Utetezi wa Dr. Louis....
Mimi ni kweli nilipanga kununua nyumba zote tatu, na kwenye mnada nilitamka fedha 700, 800 na mwisho 900...
Hakuna popote niliposema milion 900
Nimewaacha police wanarudia kusikiliza ile clip[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Dr. Shika hafungwi wala hana kesi ya kujibu, nimependa sana approach na logic yake, angalia alivyotiririka. Kimsingi yeye hakuwa kati ya watu waliotaja hela nyingi.
1. Nyumba ya kwanza yeye aliambaambaa kama ifuatavyo:
Naanza na offer ya milioni 300, milioni 400, 500 (kuwa makini hajataja neno milioni), naweka 7 (hakuna neno milioni), hebu tufanye nane, weka 900. Akawa amemaliza kazi.
2. Nyumba ya pili. Hapa amesema kwa kurudiarudia na mtiririko ulikuwa kama ifuatavyo:
Naongeza nusu / (dalali akasema eeh!) naweka nusu / naongeza nusu / 550, 700, naongeza moja. Akawa amemaliza kazi. Katika mnada wa nyumba ya pili hakuna sehemu hata moja ametaja neno milioni, dalali alikuwa analiongezea.
3. Nyumba ya tatu aliflow kama ifuatavyo:
Naweka 5 (450), tufanye 6, 700 hazitadhuru, naweka 800, 900 itapendeza sasa, na mimi naongezea hamsini nyingine, naongezea 50 (nimeongezea mia/50), tufanye na milioni 200. Akawa amemaliza kazi.
Sasa unaweza kudai hapo mwishoni ametamka au kuashiria milioni 1200, lakini sio kweli kwa sababu hilo neno milioni amelitaja kwa kushawishiwa (persuaded) na dalali - "the auctioneer persuaded Dr. Louis Shika to accept her own point of view", kwa sababu kila mara Dr. Shika alipotamka, mfano naweka 800, dalali alisema milioni 800, akisema naweka au naongezea 50, dalali anaweka neno milioni na kutamka milioni 50.
Utetezi wa Dr. Louis Shika hapa ni rahisi na ni kwamba, kutokana na dalali kutamka mil 50, mil 700, mil 800 badala ya 50, 700, 800 kinyume na yeye alivyotamka, yeye pia alitamka neno milioni 200 ("tufanye na milioni 200") kumaanisha 200.
Kesi hakuna, akili mara zote ni mali.