Utetetezi wa Sabaya, haupo kisheria, na pia unavunja kanuni za Kijasusi

Utetetezi wa Sabaya, haupo kisheria, na pia unavunja kanuni za Kijasusi

kaka kuna kitu hujakielewa hapa . Tatizo kubwa lilokuwepo katika Serikali ya Mwendazake ni kama vile nchi haikuwa na Makamu wa Rais. Kazi zake zilikuwa ni kupokea wageni wa Mheshimiwa tu kazi nyingine alikuwa anarukwa ndio maana unaona hakuna connections kati ya utawala uliopita na wa sasa
Lakini TISS si ni wale wale
 
Sebaya Kama alitumwa na Hayatti Magufuli, hii ilimaanisha taasisi ya Urais ilikuwa inajua misheni hizo, hivyo hakupaswa ajitetee kuwa alitumwa na Rais kufanya Uhalifu kwani Kwa kufanya hivyo anamdhalilisha Hayatti Magufuli na Taasisi ya Urais ya wakati huo.
Anamdhalilisha au walijidhakilisha kuongoza nchi kihalifu Mshana Jr ?!
 
Hakuna kesi ni ujinga tu, sabaya tangu mwezi wa 4 anasakamwa. Na wanajua alikuwa akipewa order kama mojawapo ya majukumu. Hawakustahili kumdhalilisha kiasi kila wakati wanajua alifanya majukumu aloagizwa

Ilibidi wamlinde maana kwa sisi tunaojua siasa kila uongozi lazima watu wachache waumie wengi wapone.
Sabaya kutumwa na rais sio dhambi ilo wazi hata ungekuwa wewe ungemtuma akusaidie kazi.kisiasa hii inaeleweka wala aliemtuma yupo sahihi.
Urais ni taasisi je hawakujua hilo? Of cause walijua sana. Sasa ndo ujuwe magufuli alikuwa akichukiwa bila yeye kutambua. Yaani sasa hivi ni kama kukomoa.
Sabaya ametaja baada ya kuona hakuna msaada.kipindi hiki chote alikuwa kimya alivyoona hakuna anaemsaidia akaongea...
Najua ataumia na wenda baabae...................

Kwa sasa hana chaguo hata mimi ningefanya hivyo.
Ni mapito tu hata awamu zilizopita hapa.mambo yalikuwepo.
watu wengine huwa wanaropoka tu bila kuzama kiundani kuhusu kitu ,unaambiwa alibaka wake za watu hotelini ,alipiga na kuteka watu ,aliiba hela .... tuyaachw yote ayo ila kubakiwa mke wako huku unaona acheni upuuzi ...huyo jamaa alitumwa kubaka watu, kama alipokea maagizo toka juu naamini hayakuwa yakubaka ....acha afungwe acheni useng#
 
Ni wasioelewa tu wanaoweza mlaumu Sabaya Kwa utetezi wake , na ni ukweli mamlaka zilimtuma , hakufanya uhalifu alitekekeza majukumu aliyoagizwa na ushahidi upo.

Rais kumfukuza kazi Sabaya na kuruhusu kudhalilishwa kwake huku akijua ofisi yake inahusika moja Kwa moja ilikuwa wrong move....Sabaya shikilia hapo hapo.
Kwani Rais aliyemtuma si alishakufa tayari utasemaje anamuacha adhalilike wakati hayupo duniani tena.
 
Ni wasioelewa tu wanaoweza mlaumu Sabaya Kwa utetezi wake , na ni ukweli mamlaka zilimtuma , hakufanya uhalifu alitekekeza majukumu aliyoagizwa na ushahidi upo.

Rais kumfukuza kazi Sabaya na kuruhusu kudhalilishwa kwake huku akijua ofisi yake inahusika moja Kwa moja ilikuwa wrong move....Sabaya shikilia hapo hapo.
Kweli ashirkirie hapo hapo hadi gerezani asiachie.karibu kisongo

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
... Sabaya kuwemo kwenye Mfumo wa ujasusi wa nchi hii haina mashaka! Toka enzi akiwa mtoto UVCCM aliwahi kukutwa na kitambulisho cha TISS kesi ikafunguliwa. Alivyoachiwa ni mamlaka yake ya uteuzi pekee ndio inajua.

In short, ameandaliwa kwa kazi maalum long time so yanayotokea kwenye sakata hili ni long time plan. Alichokisema mahakamani ni sahihi kabisa.
Unachekesha kweli kweli

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Sebaya Kama alitumwa na Hayatti Magufuli, hii ilimaanisha taasisi ya Urais ilikuwa inajua misheni hizo, hivyo hakupaswa ajitetee kuwa alitumwa na Rais kufanya Uhalifu kwani Kwa kufanya hivyo anamdhalilisha Hayatti Magufuli na Taasisi ya Urais ya wakati huo.
Hakuna taasisi ya Urais wa wakati huo. Taasisi ya Urais ni ile ile ingawa inapata viongozi tofauti. Hiyo taasisi ndio huwajibika kwa kila jema na baya la Rais wa nchi. Rais hapangi mambo mwenyewe, kuna channels na hizo hazikufa na JPM!

Hizo channel zinajua kila alichokuwa anafanya Sabaya, ila seems imekuwa handled recklessly. Unapokuwa completely unsecured unapigania pumzi yako tu, ndicho anachofanya Sabaya! Haya mambo huko mbele yatakuja kuigharimu CCM.
 
Hata mimi nimeshangaa.
Hivi majasusi huwa wanatumwa kubaka watu na kuwaibia pesa?
Hakuna jasusi anaetumwa kubaka watu na kuwaibia, jasusi hawezi kutumwa kubaka (kwani afya yake ni kipaumbele)
Jasusi hawezi kutumwa kuwaibia watu bali huwezeshwa kwa kila kitu ambacho kitamsaidia kufanikisha task aliyotumwa.
 
Yaani ati umetumwa kuua alafu unakamatwa unasema nimetumwa kuua. Hivi hata mtoto mdogo si atakushangaa Kwa ujinga.

Hata Kama umetumwa kazi na mkuu wako, ukaioa jina kazi maalumu na ambayo kimsingi huenda ni Uhalifu lazima utumie akili kuitenda, na ukishikwa utakayewajibika ni wewe 100% .

Sasa hawa ndugu zetu wanakuambia Kwa vile katumwa ataachiwa, inashangaza kweli
Ndio maana wenzetu American, Russian and likewise, jasusi anapopangiwa kazi kama ya kuua, basi nyuma yake kuna jasusi mwengine kwa ajili ya kumfatilia mwenendo wake, na huyu anaefatilia mwenendo wa jasusi wa kwanza nae nyuma yake kuna mtu anaemfatilia, waweza kuwa hata watano. Na endapo wa kwanza akifanikisha mission bila kujulikana basi ameokoka yeye na waliopo nyuma yake na endapo akifeli basi kwenye mlolongo wa wote watano anaesalimika ni mwisho pekee.
 
Hakuna jasusi anaetumwa kubaka watu na kuwaibia, jasusi hawezi kutumwa kubaka (kwani afya yake ni kipaumbele)
Jasusi hawezi kutumwa kuwaibia watu bali huwezeshwa kwa kila kitu ambacho kitamsaidia kufanikisha task aliyotumwa.
yes kiufupi yule alikuwa muhuni tu kama muhuni mwingine.
Hiyo ya kukutwa na vitambulisho ilikuwa ni kiki ya ujana tu au usela mavi
 
Asome kitabu Cha Njama kilichoandikwa na Musiba atamwona WILLY GAMBA alivyokuwa akitekeleza majukumu yake katika operation zake,,Sabaya hakuiva kuwa TIS vijana hawa wanaiaibisha mamlaka
 
Mambo ni Moto

Katika sakata linaloendelea linalomkabili Ndugu Lengai Ole Sabaya, utetezi wake unaacha watu midomo wazi.
Mimi sio mwanasheria lakini Kwa akili ndogo tuu niliyonayo namuona Ole Sabaya na mawakili wake wakishindwa kutoa utetezi wenye mantiki.

Utetezi wa Sabaya kuwa alitumwa na Wakuu wake wa kazi waliomteua kufanya Uhalifu ni utetezi wa kijinga Sana ambao mtu mwenye akili asingeweza kuusema Mahakamani.
Kusema alitumwa ni dhahiri anakiri kosa kuwa alifanya, na moja Kwa moja anajitia hatiani.

Ole Sabaya Kiujasusi tayari ameshakosa Weledi katika Kazi yake. Anaposemwa alitumwa na Rais Magufuli ambaye Kwa sasa ni Marehemu, Kwa kazi maalumu, hii inamaanisha kuwa Sabaya yupo katika mfumo wa ujasusi iwe direct au indirectly.
Hivyo Jambo la kwanza kwenye majukumu yake lilipaswa kuwa Siri ndipo mengine yafuate

Moja ya kanuni za kazi maalumu ni siri, hasa kazi maalumu/operations zisizokuwa na majina na zisizoundwa kisheria.
Operations ambazo hazifuati kanuni Rasmi, ni unapigiwa simu na unatekeleza.

Operations za hivi, anayetumwa anapaswa azifanye Kwa weledi pasipo kuleta athari mbaya ambazo zitamtia hatiani, kwani zimtiapo hatiani yeye ndiye atahusika 100% katika adhabu.

Kijasusi, mtu anapopewa kazi maalumu hata akikamatwa hapaswi kusema ukweli kuwa alitumwa na wakubwa wake, hapaswi kuwataja waliomtuma, anapaswa kutumia mbinu zingine za kujihamu au kuficha siri.

Sabaya Kama alitumwa na Hayatti Magufuli, hii ilimaanisha taasisi ya Urais ilikuwa inajua misheni hizo, hivyo hakupaswa ajitetee kuwa alitumwa na Rais kufanya Uhalifu kwani Kwa kufanya hivyo anamdhalilisha Hayatti Magufuli na Taasisi ya Urais ya wakati huo.

Kama ni kweli alitumwa, basi angekaa kimya na kujitetea Kwa namna zingine, alafu Kwa vile alitumwa na taasisi ya Urais, basi mabosi wake Kwa vile wengine wapo na wanatambua misheni hiyo, wangetafuta namna ya kumnasua. Lakini sio kuwataja, Kwa kuwataja ni tayari ameshavujisha Siri pasipo yeye kujua.

Sabaya pasipo kujua, kauli yake unazidi kuwapa nguvu Wale wote waliokuwa wakiituhumu serikali na watu wasiojulikana.

Kwa kifupi, Sabaya amekosa Weledi.

Hata Kama akitoka basi tayari ameshavujisha Siri za wakubwa wake, na Hana sifa za kuwa mtu wa vitengo Kwa mambo ya kiusalama.

Ilimpasa afe kiume. Akaze Tai shingoni.Mabosi zake ndio wamnasue. Lakini utetezi wake bado unamuweka pagumu zaidi.

Robert Heriel
kesi hii ishaisha maana Sabaya amekiri kosa.
 
watu wengine huwa wanaropoka tu bila kuzama kiundani kuhusu kitu ,unaambiwa alibaka wake za watu hotelini ,alipiga na kuteka watu ,aliiba hela .... tuyaachw yote ayo ila kubakiwa mke wako huku unaona acheni upuuzi ...huyo jamaa alitumwa kubaka watu, kama alipokea maagizo toka juu naamini hayakuwa yakubaka ....acha afungwe acheni useng#
Kumbe unaambiwa? Nilijua ulikuwepo akibaka.umbea hausikilizwi mahakamani
 
Sabaya aliwahi kushitakiwa kwa kosa la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa.

Na wakati huo alikuwa mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha.

Sasa ukiniambia Sabaya ni jasusi, ninapata mashaka kwamba inakuwaje jasusi ashitakiwe kwa kujifanya jasusi?
Nadhani swala la msingi ulitakiwa uulize ni inakuaje kada wa chama anakuwa mwana usalama?
 
Hakuna kesi ni ujinga tu, sabaya tangu mwezi wa 4 anasakamwa. Na wanajua alikuwa akipewa order kama mojawapo ya majukumu. Hawakustahili kumdhalilisha kiasi kila wakati wanajua alifanya majukumu aloagizwa

Ilibidi wamlinde maana kwa sisi tunaojua siasa kila uongozi lazima watu wachache waumie wengi wapone.
Sabaya kutumwa na rais sio dhambi ilo wazi hata ungekuwa wewe ungemtuma akusaidie kazi.kisiasa hii inaeleweka wala aliemtuma yupo sahihi.
Urais ni taasisi je hawakujua hilo? Of cause walijua sana. Sasa ndo ujuwe magufuli alikuwa akichukiwa bila yeye kutambua. Yaani sasa hivi ni kama kukomoa.
Sabaya ametaja baada ya kuona hakuna msaada.kipindi hiki chote alikuwa kimya alivyoona hakuna anaemsaidia akaongea...
Najua ataumia na wenda baabae...................

Kwa sasa hana chaguo hata mimi ningefanya hivyo.
Ni mapito tu hata awamu zilizopita hapa.mambo yalikuwepo.
Sasa unakubali kwamba magufuli alikua muuaji na jambazi? Kama sio kwann amtume sabaya kufanya mauaji na ujambazi?
 
Back
Top Bottom