Utetezi juu Ya TISS; Jee Wanaoitetea wanajua Tofauti ya TISS ya Nyerere na TISS ya Kikwete

Utetezi juu Ya TISS; Jee Wanaoitetea wanajua Tofauti ya TISS ya Nyerere na TISS ya Kikwete

Status
Not open for further replies.
Tiss ilimuokoa mbowe kule tarime asiuawe na wananchi walipomtuhumu kumuuwa chacha wangwe
 
hata waseme vp hao tiss humu ndani wanaojaribu kutetea, ukweli unabaki palepale kuwa tiss wa siku hizi kwa kweli wanakasoro kubwa na wanaipeleka nchi yetu pabaya.
 
siku zote popote pale vyombo vya ulinzi na usalama vipo kulilinda tabaka tawala. na si vinginevyo haya mengine yote tunayoyaona na kuyasikia wanayafanya kwa sababu wanajua kwa namna moja ama nyingine tabaka tawala linaweza kuathirika hivyo wanalilinda.
hii ya usalama wa taifa ni lugha tu nzuri inayotumika kutupa matumaini tulio wengi
 
Utofauti wa TISS
Enzi za Mwalimu @ TISS kulilinda taifa na watu wake.
Enzi za Dogo wa bongo flava @ TISS kuliangamiza taifa na watu wake.

Du vitu viwili tofauti kabisa na anajiskia raha wala hana ata punje ya wasiwasi
 
Kama una ndugu au mtu yeyote anaefanya kazi TISS umwambie hakuelimishe majukumu ya kada hiyo nyeti kwa taifa.

Kwa kukudokeza japo kidogo tu ili upate picha na kuachana na upotoshaji!, soma haya yafuatayo;

1. TISS ina idara zake, zipo za ujasusi, mahusiano ya kimataifa, PSU, mawasiliano na uchumi. Tuhuma za CHADEMA sidhani kama zinakaa kokote katika hizi idara. Na kama wanamjua wanaemtuhumu, waende polisi wakapeleke mashtaka yao ili hatua stahiki zichukuliwe.

2. Faida ya kuwa na idara hii kwa sasa ni kubwa kuliko awamu yeyote ile, nakupa mfano, katika hali ya kawaida, hakuna kiongozi yeyote wa taifa lolote, atakae kanyaga katika ardhi ya nchi yenye usalama wa sintomfahamu. Wote tunashuhudia wanavyopishana viongozi wa mataifa mbalimbali airport kuja hapa nchini. Ni jambo la kujipongeza.

3. Swala zima la utalii.

4. Mahusiano ya kimataifa.

5. Umoja, amani na mshikamano wa watanzania.

Kama mpaka leo bado TISS ipo chini ya utawala wa Kikwete, na hayo niliyoeleza yanazidi kuimarika, basi hawa TISS wa sasa ni bora zaidi ya awamu zote zilizopita.

Hiyo TISS unayoisifia imefanya nini cha maana kuhusu uharifu wa EPA, Deep green,Meremeta, kuuawa kwa viongozi wa dini , kung'olewa kucha na meno watu bila ganzi? kama sio wahusika kwanini haijasaidia kuwapata wahusika?
 
Enzi za mwalimu TISS
aliyejulikana ni yule atakayepewa wilaya / mkoa na ngazi zingine za juu
lakini wengine wote walikuwa hawajulikani na utakuta hata ndani baba
hajui kuwa mkewe ni TISS. lakini wa leo nenda wilaya yeyote halafu uliza
watumishi wakuorodheshee kama hawajakupa list yote mpaka huwa
wanapumzika wapi wakivizia taarifa za wapinzania.
Hata kariakoo sokoni ukipita na ukiuliza makuli wanakwambia mbona ni
fulani na fulani

kweli kabisa hasa huku uswahilini kwetu utawaona bar wakitamba waziwazi kuwa wao ni usalama yaani inatia kinyaa na aibu lakini pia inachekesha kweli
 
kweli kabisa hasa huku uswahilini kwetu utawaona bar wakitamba waziwazi kuwa wao ni usalama yaani inatia kinyaa na aibu lakini pia inachekesha kweli

mkuu, hao ni maafisa usalama wa chadema ambao hutumia mbinu hizo za kujitambulisha kwenye baa ili wajipatie vinywaji vya bure maana hawa jamaa wana njaa kweli. pia wanatumia mbinu hiyo ili kuichafua idara ya usalama wa taifa
 
Nyie mtapiga kelele usiku mtalala
Idara ya usalama wa taifa, haina tatizo na mtu isipokuwa kama huyo mtu anahatarisha usalama wa nchi, mfano mtu anasema "nchi hii haitatawalika"
Unategemea mtu kama huyo anaetaka kuhatarisha amani ya nchi aachwe tu? Lazima TISS wapige hodi mlangoni mwako,
Stephen Masatu Wassira:

iweje sasa akang'olewe kucha mtu mwingine tofauti kabisa na aliyetamka hayo maneno? Pia kuna sheria inayosema mtu anaehatarisha amani ateswe ama kung'olewa kucha, meno au jicho na si kuchukuliwa hatua za kisheria? Ukishaweza kujijibu hayo maswali utajua lilipo tatizo
 
Wewe unajua kazi
zinazofanywa na TISS? Au unashabikia tu porojo za CHADEMA na story za
mitaani. Hamna mnalolijua kuhusu ueledi na kazi zinazofanywa na chombo
hicho that is why mnabakia kutunga mambo ya uongo juu ya TISS kwakua
mnajua hawana kawaida ya kujibizana na vyombo vya habari. Wewe hapo
ulipo unaishi kwa amani na kufanya siasa zako za CHADEMA Kwa amani ila
hujui hiyo amani imepatikanaje na inakua maintained vipi. Mtasema sana
tuuuuu ila USILOLIJUA NI USOKU WA GIZA.... SHAME ON YOU!
loh USOKU wa giza umepaniki mpaka unakosea na wewe ni mmoja wao ninin?
 
kiongozi unajuaje kuwa unachokijua wewe ndicho kilicho sahihi unaweza pia ukawa umemezeshwa visivyo.
au wewe upo huko?

huhitaji akili ya ziada wala kumezeshwa kuamini kuwa TISS inafanya kazi vizuri na haipo kisiasa. nimeishi rwanda kwa takriban miaka mitano 1996 hadi 2001, niliyokuwa nayaona kule ni tofauti na maisha ya hapa tanzania. nimeishi pia uganda 2011 hadi 2012, mzee kiza besyge amehangaika sana awe rais wa uganda, yaliyomkuta nafikiri hata kwenye vyombo vya habari mlikuwa mnasikia. sasa kachoka na ameamua kuachana na siasa. juzi nimetoka burundi. nafikiri unajua sakata la mtangazaji wa Radio Bonesha na RFI, HASSAN LUVAKUKI na wengine wa aina yake. ila usipotembea japo kwa majirani zako utajiaminisha kuwa TISS ipo kwa ajili ya hao mnaowaita mafisadi
 
Nyie mtapiga kelele usiku mtalala
Idara ya usalama wa taifa, haina tatizo na mtu isipokuwa kama huyo mtu anahatarisha usalama wa nchi, mfano mtu anasema "nchi hii haitatawalika"
Unategemea mtu kama huyo anaetaka kuhatarisha amani ya nchi aachwe tu? Lazima TISS wapige hodi mlangoni mwako,
Stephen Masatu Wassira:

wote wangekuwa na busara kama zako kusingekuwa tatizo.lakini busara za magwanda ni tatizo.lakini dawa yake TISS kuimarisha operesheni zake dhiidi ya wachavuzi wa amani iwe mtu chama shehe askofu au dini.nadhani kutokana na kazi yake nzuri ndio maana kelele zinapigwa.sisi tunataka amani hawa wenye uchu wa madaraka ili wapore rasilimali zetu wamalizwe mungu ibariki tz
 
mkuu, hao ni maafisa usalama wa chadema ambao hutumia mbinu hizo za kujitambulisha kwenye baa ili wajipatie vinywaji vya bure maana hawa jamaa wana njaa kweli. pia wanatumia mbinu hiyo ili kuichafua idara ya usalama wa taifa

Acha unafiki wewe chadema wapo makini sana, unaonaje mahakama ikitoa amri ya statement za simu za wale watu kumi kuwa hadharani pamoja na sms szao zote tujue mbivu na mbichi.
 
Usalama wa ccm ndio maaana wanawatetea si unaona walivyosaidia kuchakachua mwaka 2010!!!!!!!!!!
 
sure. waambie mburula hawa
Ukiniambia mambo ya mburula nakushangaa, wala sikuelewi, lakini nilikuwa na maana kuhusu TISS ni kutumia kitu kizuri kwa njia tofauti ni sawa na kutumia mswaki wako kusugulia chooni, ndiyo hivyo baadhi ya TISS wanavyo tumika, hayo mambo ya mburu... kamwambie shangazi yako!
kama unajadili kama mtu mwenye akili timamu. Karibu!
 
Unaweza kuleta ushahidi wa hizo allegations? Au unashabikia tuu propaganda za chama chako cha CHADEMA???? SHAME ON YOU! HUNA UNALOLIJUA KUHUSU TISS HIVYO UTABAKIA KUAMINI POROJO ZA WAJINGA WENZAKO...
Wewe akili zako finyu. Usalama gani wa taifa usiolinda maslahi ya Uchumi ya nchi na watu wake? Mwenyewe unajiona unajua? Usidhani unajibishana na laymen wasojua chochote.
 
We are treading on very dangerous ground! Hivi hata hao wanaotusisitiza tujitawale kidemokrasia wanachokonoa mashirika yao ya kijasusi na majeshi yao?
Nikiri mapema kuwa uelewa wangu kuhusu ujasusi ni mdogo sana. Jasusi ninayemfahamu vizuri ni James Bond na Majasusi wachache niliowasoma kwenye novel chache. Hivyo Shirika letu la ujasusi silielewi kihivyo.
Niancho elewa ni kuwa kama jamii si busara kulichambua shirika letu la kijasusi hadharani. Wanasiasa wanajua majukwaa ambayo mambo ya ujasusi hujadiliwa. Mbunge anjua kuwa Kamati ya ulinzi na usalama ndiyo yenye kushughulika na mambo ya TISS na Majeshi yetu.
Sijisikii vizuri TISS kutuhumiwa/kushutumiwa kwa sababu katika hali ya kawaida wanatakiwa wawe juu ya tuhuma/shutuma. Kwa kuwa taasisi hii inaongozwa na binadamu, vyombo vya usimamizi wa taasisi hizi havitakiwi kuzembea eg Kamati ya Bunge ya Ulinzi & Usalama.
Kujadili weakness ya vyombo vyetu vya usalama kwa maoni yangu ni sawa na kujifunga kitanzi shingoni!
 
Kila kitu kina muonekano wa kipekee unaotofautisha na kingine,uslama ya nyerere kipindi cha ujamaa lazima iwe tofauti na hii ya kikwete katika ubeperi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom