Utetezi juu Ya TISS; Jee Wanaoitetea wanajua Tofauti ya TISS ya Nyerere na TISS ya Kikwete

Utetezi juu Ya TISS; Jee Wanaoitetea wanajua Tofauti ya TISS ya Nyerere na TISS ya Kikwete

Status
Not open for further replies.

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Nimemsikia Wassira akitetea TISS kuwa imefanya kazi nzuri sana na akakumbusha enzi za ukombozi kusini mwa Africa na haiwezi kun'goa watu kucha. Pia wabunge na mawaziri wengi wamekuwa wakirejea maneno hayo hayo katika kuitetea TISS.

Ninalotaka kujua hawa wanaotoa utetezi huo wanaelewa linalotuhumiwa na wapinzani? Wapinzani hawana wasiwasi na historia ya Idara ya Usalama wa Taifa na kazi nzuri zilizofanywa katika vipindi hivyo vya nyuma,lakini wanazungumzia utofauti wa utendaji ule wa weledi wa zamani na huu wa sasa.

Kwa nini Hawa CCM wanaitetea TISS kwa kutumia historia ya awamu zilizopita na sii kwa utendaji wa sasa? Au hawaelewi hata ni lipi wanalisemea?
 
tukiendelea kuwachekea majimboni wanaotetea maovu ya TISS na ukandamizaji kwa maslahi ya chama tawala tunaumia wapiga kura bila kujali itikadi,tathmini za wabunge wa ccm ni kutetea chama japo wachache tofauti,dawa yao kuwakataa especialy nchemba,serukamba
 
Kuna tofauti sana ya Mwalimu Nyerere ilikuwa inafanya kazi na kuwa tumikia Wa Tanzania hihi ya Mr fast jet inapambana na wananchi wake mfano kung'oa watu kucha ,meno macho bila ganzi
 
Enzi za mwalimu TISS aliyejulikana ni yule atakayepewa wilaya / mkoa na ngazi zingine za juu lakini wengine wote walikuwa hawajulikani na utakuta hata ndani baba hajui kuwa mkewe ni TISS. lakini wa leo nenda wilaya yeyote halafu uliza watumishi wakuorodheshee kama hawajakupa list yote mpaka huwa wanapumzika wapi wakivizia taarifa za wapinzania.
Hata kariakoo sokoni ukipita na ukiuliza makuli wanakwambia mbona ni fulani na fulani
 
TISS ya enzi za JK Nyerere ilikuwa na weledi wa utendaji wa kazi na pia ilikuwa inaheshimu sana raia wake. Ililinda maslahi ya nchi kwa faida ya taifa lote. Kifupi tu TISS ya mwalimu Nyerere ilipenda sana raia wake hivyo haikuwa na haja ya kuwafanyia ukatili wa kinyama kama hii ya sasa inavyowafanyia raia wake. TISS ya sasa kwanza imekosa kabisa imani ya wananchi.

TISS ya sasa ni kama chombo cha kufanyia umafia kwa serikali ya chama tawala. Inatumika vibaya sana kuua demokrasia na uhuru wa kutoa mawazo. Inasikitisha sana chombo hiki muhimu sana katika ustawi wa taifa kinatumika kama chombo cha kufanyia uhalifu wa kibinadamu. Kwa sasa si sifa na heshima kubwa kufanya kazi katika chombo hiki kwani raia wema wanaona kama ni genge la kukandamiza demokrasia na uhuru wa kutoa maoni ambayo ni haki kikatiba.

Kwa kweli inasikitisha sana kuona hadhi ya chombo hiki inaporomoka namna hii. Ifike wakati hiki chombo kijisafishe na kuachana na kufanya kazi ambazo zinakitia aibu kwa umma wa watanzania. Bado watanzania wana imani nacho kwani ni chombo muhimu sana kikitumika vizuri. Hiki ndicho chombo muhimu kinachotulinda na maadui wanaoitazama vibaya nchi yetu.

Nalaani vitendo vya kigaidi na viovu vinavyofanywa na maafisa wachache wasiojua uthamani wa chombo hiki. Pia natoa nasaha zangu kwa viongozi wa kitaifa wakiache hiki chombo kiwe huru kufanya kazi zake zilizoainishwa kisheria bila kupewa maelekezo ambayo yanapelekea chombo kufanya kazi zisizo na manufaa kwa taifa. Mwisho kabisa nawaomba ndugu zangu watanzania tuwe na ustahamilivu kwani jambo la amani ya nchi yetu sio la mzaha kabisa.
 
Nyie mtapiga kelele usiku mtalala
Idara ya usalama wa taifa, haina tatizo na mtu isipokuwa kama huyo mtu anahatarisha usalama wa nchi, mfano mtu anasema "nchi hii haitatawalika"
Unategemea mtu kama huyo anaetaka kuhatarisha amani ya nchi aachwe tu? Lazima TISS wapige hodi mlangoni mwako,
Stephen Masatu Wassira:
 
Nimemsikia Wassira akitetea TISS kuwa imefanya kazi nzuri sana na akakumbusha enzi za ukombozi kusini mwa Africa na haiwezi kun'goa watu kucha. Pia wabunge na mawaziri wengi wamekuwa wakirejea maneno hayo hayo katika kuitetea TISS.
Ninalotaka kujua hawa wanaotoa utetezi huo wanaelewa linalotuhumiwa na wapinzani? Wapinzani hawana wasiwasi na historia ya Idara ya Usalama wa Taifa na kazi nzuri zilizofanywa katika vipindi hivyo vya nyuma,lakini wanazungumzia utofauti wa utendaji ule wa weledi wa zamani na huu wa sasa.
Kwa nini Hawa CCM wanaitetea TISS kwa kutumia historia ya awamu zilizopita na sii kwa utendaji wa sasa? Au hawaelewi hata ni lipi wanalisemea?

mkuu nini unachokielewa kuhusu tiss kama siyo maneno ya kuokota ndiyo unayotuambia uaweza kubainisha namna tiss ya nyerere na ya jk inavyofanya kazi mkuu acha kutuletea nadhalia tunataka fact mkuu siyo maneno.
 
Utofauti wa TISS
Enzi za Mwalimu @ TISS kulilinda taifa na watu wake.
Enzi za Dogo wa bongo flava @ TISS kuliangamiza taifa na watu wake.

mkuu mawazo yako yamechuja kweli angalia na huyo mtoto usimlandishi akili yako make itakuwa kazi make hoja yako haina hoja ndani yake.
 
Nimemsikia Wassira akitetea TISS kuwa imefanya kazi nzuri sana na akakumbusha enzi za ukombozi kusini mwa Africa na haiwezi kun'goa watu kucha. Pia wabunge na mawaziri wengi wamekuwa wakirejea maneno hayo hayo katika kuitetea TISS.
Ninalotaka kujua hawa wanaotoa utetezi huo wanaelewa linalotuhumiwa na wapinzani? Wapinzani hawana wasiwasi na historia ya Idara ya Usalama wa Taifa na kazi nzuri zilizofanywa katika vipindi hivyo vya nyuma,lakini wanazungumzia utofauti wa utendaji ule wa weledi wa zamani na huu wa sasa.
Kwa nini Hawa CCM wanaitetea TISS kwa kutumia historia ya awamu zilizopita na sii kwa utendaji wa sasa? Au hawaelewi hata ni lipi wanalisemea?

Wewe unajua kazi zinazofanywa na TISS? Au unashabikia tu porojo za CHADEMA na story za mitaani. Hamna mnalolijua kuhusu ueledi na kazi zinazofanywa na chombo hicho that is why mnabakia kutunga mambo ya uongo juu ya TISS kwakua mnajua hawana kawaida ya kujibizana na vyombo vya habari. Wewe hapo ulipo unaishi kwa amani na kufanya siasa zako za CHADEMA Kwa amani ila hujui hiyo amani imepatikanaje na inakua maintained vipi. Mtasema sana tuuuuu ila USILOLIJUA NI USOKU WA GIZA.... SHAME ON YOU!
 
Kuna tofauti sana ya Mwalimu Nyerere ilikuwa inafanya kazi na kuwa tumikia Wa Tanzania hihi ya Mr fast jet inapambana na wananchi wake mfano kung'oa watu kucha ,meno macho bila ganzi

Unaweza kuleta ushahidi wa hizo allegations? Au unashabikia tuu propaganda za chama chako cha CHADEMA???? SHAME ON YOU! HUNA UNALOLIJUA KUHUSU TISS HIVYO UTABAKIA KUAMINI POROJO ZA WAJINGA WENZAKO...
 
utofauti wa tiss
enzi za mwalimu @ tiss kulilinda taifa na watu wake.
Enzi za dogo wa bongo flava @ tiss kuliangamiza taifa na watu wake.

amakweli chadema imewakalia hadi kwenye vichwa vyenu... Unaweza kuthibitisha ni kwa vipi tiss inaangamiza taifa na watu wake??? Je unajua shughuli za tiss? Au unafata mkumbo tu> shame on you!
 
Napendekeza huu mjadala uwe topic ya kipimajoto ITV juma lijalo
 
tiss ya enzi za jk nyerere ilikuwa na weledi wa utendaji wa kazi na pia ilikuwa inaheshimu sana raia wake. Ililinda maslahi ya nchi kwa faida ya taifa lote. Kifupi tu tiss ya mwalimu nyerere ilipenda sana raia wake hivyo haikuwa na haja ya kuwafanyia ukatili wa kinyama kama hii ya sasa inavyowafanyia raia wake. Tiss ya sasa kwanza imekosa kabisa imani ya wananchi.

Tiss ya sasa ni kama chombo cha kufanyia umafia kwa serikali ya chama tawala. Inatumika vibaya sana kuua demokrasia na uhuru wa kutoa mawazo. Inasikitisha sana chombo hiki muhimu sana katika ustawi wa taifa kinatumika kama chombo cha kufanyia uhalifu wa kibinadamu. Kwa sasa si sifa na heshima kubwa kufanya kazi katika chombo hiki kwani raia wema wanaona kama ni genge la kukandamiza demokrasia na uhuru wa kutoa maoni ambayo ni haki kikatiba.

Kwa kweli inasikitisha sana kuona hadhi ya chombo hiki inaporomoka namna hii. Ifike wakati hiki chombo kijisafishe na kuachana na kufanya kazi ambazo zinakitia aibu kwa umma wa watanzania. Bado watanzania wana imani nacho kwani ni chombo muhimu sana kikitumika vizuri. Hiki ndicho chombo muhimu kinachotulinda na maadui wanaoitazama vibaya nchi yetu.

Nalaani vitendo vya kigaidi na viovu vinavyofanywa na maafisa wachache wasiojua uthamani wa chombo hiki. Pia natoa nasaha zangu kwa viongozi wa kitaifa wakiache hiki chombo kiwe huru kufanya kazi zake zilizoainishwa kisheria bila kupewa maelekezo ambayo yanapelekea chombo kufanya kazi zisizo na manufaa kwa taifa. Mwisho kabisa nawaomba ndugu zangu watanzania tuwe na ustahamilivu kwani jambo la amani ya nchi yetu sio la mzaha kabisa.

unaweza kuleta ushahidi kwamba tiss inatesa raia???? Au na wewe unaamini propaganda za chadema? Acheni kuzungumza mambo ya uongo dhidi ya chombo nyeti kama tiss. Tiss ndio uhai wa taifa... Ila sikulaumu kwakua wale jamaa kazi zao hatuzijui hivyo ni rahisi kuwasingizia na kusema lolote kwakua huwa hawana press conference ya kujibu tuhuma...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom