Utetezi juu Ya TISS; Jee Wanaoitetea wanajua Tofauti ya TISS ya Nyerere na TISS ya Kikwete

Utetezi juu Ya TISS; Jee Wanaoitetea wanajua Tofauti ya TISS ya Nyerere na TISS ya Kikwete

Status
Not open for further replies.
dr slaa ndo anaharibu vjana wake maana hata uwezo wao wa kufikiri umekufa. ndo maana hata mawazo yao yanapinda
 
Unataka utafuniwe? UWT=Usalama wa Taifa =TISS=Tanzania Intelligence Security System!!! hiyo W nimefanya upper case makusudi!! Khaaaaaaa!!! Omba mwongozo kwa spika!!

umebugi man, kwanza hatuna chombo kinachoitwa usalama wa taifa, bali tuna Idara ya Usalama wa Taifa. ukitafutia kifupi chake kwa kiswahili utachemka maana utaleta kitu kingine chenye tafsiri tofauti kama ulivyoingia chaka.
 
Nashukuru. nimejaribu kupitia wote waliojadili topic hii hadi sasa nimeona kuwa akina mbhulula ni 99% wenye uelewa wao hawajaingia, pindi wakifika watajua nilichoandika ni nini.
Kutukana siyo ILANI YA CHADEMA. bali ilani ya CHADEMA ni uchambuzi wa mambo kwa kina.
 
Maccm yalipo kuwa yakisema CUF ni chama cha waislam na CHADEMA ni chama cha kikristo muheshimiwa alikuwa busy anakula panadol lndia hakuyasikia sivyo?
 
[h=3]HEKO IDARA YA USALAMA WA TAIFA[/h]6:53 PM 3 comments
Na Happiness Katabazi

KATIKA mchakato wa mageuzi ambayo yamefanyika kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, mfumo wa sheria na siasa za nchi, taasisi za dola zimejikuta zikiwa nyuma wakati vuguvugu la mageuzi likienda mbele.


Moja ya tasisisi zilizokumbwa na fukuto hilo ni Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ambayo hapo awali, yaani chini ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Kwanza na ya Pili, ilikuwa ni taasisi ambayo haikutambulika kisheria kutokana na muundo wake kuwa wa siri na wa gizani mno.

Matokeo ya utendaji wa idara hiyo uliiletea sifa ya kuogopwa sana na kuonekana ni chombo cha majungu, chuki na wauaji wa wananchi wenye misimamo tofauti na watawala wa serikali hizo mbili zilizopita zilizoongozwa na hayati Rais Julius Kambarage Nyerere na Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi.

Maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wakiwa katika umbile la kiraia ni wanajeshi na; idara hiyo ni chombo nyeti katika uhai wa dola letu.

Ni kweli kiasili, chombo hiki hufanya kazi kwa taratibu za idara zote za usalama wa taifa na kamwe mwanasiasa hawezi kukitumia; hata hivyo mwanasiasa anaweza kumtumia ofisa wa idara hiyo kwa siri kitendo ambacho ni cha ukiukwaji wa maadili.

Nchi inapoingia kwenye matatizo, migogoro ya kisiasa, lawama kubwa huelekezwa kwa taasisi hii kwani ndiyo inayotambua, kubashiri na kutoa ushauri wa nchi inavyoweza kukabiliana na hatari zozote zile za kiusalama na kiulinzi.

Hapa Tanzania, mageuzi ya mwaka 1992 yaliyoanzisha mfumo wa vyama vingi na mabadiliko mengine ya kisheria na Katiba, yalisababisha kuundwa kisheria kwa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kutambulika rasmi kisheria hapa nchini kulianza mwaka 1996, baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa Na.5 ya mwaka 1996 na kutambulika rasmi kwa jina la Tanzania Intelligence and Security Services (TISS), ambapo kwa sasa idara hiyo inaongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Rashid Othman.

Cheo hicho cha Mkurugenzi Mkuu ni sawa na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi na Kujenga Taifa (CDF), David Mwamunyange, na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema.
Kwa mujibu wa sehemu ya nne ya sheria hiyo inayounda (TISS), kazi na mamlaka iliyonayo ni kukusanya habari, kuchunguza na kutathmini habari zote zinazohatarisha usalama wa taifa na hatimaye kuishauri serikali hatua muafaka za kuchukua kwa maslahi ya taifa.

Ni wazi kwamba idara hii imechangia kwa kiasi kukubwa kudhibiti na kuzuia matendo mengi ya kihalifu ambayo yametendeka au yanayotarajia kutendeka kwa kutoa taarifa mapema kwa Jeshi la Polisi na taasisi nyingine husika ambazo mwisho wa siku ndizo zimeshiriki na kufanikisha kushindwa kwa matukio ya kihalifu.

Hivyo hatuna budi kuipongeza TISS kwa kazi nzuri wanayoifanya; haiwezi kuonekana moja kwa moja na wananchi kwa sababu moja ya miiko ya kazi zinazofanywa na idara hii ni siri.

Na idara hii imenyang’anywa mamlaka ya kukamata wahalifu kwani enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere idara hii ilikuwa na mamlaka hayo chini ya ‘Detention Order’ yaani sheria ya kumuweka mtu kizuizini.

Kwa muktadha wa majukumu hayo, idara hiyo ilitakiwa ijiunde upya kutoka kwenye giza na usiri ili ifanye kazi kama chombo cha dola chenye majukumu ya kulinda amani, usalama na demokrasia. Kwa vyovyote vile idara hiyo haiwezi kufuta mfumo wa utaratibu wake wa kufanya kazi zake kwa siri kwa kuwa hiyo ndiyo namna pekee inayowezesha kupata taarifa na habari za kiusalama.

Lakini pia katika dola ya kidemokrasia lazima chombo hiki kivae umbile la uwazi katika utendaji kazi wake ili wananchi wakijue, wajue majukumu yake na waweze kushirikiana nacho pale inapobidi.

Kwa vyovyote vile usalama wa taifa unalindwa na kusalitiwa na wananchi ambao ndiyo wenye nchi; hivyo ni bora wakajua masuala mbalimbali yanayowazunguka.

Idara hiyo isipojijengea haiba ya kupendwa na wananchi, na hasa wazalendo, mwisho wa siku itajikuta inashindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kwa urahisi zaidi.

Hivi sasa lawama nyingi zinahusu kuibwa au kuporwa kwa rasilimali za nchi kunakodaiwa kufanywa na matapeli kwa kushirikiana na baadhi ya wawekezaji. Idara hii inaelekezewa lawama hizo, kuhujumiwa kwa uchumi wa nchi, kuuzwa kwa mashirika ya umma kwa bei chee na sasa mikataba mibovu mbalimbali ambayo dola imeingia na wawekezaji lazima ielekezwe kwenye idara hii. Kwa vyovyote vile kashfa ya ufisadi wa BoT, EPA na ombwe la viongozi bora lazima shutuma zielekezwe kwenye idara hii.

Kumbe basi wajibu wake si kama ilivyosadikiwa hapo zamani; yaani kuwa kazi kubwa ya maofisa wa idara hii ni kubeba mikoba ya viongozi, kuwatayarishia malazi salama viongozi pindi wanaposafiri, kuwakuwadia mabibi viongozi, kuhesabu vizibo kwenye mabaa, majungu, chuki dhidi ya wananchi na viongozi wao.

Kwa hiyo tunapojikuta leo tuna mgogoro wa kisiasa katika vyama vya siasa vya ushindani vikiwa vimehujumiwa visifanye kazi, makundi yanayohasimiana kuibuka ndani ya CCM, ufisadi wa kupindukia mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika, ni mambo yanayowaelemea maofisa wetu wa idara yetu ya usalama.

Kwa vyovyote vile mbeba lawama wa mwisho ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Yeye ndiye anamteua Mkurugenzi Mkuu wa idara hiyo. Idara hiyo nyeti isipofanya kazi vizuri rais atayumba, ataboronga na dola kwa ujumla itaonekana ni ya hovyo ndani na nje ya nchi.

Wananchi wanailalamikia dola kwamba inawanyanyasa na kuminya haki zao bila fidia ya kutosha. Hii inatoa tahadhari kwamba malalamiko hayo yanatokana na utendaji usioridhisha wa idara hiyo.

Natoa wito kwa viongozi wa idara hii kuamka na kushika nafasi kikamilifu kwenye kazi hiyo nyeti ya usalama kwa maslahi ya taifa letu bila kuyumbishwa na wanasiasa manyang’au na wachumia tumbo.

Hatujasikia idara hii kukosa uwezo au vitendea kazi; kwa hiyo haya mambo madogo madogo yanayotishia usalama wa nchi, hayawezi kutolewa visingizio kwamba haijawezeshwa.

Hivi sasa nchi yetu imekuwa na uhuru mkubwa zaidi wa kutoa maoni ambapo wananchi wamekuwa wakijadili kashfa mbalimbali hadharani kila zinapoibuka pasi mtu kukamatwa, kuwekwa mbaroni na kuteswa; tunaamini Idara ya Usalama wa Taifa inafanya kazi yake kwa maadili yanayostahili. Kwa hili tunaipa heko.

Nchi nyingine maofisa wa idara kama hii hawajaenda shule vizuri na wala hawajui maadili ya kazi zao.

Watanzania wengi wangeishia kuumia na kuteswa kwenye majumba ya siri yenye giza, nge na kila aina ya mateso.

Tunasema haya kwa sababu tunajua yanayoendelea kufanywa na idara kama hii katika nchi nyingi za Afrika.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

0716 774494
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Januari 24 mwaka 2010

Asante kwa ufafanuzi. Nimejifunza mengi.
 
hawa jamaa sioni faida yao nawaona sawa na magaidi au wanafanya kazi kwa maelekezo ya idara ya uenezi ya ccm boss wao ni na pe
 
acha uongokaka!!!mimi nimekulia katika familia ya mwana tiss tangu enzi za mwalimu,kuna maeneohuwezikujificha.kwa mfanowilaya kama za makete au ileje, ukiwa ofisa wa tiss utajulikana tu, we ndo utavaa vizuri, utaonekana unauwezo wa kununua bia, vijana wa nmb na wanawake watataka uwe rafiki yao, kila mtu atataka kukujua we nani. na kwa bahati mbaya ofisi ni moja gari lilelile.
 
Dr.babu anajua yote haya kuhusu umuhimu wa tiss na kazi zake pamoja na mafanikio. Ila kwa kuwa ana tamaa ya madaraka na ushauri anaopewa na CDU ni kukisambaratisha kwa kupoteza imani ya wananchi kwa chombo hiki .watz tusibiruzwe na wanasiasa uchwara kwa maslahi yao binafsi, tutafakari kabla ya kushabikia mambo yasiyo na msingi. Ciao.
 
iweje sasa akang'olewe kucha mtu mwingine tofauti kabisa na aliyetamka hayo maneno? Pia kuna sheria inayosema mtu anaehatarisha amani ateswe ama kung'olewa kucha, meno au jicho na si kuchukuliwa hatua za kisheria? Ukishaweza kujijibu hayo maswali utajua lilipo tatizo
Ili mtu aujue uchungu na siku nyingine asilete kidomodomo, dawa ni hii sasa hivi, ni lazima mtu ajutie matendo yake.
Wapi Ulimboka? kimyaaaa! ushasikia anahamasisha madaktari wagome?.

 
Toa ushaidi acha maneno yasiyo na msingi kwenye hoja husika. Kama huna ushaidi basi upite tu sio lazima kuchangia.

Lakini pia napenda kukupa angalizo, unamfahamu Lwakatare? unajua anatuhumiwa kwa nini? basi hao watu uliowataja wenda wakawa wameshughulikiwa na huyu niliemtaja mimi katika maelezo yangu.

Huyo hawezi toa ushahidi kwani majority yao wanaongozwa na ndoto(Nightmares) potofu. Njozi zao zinawapelekea kuona mambo ni mepesimepesi kwa hiyo wanajua kwakienda Ikulu wataibadilisha Tz for one night, very bad feelings! Nachoogopa kwa sumu inayomwagwa against TISS ni kwamba itawawia vigumu sana kuongoza nchi watakapopata madaraka.
Nafikiri hawa wanasiasa uchwara waache mchezo wao mchafu wakuipaka tope TISS kwani mchezo huu ni mbaya sana kwa taifa letu. Wao waendeleze siasa zao kwani suala la usalama hawajui . Manake sikuizi kila mtu anajiona ni makini na anajua masuala ya usalama wataifa very sad!
 
Na imagine CDM wamechukua madaraka 2015.....Mkurugenzi wa TISS anateuliwa kuwa kamanda Lwakatare....Mwanakijiji (T&T ex) msaidizi wa Lwakatare........duuhh! si mchezo.......CCM lazime watashika adabu.....lol
 
Nashukuru. nimejaribu
kupitia wote waliojadili topic hii hadi sasa nimeona kuwa akina mbhulula
ni 99% wenye uelewa wao hawajaingia, pindi wakifika watajua
nilichoandika ni nini.
Kutukana siyo ILANI YA CHADEMA. bali ilani ya CHADEMA ni uchambuzi wa
mambo kwa kina.



naona umetimiza ILANI YA CHADEMA kwa kuwaita wenzako "MBULLULA"
 
Maccm yalipo kuwa yakisema CUF
ni chama cha waislam na CHADEMA ni chama cha kikristo muheshimiwa
alikuwa busy anakula panadol lndia hakuyasikia sivyo?



kamanda naona umetimiza ILANI YA M4C. kwa lugha chafu
 
Wewe Kijana huna lolote ! lengo lako ni kuvuruga uzi huu , hivi unadhani kuna Great thinker utakaye mshawishi na hizo propaganda zako ! kama mpaka leo hujajua uozo wa Tiss basi bila shaka utakuwa mgeni nchi hii , na wala hakuna haja ya kukuelewesha , maana unajua , bali umeingia kwenye uzi huu kwa kazi maalum , endelea kujidhalilisha !

I have the right to speak my mind. If you are not amused by my opinion about TISS then just tell us what you know instead of talking nonsense.
 
Ndugu usjidanganye,,,wale jamaa wapo kwa ajili ya kulinda maslahi ya chama tawala..mi kuna mtu wa karibu namfaham yupo kule...na hua siachi kumwambia ukweli...kazi yao ni majungu na umbea....fitna za hapa na pale.....Wizi WA EPA. CIS..TANGOLD...HAO TISS Walikuwa wapi? ile TAASIS IPO KISIASA ZAID....CKU HIZI....IMEJAA WAHUNI WALIO TAYARI KUTESA WATU WASIO NA HATIA KWA AJILI YA KUWAFURAHISHA WAKUBWA....SHAME ON THEM.....

If you believe in what you say why don't you call a press conference in daylight and say this rubbish to the Tanzanian people? And, if you know that there are "wahuni" in TISS why don't you report them to the police so that they are dealt with according to the law? What you say here are exaggerated lies intended to tarnish the image of a State Security Organ of which you do not know how it operates. You are simply a failure. Shame on you!
 
Shutuma dhidi yaTISS ni sawa na shutuma zinazomkabli mama wa kambo. ni kawaida kabisa. ni dhahiri kwamba serikali ina wajibu wa kuonyesha ni nani anawang'oa watu meno na kucha kwa kuwa ina vyombo. ikiwa haifanyi hivo itaendelea kubeba lawama za mama wa kambo. sasa watu wasemeje mazimwi, majini au? afadhali zamani kulikuwa na ujinga vitu vya namna hii walisingiziwa mumiani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom