Utetezi juu Ya TISS; Jee Wanaoitetea wanajua Tofauti ya TISS ya Nyerere na TISS ya Kikwete

Utetezi juu Ya TISS; Jee Wanaoitetea wanajua Tofauti ya TISS ya Nyerere na TISS ya Kikwete

Status
Not open for further replies.
Nimemsikia Wassira akitetea TISS kuwa imefanya kazi nzuri sana na akakumbusha enzi za ukombozi kusini mwa Africa na haiwezi kun'goa watu kucha. Pia wabunge na mawaziri wengi wamekuwa wakirejea maneno hayo hayo katika kuitetea TISS.
Ninalotaka kujua hawa wanaotoa utetezi huo wanaelewa linalotuhumiwa na wapinzani? Wapinzani hawana wasiwasi na historia ya Idara ya Usalama wa Taifa na kazi nzuri zilizofanywa katika vipindi hivyo vya nyuma,lakini wanazungumzia utofauti wa utendaji ule wa weledi wa zamani na huu wa sasa.
Kwa nini Hawa CCM wanaitetea TISS kwa kutumia historia ya awamu zilizopita na sii kwa utendaji wa sasa? Au hawaelewi hata ni lipi wanalisemea?
Wala wasiwaumize kichwa wanafanya watu wote watoto na hawajui kitu ila wao tu!
 
Nimemsikia Wassira akitetea TISS kuwa imefanya kazi nzuri sana na akakumbusha enzi za ukombozi kusini mwa Africa na haiwezi kun'goa watu kucha. Pia wabunge na mawaziri wengi wamekuwa wakirejea maneno hayo hayo katika kuitetea TISS.
Ninalotaka kujua hawa wanaotoa utetezi huo wanaelewa linalotuhumiwa na wapinzani? Wapinzani hawana wasiwasi na historia ya Idara ya Usalama wa Taifa na kazi nzuri zilizofanywa katika vipindi hivyo vya nyuma,lakini wanazungumzia utofauti wa utendaji ule wa weledi wa zamani na huu wa sasa.
Kwa nini Hawa CCM wanaitetea TISS kwa kutumia historia ya awamu zilizopita na sii kwa utendaji wa sasa? Au hawaelewi hata ni lipi wanalisemea?

[h=3]Ijue idara ya USALAMA WA TAIFA...(III)[/h]
Habari News Tanzania

[h=3][/h]
Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania Intelligence and Security Service) ndiyo idara maarufu na inayoogopwa sana na wananchi walio wengi. Kutokana na kutoifahamu vizuri idara hii, wananchi wengi wanaichukia na kuiogopa kwa kudhani kuwa hii ndiyo idara inayotumika katika kuwaua na kuwatesa watu wenye mlengo na mawazo tofauti ya kisiasa hususan viongozi wa vyama vya upinzani. Kwa mfano, katika hali isiyo ya kawaida idara hii ilitajwa sana na kuhusishwa na vifo vya aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba, aliyekuwa waziri wa mipango na uchumi wakati wa serikali ya wamu ya pili Profesa Kigoma Ali Malima, na hata mzee Mahimbo aliye fariki hivi karibuni kwa ajali ya gari. Hata hivyo hakuna ushahidi wowote unao onesha au kuthibitisha kwamba idara hii ilihusika kwa namna moja au nyingine na vifo hivyo.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Naibu Mkurugenzi Jacky Nzoka[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Idara ya usalama wa Taifa (TISS) imeundwa kwa sheria ya bunge namba 15 ya mwaka 1996 (Tanzania Intelligence and Security Service act No. 15 of 1996) iliyosainiwa na Rais Benjamin Mkapa tarehe 20 mwezi Januari mwaka 1997. Sheria hiyo ndio inayoipa mamlaka Idara ya Usalama wa Taifa kufanya kazi zake ndani na nje ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, na pia ina ainisha majukumu, mamlaka na mipaka ya idara ya usalama wa Taifa. Kutokana na kuwepo kwa sheria hiyo siyo rahisi kwa idara hiyo kufanya mauaji ya raia wasio kuwa na hatia kwani idara itakuwa inavunja sheria na kukiuka mamlaka iliyopewa na bunge.

Hata hivyo, kama ilivyo kwa jeshi la wananchi wa Tanzania na Jeshi la Polisi, kadhalika idara hii INARUHUSIWA kutumia nguvu ya ziada (Reasonable force) katika kuwazuia maadui kumdhuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, viongozi wengine na wananchi wote wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kwa msingi huo, maafisa wa Usalama wa Taifa wanaweza kutumia nguvu au silaha yoyote inayofaa (reasonable force) katika kuwazuia magaidi, majasusi au maadui wanaotaka kufanya hujuma.
Hata hivyo nguvu hiyo ni lazima iwe inayofaa na isiyozidi kupita kiasi (reasonable force). Endapo adui atakuwa na silaha, basi maafisa wa Usalama wa Taifa watatumia silaha kumkabili adui hiyo. Ndio maana mtu aliyempiga kibao Rais mstaafu Ali Hassan Mwnyi hakuuawa kwa kupigwa risasi, bali alikamatwa na kushitakiwa.

Pamoja na idara hii kusajiliwa kisheria mwaka 1996, idara hii ilkuwepo tangu wakati wa utawala wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo ilikuwa ikifanya kazi chini ya mwamvuli wa ofisi ya Rais. Pengine kitu kilicho pelekea kusajiliwa kwa idara hii ki sheria ni mabadiliko ya mfumo wa kisiasa na uchumi yaliyotokea duniani mwishoni mwa miaka ya 1980 na kuingia Tanzania kwa kasi miaka ya 1990. Mabadiliko hayo na hasa kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi viliiweka idara hii katika hali ngumu ki utendaji kutokana na viongozi wengi wa vyama vya siasa kuamini kuwa idara hiyo ina kilinda chama tawala.

Baadhi ya wakurugenzi waliopata kuongoza idara hii ni marehemu Emilio Mzena (mkurugenzi wa kwanza) ambae alijipatia umaarufu mkubwa miongoni mwa wananchi kiasi cha kujulikana kwa jina la 'Mr Serikali'. Wengine ni marehemu Dr Laurence Gama, Mzee Hans Kitine, marehemu Luteni Jenerali Imran Kombe, na Colonel Abson. Wakati wa uongozi wake Colonel Abson aliiboresha idara ya usalama wa Taifa na kuhakikisha muswaada wa kuundwa kwa idara ya usalama wa Taifa kisheria unapelekwa bungeni na hatimae kusainiwa na Rais Mkapa. Hivi sasa Idara ya Usalama wa Taifa inaongozwa na Rashid Othman (Mkurugenzi mkuu) akisaidiwa na wakurugenzi wengine wanao ongoza kurugenzi ndogo.

Majukumu ya idara ya usalama wa Taifa.

Ni jukumu la idara hii kumchunguza mtu yeyote, kikundi cha watu au taasisi yoyote endapo idara hiyo inayo sababu ya kuamini (reasonable cause) kwamba mtu huyo anahatalisha au ni chanzo cha hatari kwa usalama wa Taifa. Kwa sababu hiyo idara hii inaruhusiwa kuingia (kumchunguza) kwa mtu yeyote, idara yoyote ya serikali, mamlaka yoyote, polisi au 'policing organisation' yoyote.

Kukusanya taarifa za ki intelejensia na ki usalama, kuzichambua na kuzitumia taarifa hizo kuzuia vitendo vyovyote vya ki adui vinavyoelekezwa kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kumshauri Rais na Mawaziri kuhusu maswala mbali mbali ya ki usalama. na kuvifahamisha vyombo vingine vya dola kuhusu uwezekano au kuwepo kwa vitendo vya ki adui katika jamhuri ya muungano wa Tanzania. Idara hii ndio iliyopewa jukumu la kuilinda jamhuri ya muungano wa Tanzania kutokana na vitendo vyote vya ki adui ikiwa ni pamoja na ujasusi (espionage), uhujumu (sabotage) ugaidi (terrorism) na uhaini na uzandiki (subversion)

Kwa sababu hiyo, idara ya usalama wa Taifa inao wajibu wa kuilinda na kuitetea serikali ILIYO CHAGULIWA na wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ili isiondolewe madarakani KINYUME cha sheria. Idara inatakiwa kuwadhibiti watu au kikundi cha watu wanaopanga mapinduzi, wanaotoa vitisho au maneno ya kuwashawishi wananchi kuipindua serikali (uzandiki) au namna nyingine yoyote ya kuiondoa serikali pasipo kupiga kura kama inavyo agizwa na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]DCI Robert Manumba[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Aidha idara hii inao wajibu wa kuzuia vitendo vyote vya kigaidi (terrorism) vinavyopangwa kufanyika katika ardhi ya Tanzania bara, Zanzibar na sehemu nyinginezo ambazo ni mali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ( k.m barozi zetu). Idara inawajibika kufanya uchunguzi, kuwatambua magaidi, na kuvifahamisha vyombo vingine vya dola ili kupanga mikakati ya kuwakamata na kuwafikisha mahakamani.

Idara hii pia inalo jukumu la kuchunguza, kugundua na kuzuia njama zozote zinazopangwa na mtu binafsi, kikundi cha watu, au nchi jirani zenye lengo la kuleta machafuko, mauaji au maangamizi ya aina yoyote kwa wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa lengo la kujipatia mafanikio ya kisiasa, ki uchumi, au kijamii ndani au nje ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Idara ya usalama inatakiwa kuwatambua watu wanaopanga mipango hiyo na watu au serikali zinazo wasaidia katika kutekeleza mipango hiyo, Kuchunguza vitendo vinavyofanywa na serikali za nje, asasi zisizo za kiserikali na wageni ili kubaini njama zinazounga mkono au kusaidia vitendo vya kijasusi au hujuma katika nchi yetu.

Aidha ni wajibu wa idara ya usalama wa Taifa kuhakikisha kuwa wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wanaendelea kuishia kwa utulivu, amani na mshikamano kwa kuchunguza na kubaini matatizo mbali mbali yanayo wakabili wananchi na kuishauri serikali iliyopo madarakani namna ya kuondoka kero zinazo wakabili wananchi.

Idara hii pia ndio yenye jukumu la kuwalinda viongozi wote wa kitaifa ikiwa ni pamoja na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais, Rais wa serikali ya baraza la mapinduzi Zanzibar, na wengineo ambao idara kwa sababu moja au nyingine itaona wanafaa kupewa ulinzi.

Aidha idara ya usalama wa Taifa inawajibika kukusanya taarifa zote za kiusalama ndani na nje ya nchi na kuishauri serikali (Rais) kufanya maamuzi mazuri na yenye faida kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Kutokana na majukumu ya idara hii, maafisa wa usalama wa Taifa wanalindwa na sheria na kwamba hawawezi kushitakiwa mahakamani kwa jambo lolote walilolifanya wakati wa kutekeleza majukumu ya idara ya usalama wa Taifa.

We are treading on very dangerous ground! Hivi hata hao wanaotusisitiza tujitawale kidemokrasia wanachokonoa mashirika yao ya kijasusi na majeshi yao?
Nikiri mapema kuwa uelewa wangu kuhusu ujasusi ni mdogo sana. Jasusi ninayemfahamu vizuri ni James Bond na Majasusi wachache niliowasoma kwenye novel chache. Hivyo Shirika letu la ujasusi silielewi kihivyo.
Niancho elewa ni kuwa kama jamii si busara kulichambua shirika letu la kijasusi hadharani. Wanasiasa wanajua majukwaa ambayo mambo ya ujasusi hujadiliwa. Mbunge anjua kuwa Kamati ya ulinzi na usalama ndiyo yenye kushughulika na mambo ya TISS na Majeshi yetu.
Sijisikii vizuri TISS kutuhumiwa/kushutumiwa kwa sababu katika hali ya kawaida wanatakiwa wawe juu ya tuhuma/shutuma. Kwa kuwa taasisi hii inaongozwa na binadamu, vyombo vya usimamizi wa taasisi hizi havitakiwi kuzembea eg Kamati ya Bunge ya Ulinzi & Usalama.
Kujadili weakness ya vyombo vyetu vya usalama kwa maoni yangu ni sawa na kujifunga kitanzi shingoni!

[h=3]HEKO IDARA YA USALAMA WA TAIFA[/h]6:53 PM 3 comments
Na Happiness Katabazi

KATIKA mchakato wa mageuzi ambayo yamefanyika kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, mfumo wa sheria na siasa za nchi, taasisi za dola zimejikuta zikiwa nyuma wakati vuguvugu la mageuzi likienda mbele.

Moja ya tasisisi zilizokumbwa na fukuto hilo ni Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ambayo hapo awali, yaani chini ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Kwanza na ya Pili, ilikuwa ni taasisi ambayo haikutambulika kisheria kutokana na muundo wake kuwa wa siri na wa gizani mno.

Matokeo ya utendaji wa idara hiyo uliiletea sifa ya kuogopwa sana na kuonekana ni chombo cha majungu, chuki na wauaji wa wananchi wenye misimamo tofauti na watawala wa serikali hizo mbili zilizopita zilizoongozwa na hayati Rais Julius Kambarage Nyerere na Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi.

Maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wakiwa katika umbile la kiraia ni wanajeshi na; idara hiyo ni chombo nyeti katika uhai wa dola letu.

Ni kweli kiasili, chombo hiki hufanya kazi kwa taratibu za idara zote za usalama wa taifa na kamwe mwanasiasa hawezi kukitumia; hata hivyo mwanasiasa anaweza kumtumia ofisa wa idara hiyo kwa siri kitendo ambacho ni cha ukiukwaji wa maadili.

Nchi inapoingia kwenye matatizo, migogoro ya kisiasa, lawama kubwa huelekezwa kwa taasisi hii kwani ndiyo inayotambua, kubashiri na kutoa ushauri wa nchi inavyoweza kukabiliana na hatari zozote zile za kiusalama na kiulinzi.

Hapa Tanzania, mageuzi ya mwaka 1992 yaliyoanzisha mfumo wa vyama vingi na mabadiliko mengine ya kisheria na Katiba, yalisababisha kuundwa kisheria kwa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kutambulika rasmi kisheria hapa nchini kulianza mwaka 1996, baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa Na.5 ya mwaka 1996 na kutambulika rasmi kwa jina la Tanzania Intelligence and Security Services (TISS), ambapo kwa sasa idara hiyo inaongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Rashid Othman.

Cheo hicho cha Mkurugenzi Mkuu ni sawa na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi na Kujenga Taifa (CDF), David Mwamunyange, na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema.
Kwa mujibu wa sehemu ya nne ya sheria hiyo inayounda (TISS), kazi na mamlaka iliyonayo ni kukusanya habari, kuchunguza na kutathmini habari zote zinazohatarisha usalama wa taifa na hatimaye kuishauri serikali hatua muafaka za kuchukua kwa maslahi ya taifa.

Ni wazi kwamba idara hii imechangia kwa kiasi kukubwa kudhibiti na kuzuia matendo mengi ya kihalifu ambayo yametendeka au yanayotarajia kutendeka kwa kutoa taarifa mapema kwa Jeshi la Polisi na taasisi nyingine husika ambazo mwisho wa siku ndizo zimeshiriki na kufanikisha kushindwa kwa matukio ya kihalifu.

Hivyo hatuna budi kuipongeza TISS kwa kazi nzuri wanayoifanya; haiwezi kuonekana moja kwa moja na wananchi kwa sababu moja ya miiko ya kazi zinazofanywa na idara hii ni siri.

Na idara hii imenyang'anywa mamlaka ya kukamata wahalifu kwani enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere idara hii ilikuwa na mamlaka hayo chini ya ‘Detention Order' yaani sheria ya kumuweka mtu kizuizini.

Kwa muktadha wa majukumu hayo, idara hiyo ilitakiwa ijiunde upya kutoka kwenye giza na usiri ili ifanye kazi kama chombo cha dola chenye majukumu ya kulinda amani, usalama na demokrasia. Kwa vyovyote vile idara hiyo haiwezi kufuta mfumo wa utaratibu wake wa kufanya kazi zake kwa siri kwa kuwa hiyo ndiyo namna pekee inayowezesha kupata taarifa na habari za kiusalama.

Lakini pia katika dola ya kidemokrasia lazima chombo hiki kivae umbile la uwazi katika utendaji kazi wake ili wananchi wakijue, wajue majukumu yake na waweze kushirikiana nacho pale inapobidi.

Kwa vyovyote vile usalama wa taifa unalindwa na kusalitiwa na wananchi ambao ndiyo wenye nchi; hivyo ni bora wakajua masuala mbalimbali yanayowazunguka.

Idara hiyo isipojijengea haiba ya kupendwa na wananchi, na hasa wazalendo, mwisho wa siku itajikuta inashindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kwa urahisi zaidi.

Hivi sasa lawama nyingi zinahusu kuibwa au kuporwa kwa rasilimali za nchi kunakodaiwa kufanywa na matapeli kwa kushirikiana na baadhi ya wawekezaji. Idara hii inaelekezewa lawama hizo, kuhujumiwa kwa uchumi wa nchi, kuuzwa kwa mashirika ya umma kwa bei chee na sasa mikataba mibovu mbalimbali ambayo dola imeingia na wawekezaji lazima ielekezwe kwenye idara hii. Kwa vyovyote vile kashfa ya ufisadi wa BoT, EPA na ombwe la viongozi bora lazima shutuma zielekezwe kwenye idara hii.

Kumbe basi wajibu wake si kama ilivyosadikiwa hapo zamani; yaani kuwa kazi kubwa ya maofisa wa idara hii ni kubeba mikoba ya viongozi, kuwatayarishia malazi salama viongozi pindi wanaposafiri, kuwakuwadia mabibi viongozi, kuhesabu vizibo kwenye mabaa, majungu, chuki dhidi ya wananchi na viongozi wao.

Kwa hiyo tunapojikuta leo tuna mgogoro wa kisiasa katika vyama vya siasa vya ushindani vikiwa vimehujumiwa visifanye kazi, makundi yanayohasimiana kuibuka ndani ya CCM, ufisadi wa kupindukia mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika, ni mambo yanayowaelemea maofisa wetu wa idara yetu ya usalama.

Kwa vyovyote vile mbeba lawama wa mwisho ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Yeye ndiye anamteua Mkurugenzi Mkuu wa idara hiyo. Idara hiyo nyeti isipofanya kazi vizuri rais atayumba, ataboronga na dola kwa ujumla itaonekana ni ya hovyo ndani na nje ya nchi.

Wananchi wanailalamikia dola kwamba inawanyanyasa na kuminya haki zao bila fidia ya kutosha. Hii inatoa tahadhari kwamba malalamiko hayo yanatokana na utendaji usioridhisha wa idara hiyo.

Natoa wito kwa viongozi wa idara hii kuamka na kushika nafasi kikamilifu kwenye kazi hiyo nyeti ya usalama kwa maslahi ya taifa letu bila kuyumbishwa na wanasiasa manyang'au na wachumia tumbo.

Hatujasikia idara hii kukosa uwezo au vitendea kazi; kwa hiyo haya mambo madogo madogo yanayotishia usalama wa nchi, hayawezi kutolewa visingizio kwamba haijawezeshwa.

Hivi sasa nchi yetu imekuwa na uhuru mkubwa zaidi wa kutoa maoni ambapo wananchi wamekuwa wakijadili kashfa mbalimbali hadharani kila zinapoibuka pasi mtu kukamatwa, kuwekwa mbaroni na kuteswa; tunaamini Idara ya Usalama wa Taifa inafanya kazi yake kwa maadili yanayostahili. Kwa hili tunaipa heko.

Nchi nyingine maofisa wa idara kama hii hawajaenda shule vizuri na wala hawajui maadili ya kazi zao.

Watanzania wengi wangeishia kuumia na kuteswa kwenye majumba ya siri yenye giza, nge na kila aina ya mateso.

Tunasema haya kwa sababu tunajua yanayoendelea kufanywa na idara kama hii katika nchi nyingi za Afrika.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

0716 774494
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Januari 24 mwaka 2010
 
Nimemsikia Wassira akitetea TISS kuwa imefanya kazi nzuri sana na akakumbusha enzi za ukombozi kusini mwa Africa na haiwezi kun'goa watu kucha. Pia wabunge na mawaziri wengi wamekuwa wakirejea maneno hayo hayo katika kuitetea TISS.
Ninalotaka kujua hawa wanaotoa utetezi huo wanaelewa linalotuhumiwa na wapinzani? Wapinzani hawana wasiwasi na historia ya Idara ya Usalama wa Taifa na kazi nzuri zilizofanywa katika vipindi hivyo vya nyuma,lakini wanazungumzia utofauti wa utendaji ule wa weledi wa zamani na huu wa sasa.
Kwa nini Hawa CCM wanaitetea TISS kwa kutumia historia ya awamu zilizopita na sii kwa utendaji wa sasa? Au hawaelewi hata ni lipi wanalisemea?
wabunge wa CCM na serikali wanafahamu mchezo mchafu unaofanywa na Usalama wa Taifa kwa maslahi ya CCM!
 
naishauri serikali ipokee maoni ya wabunge na kuyafanyia kazi na baadaye itoe mrejesho wa kitaalamu kuhusiana na madai hayo badala ya kubishana na wabunge waliotoa shutuma! mimi binafsi naona serikali inakuwa kama inajitetea sana badala ya kutoa suluhu ya tatizo,hivi kuitetea TISS ndio suluhisho la malalamiko ya wabunge?inafahamika wazi kuwa kuna viongozi na matajiri nchi hii wananufaika na udhaifiu wa TISS kwa kuwa huru kufanya watakavyo!!!TISS inafahamu jinsi watu wanavyoiba mali za umma,jinsi watu wanavyofanya kazi kwa ukabila , jinsi watu wanavyoendekeza masual ya udini kwenye uendeshaji wa taasisi za umma namambo mengine hatari kwa nchi.Hapa tujiulize kwanini TISS hawakuyaona haya mapeme na kuyaripoti ili yazuiliwe kabla hayajaleta madhra na manung"uniko katika jamiiHapa pana udhaifu pafanyiwe kazi kubwa na viongozi wazalendo badala ya kujitetea!wananchi wanataka mabadiliko
 
nakumbuka wakati nasoma darasa la sita jambazi moja lilikuja kuishi kijijini(ilikuwa mwaka 1986) lilifanya uhalifu DSM likakimbilia kijijini kwetu likawa linafanya uhalifu(ila sio hapo kijijini) na uwindaji haramu. siku moja akaja jamaa moja akapanga chumba nyumbani kwetu kwa kujitabulisha kuwa anatokea Muheza kazi yake ikawa kuziba sufuria na maplastic yanayovuja jioni anazunguka mtaani huku anapiga kinanda watoto tukawa tunafuata nyuma. Jioni usiku jamaa anaenda kilabuni kupiga pombe ya mnazi, gongo na boha.

baada ya wiki tatu hatukuamini kwani alipotea na siku mbili baadaye walikuja polisi kumkamata jambazi ambaye bila kujijua(huyu jambazi) alijenga urafiki wakaribu na mpangaji wetu na walikuwa wanakunywa pamoja kilabuni.

Wanakijiji hatukuamini kwani jambazi huyu alikuwa akifanyia ujambazi mbali sana na kijiji ila pale kijijini alikuwa mtu mwema na alikuwa akisaidia majirani anaokaa nao kwenye misiba na ugonjwa kwa muda wa miezi sita Jambazi huyu aliyokaa kijijini pale alijenga umaarufu mno ila alikuwa haishi miezi miwili lazima asafiri na akafungua bucha la kuuza nyama ila bei yake aliiweka chini sana kwa kilo kwa kisingizio anawasaidia watu na aliruhu kukopesha nyama kwa wanakijiji siku za wikiend.

siku ya kukamatwa kwake hakuna aliyeamini mjomba ambaye alikuwa mkuu wa kituo kwenye tarafa yetu alimdokeza baba kuwa jamaa alikuwa usalama wa taifa na ndiye aliyewapa taarifa kuwa jamaa akamatwe apelekwe Dar es Salaam kwani ni Jambazi hatari na huyu TISS alitoa taarifa baada ya kukamilisha kazi yake na hakuacha details zozote na uncle wala hakumjua kuwa jamaa alikuwa usalama zaidi ya fundi sufuria na plastic, mlevi na mpiga kinanda na hata uvaaji wake ilikuwa nguo chafu zilizochakaa kuendana na mazingira ya kijijini. Mbaya zaidi akawa anajinyenyekeza kwa jambazi ili anunuliwe pombe za bure hadi wakajenga urafiki kiasi kwamba jambazi akitaka kwenda kilabuni anakuja kumtafu jamaa(TISS).

Na hii ndiyo TISS iliyoachwa na Nyerere ngumu kumjua nani ni usalama wa taifa. Jamaa walikuwa werevu mno na wanajichanganya na jamii na walikuwa wako kwa ahili ya kuwatumikia wananchi.
 
TusijiteteE sana tutafute suluhisho la matatizo ya TISS.TISS itoe taarifa za matatizo yaliyopo kwenye jamii pale tu yanapoanza sio kuacha hadi yanaota mizizi na kuleta madhara kwa jamii!
 
