Utetezi juu Ya TISS; Jee Wanaoitetea wanajua Tofauti ya TISS ya Nyerere na TISS ya Kikwete

Utetezi juu Ya TISS; Jee Wanaoitetea wanajua Tofauti ya TISS ya Nyerere na TISS ya Kikwete

Status
Not open for further replies.
toauti ni kubwa sana,enzi za mwalimu TISS ilikuwa inafanya kazi kwa kuzingatia weledi na katiba na sharia za nchi bila kusahau ETHICS za kazi zao ambazo zinahitajiconfidentiality ya hali ya juu!na msingi wa kazi yao ni kuhakikisha maslahi ya nchi yanalindwa dhidi ya yeyote anayetaka kuhujumu!na pia target kubwa ya TISS ya mwalimu ilikuwa kuhakikisha viongozi wetu wa ngazi za juu mawaziri,wakuu wa mikoa na vigogo wote kwy mashirika ya umma na tahasisi mbalimbali wanazingatia ETHICS kweney utendaji wao hivyo TISS ilikuwa inawafuatalia kwa karibibu viongozi waliokuwa wanakiuka MIIKO ya uongozi kama ilivyoanishwa kwenye AZIMIO LA ARUSHA.TISS ya JK Kazi ni mabingwa wa kungoa meno na kucha bila GANZI, kutesa na kutelekeza watu kwenye msitu wa PANDE kama vile Dr.Ulimboka,Kibanda.
 
Hiyo TISS ni idara ambayo ipo kwa mujibu wa katiba, wewe kwa nini unadhani shughuli au wajibu wake hautakiwi kujulikana?

Inaonekana wewe ni muelewa. Hebu nipatie mfano wa nchi moja tu duniani ambayo idara yake ya usalama inaanika targets zake na goals zake. Just one country on earth!
 
Inasikitisha sana kuona vijana ambao ni nguvu kazi la taifa letu,wanapoteza weledi wao na kutiwa upofu na Nape kwa kuchukua elfu tano tano za voucher kila week kiasi ambacho mnashindWa hata kutetea taifa lenu linapodondoka,
Njaa mbaya sana wewe dada Metsada itakuponza

Ni ushaidi upi unaoitaji kuthibitisha hizo allegations wakati Kibanda na dr ulimboka wanatosha? SHAME ON YOURSELF husietaka kufanya kazi unategemea kuongwa na NAPE ili uje kupost pumba

Wewe akili yako ni usiku wa giza. Nape anihonge mimi??? Ananijua mimi??? I am independent and I have the right to freely express my feelings here just like you do. You would not put words into my mouth so as to say what you want to hear or read. All those allegations you are referring to are mere gossip with no truth at all. Do you believe everything reported in Newspapers? Do you? Unless the culprits are arraigned in court and dealt with according to the law, no one really knows who the real culprits are...
 
TISS ya enzi za JK Nyerere ilikuwa na weledi wa utendaji wa kazi na pia ilikuwa inaheshimu sana raia wake. Ililinda maslahi ya nchi kwa faida ya taifa lote. Kifupi tu TISS ya mwalimu Nyerere ilipenda sana raia wake hivyo haikuwa na haja ya kuwafanyia ukatili wa kinyama kama hii ya sasa inavyowafanyia raia wake. TISS ya sasa kwanza imekosa kabisa imani ya wananchi.

TISS ya sasa ni kama chombo cha kufanyia umafia kwa serikali ya chama tawala. Inatumika vibaya sana kuua demokrasia na uhuru wa kutoa mawazo. Inasikitisha sana chombo hiki muhimu sana katika ustawi wa taifa kinatumika kama chombo cha kufanyia uhalifu wa kibinadamu. Kwa sasa si sifa na heshima kubwa kufanya kazi katika chombo hiki kwani raia wema wanaona kama ni genge la kukandamiza demokrasia na uhuru wa kutoa maoni ambayo ni haki kikatiba.

Kwa kweli inasikitisha sana kuona hadhi ya chombo hiki inaporomoka namna hii. Ifike wakati hiki chombo kijisafishe na kuachana na kufanya kazi ambazo zinakitia aibu kwa umma wa watanzania. Bado watanzania wana imani nacho kwani ni chombo muhimu sana kikitumika vizuri. Hiki ndicho chombo muhimu kinachotulinda na maadui wanaoitazama vibaya nchi yetu.

Nalaani vitendo vya kigaidi na viovu vinavyofanywa na maafisa wachache wasiojua uthamani wa chombo hiki. Pia natoa nasaha zangu kwa viongozi wa kitaifa wakiache hiki chombo kiwe huru kufanya kazi zake zilizoainishwa kisheria bila kupewa maelekezo ambayo yanapelekea chombo kufanya kazi zisizo na manufaa kwa taifa. Mwisho kabisa nawaomba ndugu zangu watanzania tuwe na ustahamilivu kwani jambo la amani ya nchi yetu sio la mzaha kabisa.

Big Up. Una uzalendo wa kweli kwa nchi japo mapenzi ya chama yanaweza kuwapo kwenye akili yako. Nchi kwanza. Napenda unavyochambua issue in a positive and crically withou any bias. Tungekuwa wote kama Bw. Kiroba JF inegkuwa ni jamvi la manufaa hasa kuliko ambavyo wengi wetu tumekuwa negatively moved only on political affiliations and supportive fans without looking on issues critically and analytically.
 
usalama wa taifa wapambane na mafisadi. watusaidie katika uchumi wa taifa. vipi kama kuna vyama au vikundi vinaanzishwa kuvunja umoja/utaifa uliopo? wafanyeje? usalama wa taifa wasaidie kuhakikisha kuwa wana vishughulikia vyama na vikundi hivi. usalama wetu si kulinda tusiibiwe tu. usalama wetu ni pamoja na kulinda taifa hili linaloitwa tanzania.
 
Una maana Jack Zoka na Ramadhani IGHONDU!? Hamna kitu! hamna lolote! who is to get ashamed?! TISS!! TISS!! genge la wauaji vilaza fulani hivi. wanaotumiwa kama magogo ya chooni!! Plain stupidity are defending this crooks!?
wanajua kujibu kwa vitendo kwa kutoboa watu macho hasa wapinzani wa mfumo tawala!! hiyo ndiyo TISS ya Fastjet! like father like son!!

Ahaaaa, kwa hiyo unakuja hapa JF kutoa matusi hayo bila hata kujadili hoja objectively. Ukitafutwa ukapatikana utaweza kuthibitisha hayo unayosema??????
 
toauti ni kubwa sana,enzi za mwalimu TISS ilikuwa inafanya kazi kwa kuzingatia weledi na katiba na sharia za nchi bila kusahau ETHICS za kazi zao ambazo zinahitajiconfidentiality ya hali ya juu!na msingi wa kazi yao ni kuhakikisha maslahi ya nchi yanalindwa dhidi ya yeyote anayetaka kuhujumu!na pia target kubwa ya TISS ya mwalimu ilikuwa kuhakikisha viongozi wetu wa ngazi za juu mawaziri,wakuu wa mikoa na vigogo wote kwy mashirika ya umma na tahasisi mbalimbali wanazingatia ETHICS kweney utendaji wao hivyo TISS ilikuwa inawafuatalia kwa karibibu viongozi waliokuwa wanakiuka MIIKO ya uongozi kama ilivyoanishwa kwenye AZIMIO LA ARUSHA.TISS ya JK Kazi ni mabingwa wa kungoa meno na kucha bila GANZI, kutesa na kutelekeza watu kwenye msitu wa PANDE kama vile Dr.Ulimboka,Kibanda.

Pole. tatizo letu watz tunapenda saana kusahau historia kwa kudandia yaliyopo sasa. Nani kasema wakati wa mwalimu TISS haikutesa watu na hata kupoteza kabisa? TISS ndo kilikuwa chombo kama mungu mtu hapa TZ, nani alikuwa na uhuru wa kukijadili kama hivi inavyofanyika sasa? Au ndo tunapenda kujitia upofu kwa sababu sasa ni kikwete dhidi ya nyerere? Kwani huyu kikwete karithi kutoka kwa nani kama siyo huyo mnaemdhania kuwa hakukosea (nyerere)? Tuache kufikiri kwa mrengo wa nyuma, tufikiri kwa kutumia akili. Ingekuwa uhuru na wingi wa vyombo vya habari kwa sasa ni sawa na wakati ule wa nyerere mbona kila mtu angemkataa asiwe rais wa nchi hii. amefanya mabaya makubwa yenye uovu na uonevu mkubwa kwa wa TZ ambayo hayafikiriki? Let us leave biasness and be analytical criticisers
 
Ahaaaa, kwa hiyo unakuja hapa JF kutoa matusi hayo bila hata kujadili hoja objectively. Ukitafutwa ukapatikana utaweza kuthibitisha hayo unayosema??????
GO TO HELL!! huna wa kumtisha!!
 
on a curious note mkuu, huyo jamaa kwenye avatar yako ungempatia hata meno ya bandia tu, manake yatakuwa yalishamkuta!

noted mkuu, tamaduni zinaruhusu mkuu, hiyo ni njia maalum ya tiba, kwa magonjwa kama tetenus, na mengine mkuu, huyu yupo salama kabisa anafurahia maisha mkuu, kama unavyoona, smile kubwa linamananisha mambo poa kabisa,
 
Ahaaaa, kwa hiyo unakuja hapa JF kutoa matusi hayo bila hata kujadili hoja objectively. Ukitafutwa ukapatikana utaweza kuthibitisha hayo unayosema??????

Kwa nini usimtafute bila ya kumwambia? Au sheria inasema mhalifu anapigiwa simu kabla ya kutuma kikosi cha kumkamata....Yaani kama mitaa ya kwetu kila mtu anatoa haya mabiti loooooooooooooooooh!!!!!! TZ kiboku.
 
Naona hujanielewa. Mimi sina mamlaka wala uwezo wa kumkamata. Bali nilimuuliza, je iwapo ukatafutwa na ukapatikana utaweza kuthibitisha hayo unayosema???
 
It was a beacon of our nation. Leo hii mhhh!

Ukweli TISS ya leo inatia aibu sana, nawahurumia zaidi wale waliokuwa vijana ndani ya TISS ya Nyerere ambao nasikia kuwa siku hizi wametengwa kiaina fulani vile..yaani wapowapo tu ili wapate mshahara mwisho wa mwezi

Kweli ilikuwa vigumu kuwajua lakini kwa wale kama wa Ubungo flats pale tulikuwa tunawajua kwa uchache na si kwa undani sana kama hawa wa leo wanojianika utafikiri mitumba ipo Gulioni
 
Unamjua IGHONDU wewe au unashabikia tu taarifa za kutunga za magazeti?

Wewe una kila sababu ya kumjua kwavile nyie wote ni majasusi; mimi sina hata haja ya kuona uso wake kwani ni muuaji!!
 
Naona hujanielewa. Mimi sina mamlaka wala uwezo wa kumkamata. Bali nilimuuliza, je iwapo ukatafutwa na ukapatikana utaweza kuthibitisha hayo unayosema???

Mkuu lazima tukubali kuna tatizo huko TISS kwani hii idara inatumika vibaya na lazima wawe wakali kutoruhusu wahuni wachache ambao ni watendaji wanaotumika ili kuharibu maana na malengo yao.
 
Inaonekana wewe ni muelewa. Hebu nipatie mfano wa nchi moja tu duniani ambayo idara yake ya usalama inaanika targets zake na goals zake. Just one country on earth!
Simaanishi kwamba waseme Metsada leo tumechunguza na kugundua ujangili, namaanisha kwamba shughuli na wajibu wa idara hiyo unajulikana na mambo kama kushamiri kwa ufisadi, biashara za magendo, utoroshwaji wa wanyama wakiwa hai, udini, usafirishwaji wa meno ya tembo,kutekwa kwa watu mara kwa mara na kunyofolewa kucha, meno na macho, mauaji ya albino, mauaji ya viongozi wa dini, kuzagaa hadharani kwa kanda zinachochea mauaji hayo n.k, ni ishara kuwa ama idara hiyo ni dhaifu sana katika kutekeleza majukumu yake au inashiriki moja kwa moja kutekeleza mambo hayo.
 
Pole. tatizo letu watz tunapenda saana kusahau historia kwa kudandia yaliyopo sasa. Nani kasema wakati wa mwalimu TISS haikutesa watu na hata kupoteza kabisa? TISS ndo kilikuwa chombo kama mungu mtu hapa TZ, nani alikuwa na uhuru wa kukijadili kama hivi inavyofanyika sasa? Au ndo tunapenda kujitia upofu kwa sababu sasa ni kikwete dhidi ya nyerere? Kwani huyu kikwete karithi kutoka kwa nani kama siyo huyo mnaemdhania kuwa hakukosea (nyerere)? Tuache kufikiri kwa mrengo wa nyuma, tufikiri kwa kutumia akili. Ingekuwa uhuru na wingi wa vyombo vya habari kwa sasa ni sawa na wakati ule wa nyerere mbona kila mtu angemkataa asiwe rais wa nchi hii. amefanya mabaya makubwa yenye uovu na uonevu mkubwa kwa wa TZ ambayo hayafikiriki? Let us leave biasness and be analytical criticisers

Tunapojadili tusiifishe fikra kwa vitu complex ambavyo hata hatuna ushahidi navyo. Bila kujua sana majukumu ya TISS tujiulize matukio ya hivi karibuni na jitihada za TISS kuzuia yasitokee. Benki kuu yetu mwaka 2005-2006 ilivunjwa kweupe na Watanzania katika jua la utosi bilioni 150 zikachotwa na kuishia mifukoni mwa watu. Tukaambiwa kati ya wezi hao ni Kagoda ambayo tuliambiwa fedha zilienda kwa mambo ya usalama kabla Zakia Meghji hajabanwa naye kumsakizia aliyekufa na hali akijua hawezi kuwa shahidi.

Kuna Meremeta, Buzwagi, Richmond, Twiga na wanyama wengine kutoroshwa kweupe na ndege za kitapeli toka nje. Nijuavyo viwanja vya ndege vya kimataifa kuna mtu wa TISS anayetakiwa kukagua kila ndege ya nje inayofika hapa na kutoka. Naambiwa twiga hawa walitoroshwa na ndege za kijeshi za Qatar. Hivi bado viko kwenye kumbukumbu zetu. Riporti za CAG na mengineyo.

Tujiulize hivi kweli chombo hiki ni mahili and ethical wakati mambo haya yametokea na kulitia Taifa letu doa kiasi hicho? Kinastahili kuenziwa na kisiojiwe? Ndugu yangu nafikiri matukio haya na majibu mepesi toka serikalini na idara zake yanaleta opportunity of doubt.
 
Nani anapenda mijadala hii iendelee na kwa manufaa ya nani. Hoja ni kuwa ipo tuhuma dhidi ya baadhi ya watendaji wa chombo hiki ambayo haipaswi kupuuzwa. Kuipuuza ni kukubali kuwa haki ya watu fulani kuishi itatawaliwa na utashi wa chombo hiki na hakuna anayepaswa kuhoji. Mwenye wajibu wa kukisafisha chombo hiki na tuhuma hizi ni serikali kwa kuhakikisha unawahoji wahanga wa (wale waliong'olewa kucha na meno) ili wawataje wale wanaowahisi walifanya vitendo hivyo. Kuendelea kutofuatilia madai hayo yanayoichafua serikali wakati watu wakiwa tayari kutoa ushirikiano na vyombo hivyo ni kuruhusu mjadala huu uendelee maana kili ya mwanadamu haiachi kuhoji hadi inapopata maelezo ya kuridhisha. Badala ya kuwalalamikia wanaohoji serikali ijilalamikie yenyewe kwa kushindwa kuwahoji raia wema walio tayari kutoa msaada kwa jeshi la polisi kama sehemu ya utaratibu wa ulinzi shirikishi. Kama inashindwa kufanya yote hayo kwa nini watu wasidhani kuwa serikali inawajua wang'oa meno bali inawalinda kwa sababu inazozijua yenyewe.

Ningependa kuiamini TISS kama Taasisi kwa sababu hata tukibadili Wapangaji wa Ikulu TISS itafanya kazi na yeyote atakayeingia madarakani. Hili liko Kisheria/Kikatiba.
Hao Individuals wanaotajwa tajwa kuhusika na matukio ya utesaji hawawezi kusababisha tufike mahala tuione TISS kuwa haifai hata kuwepo. Ndiyo maana nilisema taasisi zenye majukumu ya kuisimamia TISS ZIWAJIBIKE. Lakini katika huo uwajibikaji tusijikute tuna-broadcast our weakness.
 
toauti ni kubwa sana,enzi za mwalimu TISS ilikuwa inafanya kazi kwa kuzingatia weledi na katiba na sharia za nchi bila kusahau ETHICS za kazi zao ambazo zinahitajiconfidentiality ya hali ya juu!na msingi wa kazi yao ni kuhakikisha maslahi ya nchi yanalindwa dhidi ya yeyote anayetaka kuhujumu!na pia target kubwa ya TISS ya mwalimu ilikuwa kuhakikisha viongozi wetu wa ngazi za juu mawaziri,wakuu wa mikoa na vigogo wote kwy mashirika ya umma na tahasisi mbalimbali wanazingatia ETHICS kweney utendaji wao hivyo TISS ilikuwa inawafuatalia kwa karibibu viongozi waliokuwa wanakiuka MIIKO ya uongozi kama ilivyoanishwa kwenye AZIMIO LA ARUSHA.TISS ya JK Kazi ni mabingwa wa kungoa meno na kucha bila GANZI, kutesa na kutelekeza watu kwenye msitu wa PANDE kama vile Dr.Ulimboka,Kibanda.

tofauti ni kuwa enzi za nyerere, idara hii haikuwepo kisheria. hivyo ilikuwa inaendeshwa kutokana na utashi wa rais. baada ya vyama vingi, kukawa na ulazima wa chombo hiki kuwa rasmi ndipo bunge lilipotunga sheria ya idara ya usalama wa taifa mwaka 1996. kwa sasa haifanyi tena kazi kwa matakwa ya mtu mmoja tu. idara inajitahidi kuaccomodate watu wote japo wengine hatuoni hilo
 
utajie hao watu ambao TISS ya mwalimu iliwatesa na hata kupoteza kabisa na kasha tufanye comparison na hawa wanaoteswa ha JK tuone kama kuna uwiano,awa wakina kibanda na Ulimboka Nyerere angewaona na hatia angekamata na kuweka ndani(detention) na hiyo ingelikuwa ni kazi ya POLISI tu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom