia watu kuwa ni TISS,hadi akakamatwa na kitambulisho fake cha TISS na kufunguliwa mashtaka akiwa mwenyekiti wa mkoa wa UVCCM Arusha.
Magufuli alifanya terrible blunder ya kumshirikisha Sabaya katika kazi chafu,sasa ameanza kuilambisha mchanga serikali ya CCM. Akifungwa na akiamua kutunga kitabu cha madhambi ya serikali awamu ya tano ...........
 
Sabaya aitakuwa alitumwa na mamlaka, lakini ninalo liona hapa, Sabaya sio sehemu ya ile mamlaka.

Sabaya alitumika tuu kufanikisha kazi za mamlaka;
Mosi, kwa kuwa alikuwa katika nafasi ya kufanya hivyo kwa nafasi yake ya kisiasa.

Pili, alikuwa na sifa za kuweza kufanya hiyo kazi, na ilikuwa na sehemu ya kazi chafu za mamlaka.

Sasa, sabaya alifanya kazi na sehemu kubwa ya waliomtuma hawapo tena, waliopo nao hawako tayari kumtetea Sabaya kwa Boss mpya.

Hivyo, ushahidi wa sabaya amefanya makusudi kuwataka magufuli ambaye hayupo, ila kamtaja mpango na Gavana wa BOT.

Na akaenda mbele zaidi kusema ana siri zingine hawezi kusema kwa sababu alishakula kiapo ( yawezekana hakuna hata siri) , ila anafanya hivi ili wao ndio wamnasue
Kitanzini.

Sabaya na mawakili wake sio mafala watoe ushaidi ambao ni kama anakiri kosa.


Transcend, 2021.
 
... Sabaya kuwemo kwenye Mfumo wa ujasusi wa nchi hii haina mashaka! Toka enzi akiwa mtoto UVCCM aliwahi kukutwa na kitambulisho cha TISS kesi ikafunguliwa. Alivyoachiwa ni mamlaka yake ya uteuzi pekee ndio inajua.

In short, ameandaliwa kwa kazi maalum long time so yanayotokea kwenye sakata hili ni long time plan. Alichokisema mahakamani ni sahihi kabisa.
Acha kunchanganya usalama wa chama na usalama wa nchi,
Ni vitu viwili tofauti Pamoja Hawa wa chama wanatabia ya kufosi.
 
Bibi anafanya anachokijua ktk hii ishu spinning nje nje na character assasination ndo target ya bibi. Lakini, jpm atabaki ni jpm na hawatafanikiwa kamwe kumpaka vinyesi vyao vya magogoni/msoga.


Sasa Sebaya ndio keshamuingiza JPM katika Uhalifu alioufanya, na ikithibitika ni kweli alikuwa ameagizwa huoni Kama JPM atakuwa amechafuka na zile nadharia zote kipindi akiwa hai zitakuwa zimepata ushahidi wa wazi
 
Huyu kijana ni kuwa ni Tis Lakini anachopungukiwa namna operation zake alivyokuwa akizifanya mbona wengine wanatekeleza majukumu mazito na hakuna anaejua,, Kwanza ni upumbavu kujulikana hadharani kuwa wewe ni Tis, Kwanza Mfano mtu Kama Mahiga alikuwa anafahamika kwa sababu yeye aliwahi kuwa Mkuu wa kile kitengo,, kwa huyu jamaa hafai hata akina Samia na mpango wanafahamu ila wanajifanya hawajui

😃😃😃
 
Ni wasioelewa tu wanaoweza mlaumu Sabaya Kwa utetezi wake , na ni ukweli mamlaka zilimtuma , hakufanya uhalifu alitekekeza majukumu aliyoagizwa na ushahidi upo.

Rais kumfukuza kazi Sabaya na kuruhusu kudhalilishwa kwake huku akijua ofisi yake inahusika moja Kwa moja ilikuwa wrong move....Sabaya shikilia hapo hapo.
Ridia ulichokiandika. Google utafute ukweli from decided cases on similar issues raised by Sabaya
 
Kszi maalumu wanamahakama zao..

Ndio maana maelezo yake yanaonekana Kama porojo,
Hajui wapi pakusema nini.

Kama angekuwa kitengo Kama maelezo yake yanavyomtambulisha, kwamba alipewa kazi maalumu na Mkuu aliyemteua, asingetoa maelezo ya hivyo kwenye Mahakama kuu ya kiraia ilhali anajua kuna Mahakama zao
 
Mambo ni Moto

Katika sakata linaloendelea linalomkabili Ndugu Lengai Ole Sabaya, utetezi wake unaacha watu midomo wazi.
Mimi sio mwanasheria lakini Kwa akili ndogo tuu niliyonayo namuona Ole Sabaya na mawakili wake wakishindwa kutoa utetezi wenye mantiki.

Utetezi wa Sabaya kuwa alitumwa na Wakuu wake wa kazi waliomteua kufanya Uhalifu ni utetezi wa kijinga Sana ambao mtu mwenye akili asingeweza kuusema Mahakamani.
Kusema alitumwa ni dhahiri anakiri kosa kuwa alifanya, na moja Kwa moja anajitia hatiani.

Ole Sabaya Kiujasusi tayari ameshakosa Weledi katika Kazi yake. Anaposemwa alitumwa na Rais Magufuli ambaye Kwa sasa ni Marehemu, Kwa kazi maalumu, hii inamaanisha kuwa Sabaya yupo katika mfumo wa ujasusi iwe direct au indirectly.
Hivyo Jambo la kwanza kwenye majukumu yake lilipaswa kuwa Siri ndipo mengine yafuate

Moja ya kanuni za kazi maalumu ni siri, hasa kazi maalumu/operations zisizokuwa na majina na zisizoundwa kisheria.
Operations ambazo hazifuati kanuni Rasmi, ni unapigiwa simu na unatekeleza.

Operations za hivi, anayetumwa anapaswa azifanye Kwa weledi pasipo kuleta athari mbaya ambazo zitamtia hatiani, kwani zimtiapo hatiani yeye ndiye atahusika 100% katika adhabu.

Kijasusi, mtu anapopewa kazi maalumu hata akikamatwa hapaswi kusema ukweli kuwa alitumwa na wakubwa wake, hapaswi kuwataja waliomtuma, anapaswa kutumia mbinu zingine za kujihamu au kuficha siri.

Sabaya Kama alitumwa na Hayatti Magufuli, hii ilimaanisha taasisi ya Urais ilikuwa inajua misheni hizo, hivyo hakupaswa ajitetee kuwa alitumwa na Rais kufanya Uhalifu kwani Kwa kufanya hivyo anamdhalilisha Hayatti Magufuli na Taasisi ya Urais ya wakati huo.

Kama ni kweli alitumwa, basi angekaa kimya na kujitetea Kwa namna zingine, alafu Kwa vile alitumwa na taasisi ya Urais, basi mabosi wake Kwa vile wengine wapo na wanatambua misheni hiyo, wangetafuta namna ya kumnasua. Lakini sio kuwataja, Kwa kuwataja ni tayari ameshavujisha Siri pasipo yeye kujua.

Sabaya pasipo kujua, kauli yake unazidi kuwapa nguvu Wale wote waliokuwa wakiituhumu serikali na watu wasiojulikana.

Kwa kifupi, Sabaya amekosa Weledi.

Hata Kama akitoka basi tayari ameshavujisha Siri za wakubwa wake, na Hana sifa za kuwa mtu wa vitengo Kwa mambo ya kiusalama.

Ilimpasa afe kiume. Akaze Tai shingoni.Mabosi zake ndio wamnasue. Lakini utetezi wake bado unamuweka pagumu zaidi.

Robert Heriel
Hao ndiyo watu walioingizwa kitengo bila mafunzo wala uzoefu wa kazi.
Mtu anabwabwaja kuwa yeye ana kazi maalum na ana flash kitambulish cha UWT ovyo.
Hao watu wamelalamikiwa sna na wako wengi.
Wanawatia aibu hata Proffessional Intelligence Officers waliofunzwa na kupikika.

\lakini wananchi tunajua kuwa Magufuli is partly to blame kwa kuidhalilisha proffession ya Intelligence, yeye alikichukulia kitengo kuwa idara ya visasi na coercion.
Intelligence ni proffession ambayo si tu infundishwa kwa miaka bali ina practicals ambazo ni za kiuhalisia zinafanyika leaving no trace.

Huyu Sabaya alikuwa kama Boy Scout, sasa anabwabwaja ovyo kuwa alipelekwa kazi hizo na Mgufuli, Mpango na Gavana wa BOT.
What a shame.
 
Yaani ati umetumwa kuua alafu unakamatwa unasema nimetumwa kuua. Hivi hata mtoto mdogo si atakushangaa Kwa ujinga.

Hata Kama umetumwa kazi na mkuu wako, ukaioa jina kazi maalumu na ambayo kimsingi huenda ni Uhalifu lazima utumie akili kuitenda, na ukishikwa utakayewajibika ni wewe 100% .

Sasa hawa ndugu zetu wanakuambia Kwa vile katumwa ataachiwa, inashangaza kweli
Ni mjinga tu ndiye ataelewa huu upuuzi. Kama alitumwa kweli, kwa nini Hakuwapa huo ushahidi wapelelezi wakajiridhisha na kumfutia mashtaka kabla ya kumpeleka mahakamani.....!!?
 
Ni mjinga tu ndiye ataelewa huu upuuzi. Kama alitumwa kweli, kwa nini Hakuwapa huo ushahidi wapelelezi wakajiridhisha na kumfutia mashtaka kabla ya kumpeleka mahakamani.....!!?


Kusema hivyo moja Kwa moja ni kuichafua serikali iliyopita. Sijajua yote haya mwisho wake utakuwaje Ila kama atathibitisha atazidi kuwapa nguvu Wale waliokuwa wakimsema JPM
 
Yaani ati umetumwa kuua alafu unakamatwa unasema nimetumwa kuua. Hivi hata mtoto mdogo si atakushangaa Kwa ujinga.

Hata Kama umetumwa kazi na mkuu wako, ukaioa jina kazi maalumu na ambayo kimsingi huenda ni Uhalifu lazima utumie akili kuitenda, na ukishikwa utakayewajibika ni wewe 100% .

Sasa hawa ndugu zetu wanakuambia Kwa vile katumwa ataachiwa, inashangaza kweli
... sisi tunangoja ushahidi tuu, yaani alete kimemo au clip ya simu aliyopigiwa na MKULU!
1628953955783.png
 
Back
Top Bottom