Enzi za mwalimu TISS aliyejulikana ni yule atakayepewa wilaya / mkoa na ngazi zingine za juu lakini wengine wote walikuwa hawajulikani na utakuta hata ndani baba hajui kuwa mkewe ni TISS. lakini wa leo nenda wilaya yeyote halafu uliza watumishi wakuorodheshee kama hawajakupa list yote mpaka huwa wanapumzika wapi wakivizia taarifa za wapinzania.
Hata kariakoo sokoni ukipita na ukiuliza makuli wanakwambia mbona ni fulani na fulani

hahahahahahahahahaaaaaa...
..duh! U made my day mkuu. Ubarikiwe.
 
nakumbuka wakati nasoma darasa la sita jambazi moja lilikuja kuishi kijijini(ilikuwa mwaka 1986) lilifanya uhalifu DSM likakimbilia kijijini kwetu likawa linafanya uhalifu(ila sio hapo kijijini) na uwindaji haramu. siku moja akaja jamaa moja akapanga chumba nyumbani kwetu kwa kujitabulisha kuwa anatokea Muheza kazi yake ikawa kuziba sufuria na maplastic yanayovuja jioni anazunguka mtaani huku anapiga kinanda watoto tukawa tunafuata nyuma. Jioni usiku jamaa anaenda kilabuni kupiga pombe ya mnazi, gongo na boha.

baada ya wiki tatu hatukuamini kwani alipotea na siku mbili baadaye walikuja polisi kumkamata jambazi ambaye bila kujijua(huyu jambazi) alijenga urafiki wakaribu na mpangaji wetu na walikuwa wanakunywa pamoja kilabuni.

Wanakijiji hatukuamini kwani jambazi huyu alikuwa akifanyia ujambazi mbali sana na kijiji ila pale kijijini alikuwa mtu mwema na alikuwa akisaidia majirani anaokaa nao kwenye misiba na ugonjwa kwa muda wa miezi sita Jambazi huyu aliyokaa kijijini pale alijenga umaarufu mno ila alikuwa haishi miezi miwili lazima asafiri na akafungua bucha la kuuza nyama ila bei yake aliiweka chini sana kwa kilo kwa kisingizio anawasaidia watu na aliruhu kukopesha nyama kwa wanakijiji siku za wikiend.

siku ya kukamatwa kwake hakuna aliyeamini mjomba ambaye alikuwa mkuu wa kituo kwenye tarafa yetu alimdokeza baba kuwa jamaa alikuwa usalama wa taifa na ndiye aliyewapa taarifa kuwa jamaa akamatwe apelekwe Dar es Salaam kwani ni Jambazi hatari na huyu TISS alitoa taarifa baada ya kukamilisha kazi yake na hakuacha details zozote na uncle wala hakumjua kuwa jamaa alikuwa usalama zaidi ya fundi sufuria na plastic, mlevi na mpiga kinanda na hata uvaaji wake ilikuwa nguo chafu zilizochakaa kuendana na mazingira ya kijijini. Mbaya zaidi akawa anajinyenyekeza kwa jambazi ili anunuliwe pombe za bure hadi wakajenga urafiki kiasi kwamba jambazi akitaka kwenda kilabuni anakuja kumtafu jamaa(TISS).

Na hii ndiyo TISS iliyoachwa na Nyerere ngumu kumjua nani ni usalama wa taifa. Jamaa walikuwa werevu mno na wanajichanganya na jamii na walikuwa wako kwa ahili ya kuwatumikia wananchi.

du wewe kweli hujui kazi za usalama wa taifa. je kazi za polisi ni nini? je polisi hawana kitengo ya upelelezi ambao moja ya majukumu yao ni kufuatilia nyenendo za wahalifu?
 
unaweza kuleta ushahidi kwamba tiss inatesa raia???? Au na wewe unaamini propaganda za chadema? Acheni kuzungumza mambo ya uongo dhidi ya chombo nyeti kama tiss. Tiss ndio uhai wa taifa... Ila sikulaumu kwakua wale jamaa kazi zao hatuzijui hivyo ni rahisi kuwasingizia na kusema lolote kwakua huwa hawana press conference ya kujibu tuhuma...

Yule alietajwa kumteka ulimboka anafanya kazi wapi vile?
 
naishauri serikali ipokee maoni ya wabunge na kuyafanyia kazi na baadaye itoe mrejesho wa kitaalamu kuhusiana na madai hayo badala ya kubishana na wabunge waliotoa shutuma! mimi binafsi naona serikali inakuwa kama inajitetea sana badala ya kutoa suluhu ya tatizo,hivi kuitetea TISS ndio suluhisho la malalamiko ya wabunge?inafahamika wazi kuwa kuna viongozi na matajiri nchi hii wananufaika na udhaifiu wa TISS kwa kuwa huru kufanya watakavyo!!!TISS inafahamu jinsi watu wanavyoiba mali za umma,jinsi watu wanavyofanya kazi kwa ukabila , jinsi watu wanavyoendekeza masual ya udini kwenye uendeshaji wa taasisi za umma namambo mengine hatari kwa nchi.Hapa tujiulize kwanini TISS hawakuyaona haya mapeme na kuyaripoti ili yazuiliwe kabla hayajaleta madhra na manung"uniko katika jamiiHapa pana udhaifu pafanyiwe kazi kubwa na viongozi wazalendo badala ya kujitetea!wananchi wanataka mabadiliko

hakuna mbunge wa upinzani aliyetoa ushauri. wote wamelalamika tu na kuendeleza mipasho ya zero brain, mbowe
 
hawa TISS wa sasa ambao nchi yetu inatafunwa wanaangalia au na wao wanashirikishwa, kuna tofauti sana, waache wana siasa wawatetee maana ndio wanawalinda.
 
Tofauti kweli ipo, ile ya Nyerere watu walikuwa wanapotea ki ajabu ajabu ilikuwa inafanya kazi ki KGB KGB!

Siku hizi naona TISS inafanya kazi vizuri kwa weledi.
 
TusijiteteE sana tutafute suluhisho la matatizo ya TISS.TISS itoe taarifa za matatizo yaliyopo kwenye jamii pale tu yanapoanza sio kuacha hadi yanaota mizizi na kuleta madhara kwa jamii!

je taarifa unazopata kutoka polisi na CAG hasikutoshelezi?
 
Issue ni je wanahusika au la. Maana kutetea sio issue yawezekana wamefanya kwa matakwa yao hawajatumwa.
 
Nimemsikia Wassira akitetea TISS kuwa imefanya kazi nzuri sana na akakumbusha enzi za ukombozi kusini mwa Africa na haiwezi kun'goa watu kucha. Pia wabunge na mawaziri wengi wamekuwa wakirejea maneno hayo hayo katika kuitetea TISS. Ninalotaka kujua hawa wanaotoa utetezi huo wanaelewa linalotuhumiwa na wapinzani? Wapinzani hawana wasiwasi na historia ya Idara ya Usalama wa Taifa na kazi nzuri zilizofanywa katika vipindi hivyo vya nyuma,lakini wanazungumzia utofauti wa utendaji ule wa weledi wa zamani na huu wa sasa. Kwa nini Hawa CCM wanaitetea TISS kwa kutumia historia ya awamu zilizopita na sii kwa utendaji wa sasa? Au hawaelewi hata ni lipi wanalisemea?
Jambo ambalo hawalisemi waziwazi ni kuwa je inawakera wanapoona vitendo hivi vya watu kung'olewa kucha, meno na macho? Hata kama wanaong'olewa si Dr. Slaa wala Mbowe hao waliotendewa hayo walistahili kutendewa? Kwa nini ikiwa wanakerwa na vitendo hivi hawajamuhoji Ulimboka awasaidie kutambua waliotenda vitendo hivyo? Au wanafikiri upeo wa Watanzania kufikiri ni kama huo walionao?
 
je taarifa unazopata kutoka polisi na CAG hasikutoshelezi?

Kwa hiyo taarifa ya CAG ya mwaka juzi na polisi baada ya matukio ndio kazi ya TISS, wa wapi wewe. Jaribu kucheck hata movie za kijasusi kama James Bond et el ujue ujasusi ni nini?.
 
Tofauti kweli ipo, ile ya Nyerere watu walikuwa wanapotea ki ajabu ajabu ilikuwa inafanya kazi ki KGB KGB!

Siku hizi naona TISS inafanya kazi vizuri kwa weledi.

hayo ndo wafuasi wa chadema hawayataki. wanataka idara hii isiangalie uhuru wa watu kuongea, ikamate hovyo hovyo, na wanasiasa uchwara kama akina slaa wasipumue. ashukuriwe rais kikwete kwa uvumilivu wake maana chombo hiki kipo chini yake na ninaamini hakuna amri ya kupingwa ikiwa ataamrisha hiyo kamatakamata iwepo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom