UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka...


afya ya mwendazake hatutaki kuiongelea hata chembe..................DPP angependa aonekane alikuwa ni mzima......lakini huyu daktari wake wa kulithibitisha hilo hawataki kumhoji kwa sababu majibu wanayo..........hiv related complications resulted into a massive internal organs failure............na huyu mtoto was a mere victim of circumstances.......
 
Mbona kwenye vipindi vya tv alisema 18

hicho siyo kiapo kinachokubalika mahakamani...................vyombo vya khabari hata haya tunayoaongelea huwezi kwenda nayo kama kuthibitisha umri wa mtoto huyo ambaye anapaswa kauchiwa aharaka aende kunyonya ziwa la mamaa yake
 
Nimekuelewa sana Ruta hilo wazo la ubakaji ndilo nilikuwa nawaza na anatokea hapo. tuache ushabiki wa filamu

na wengineo fuateni mfano huu wa kuelewa haraka filamu zake tuendelee kuziangalia lakini tukumbuke he was only human............
 

Well said mkuu,cha ajabu bado wengi hawatakuelewa...kwa maelezo yako unakuja kwenye hoja yangu,kwamba kuna sababu nyingi za Lulu kuonekana hana hatia na chache kuonekana ana hatia..80% innocent 20% guilty
 
katoto kanakofanya mapenzi na Muheshimiwa waziri!

huyo mheshimiwa nimbakaji tu....na hicho cheo ndicho kinamweka pabaya zaidi ya kuwa anatumia madaraka ya umma kudhulumu haki za watoto kama una ushidi wakilisha polisi akamatwe haraka...................mtoto chini ya sheria hajui sheria hata kama anafanya kwa kupenda mwenyewe..............

huyo waziri ni-PM nianze kuchapa kazi ya kumtia kitanzini......ningependa awe mfano wa kuigwa.........hata Dpp asiweze kumbadilishia hati ya mashitaka na kuiita manslaughter kama alivyofanya kwa ukiwaona Ditopile Mzuzuri......lol
 
Well said mkuu,cha ajabu bado wengi hawatakuelewa...kwa maelezo yako unakuja kwenye hoja yangu,kwamba kuna sababu nyingi za Lulu kuonekana hana hatia na chache kuonekana ana hatia..80% innocent 20% guilty

hakuna nusu nusu hapa....................Lulu is innocent......and she is a victim of concerted rape for many years down the road.........mwendazake ndiye mbakaji na anapaswa kulaumiwa kwa yote...........................hao wengine kutonielewa ni haki yao.........it is free World.......
 
mimi,kanumba na mh waziri wote tuliamini kuwa Lulu ana miaka 18 kwa mujibu wa maelezo aliyotoa yeye mwenyewe kwenye vyombo vya habari na hakuna aliyewah kukanusha hilo hata mama yake mzazi, sasa je kanumba angejuaje kuwa huyu bint yuko na miaka 17?
 

haya maneno yanaweza kuwa madogo sema ukiangalia ushahidi wa kumazingara inatisha...nasikia tatizo la ARV wazungu walichotufanya wametutengenezea mazingira tuwahi kufa unafutuka af ukimix na vilevi ndo kabisaa....hatari kwelikweli kwa sisi vijana
 
Wachangiaji, mie sijasomea sheria ila nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa mijadala inayohusiana na kesi kama hizi.

Kuna kampuni fulani USA ilichukua binti mmoja na binti akaweka sahihi kuwa ameshamaliza miaka 18 na wakamchezesha film ya ngono. Baada ya miaka zaidi ya 10, ikaja kufumuka kesi ya binti kuwa alidanganya jina sehemu fulani na hapo ikafumuliwa historia yake nzima na mwisho wa siku ikaja kuonekana alishacheza hadi Porn. Walipufuatilia kiumri, wakakuta kuwa wakati anacheza hizo film, alikuwa hajatimiza miaka 18 na unaambiwa hiyo kampuni ya Porn walianza kuhaha baada ya kugundua kuwa waliingizwa mjini na huyo binti kabla hata hawajafuatwa kushtakiwa. Binti wala hakuwa na matatizo nao kwani yalikuwa ni makosa yake ila kisheria, moto uliwaka.

Roman Polanski, huyu mzee hadi leo hawezi kufika USA. Mwaka jana kama sikosei alikamatwa na habari zake kuandikwa sana kwenye media. Huyu Mzee si kuwa yule mama (Wa miaka zaidi ya 40 sasa) anataka kumshtaki ila ni SHERIA za USA ndiyo zinamtafuta kwa usiku na mchana na siku akikanyaga tu USA, imekula kwake.

Tanzania tuna Sheria zetu na MILA/DINI zetu. Hizi wakati mwingine huingiliana sana na hata mahakimu wanaweza kufumbia macho sheria za nchi na kuziacha sheria za dini/mila zifanye kazi yake. Kwa mfano nilishashuhudia kwenye train, jamaa mmoja aliyekuwa akiwatukana Wanyamwezi safari nzima. Tumeshakaribia Dodoma, mzee mmoja wa Kinyamwezi akamsfia huyo kijana kuwa ana saa nzuri sana na anaomba aione. Yule Mgogo akavua saa na kuisifia sana na mwisho akamkabidhi yule mzee wa Kinyamwezi na Mzee yule akampa ASANTE nzito sana na kuichukua ile saa na kuivaa. Niliona yule kijana wa Kigogo akinywea na nilipodadisi nikaambiwa kuwa ile ndiyo imekwenda kwani kimila, alitakiwa kuiweka chini na na yule mzee aichukue ila ukishampa mtani wako kitu mkononi, basi kimekwenda. Ninajiuliza hapa kama yule kijana angelikuja juu na kesi iende Mahakamani, ingelikuwaje? Si ajabu badi angelishindwa kesi ingawa hakuna sheria kama hii ya mila.

Kwa maana hiyo, Tanzania kuna ndoa hadi za mabinti wa miaka 13 na watu wanaona hilo. Ila hapa ni MILA zaidi zinatawala na watu wanafumbia macho ila mtu akiamua kwenda mahakamani kwa sababu moja au nyingine basi wewe Mbaba imekula kwako. Pia wakati mwingine tukumbuke kuwa mtu unaweza kumuoa binti na usimwgilie na kusubiri kwanza akue (mhh!?!?!) na pia unaweza kuwa hujamuowa na ukaanza kumwingilia (Fataki). Kwa hiyo hata Kanumba (RIP) kama alikuwa katangaza uchumba, si lazima awe alishaanza kuliembelea machimbo ya mfalme Suleiman.

Lulu kuna kila dalili kuwa ugomvi ulikuwa ni SIMU ALIYOPIGIWA. Ila kama atataka kujinasua kwa udi na uvumba jambo ambalo wengi wetu tungelifanya, basi anaweza kutumia mtindo wa C. Ronaldo kwa kudanganya. Nilishakaa na mama mmoja kutoka majuu ambaye anafanya kazi ofisi ya Wana sheria na akaniambia mbinu kadhaa chafu sana ambazo hutumika kushinda kesi kwa akina mama/dada ili waweze kubaki na watoto. Mara nyingi hutumika mbinu mbili:
1. Mama kurudi nyumbani (hasa sehemu za magorofa) na kufungua dirisha na kuanza kupiga kelele kama vile anapigwa na kulia sana ili majirani wasikie. Majirani baadaye huwekwa sawa na mahakamani wakiitwa watadai ni kweli walikuwa wasikia mamaa akilia na kupiga kelele za maumivu na kudai "Leave me alone....."

2. Baba ni PEDOPHILE. Hii hata ucheze vipi, hutoki maana ni wewe sasa inabidi uthibitishe kuwa siyo. Kibaya zaidi ambacho wengi wanasahau ni kuwa sisi wanaume wengi wetu, popote pale ulipo, unakuwa na KIFAA CHA KUBAKIA. Hivyo kukusakizia kuwa ulitaka kubaka ni kazi rahisi sana na inatakiwa kusema tu.

Kuhusu Binti kukamatwa, inaweza kuwa ina upande wa pili wa shilingi maana kwa usalama wa binti na ukiangalia watu walivyo na hasira, binti angeliweza kupigwa hata kuuliwa. Lakini ukiangalia mashtaka yanayowekwa mbele yake kwa kweli ni kasheshe na inanikumbusha hukumu ya Lema ambapo vifungu vya hukumu vimechanganywa. Kwa Tz hilo kwa sasa wala si ajabu maana ukiona shirika zima la Air Tanzania lina ndege moja tu.... ila wafanyakazi ni wangapi sijui.
O.J. Simpson kesi yake ilikuwa wazi kabisa ila kwa ujingwa wa Mapolisi wakiamini kuwa wameshamdaka Mpingo na wakaanza kufanya mambo huku wamejisahau ila lilipowekwa kundi la Mawakili huku Baba yake Kim Kardashian (Marehemu Robert Kardashian) akiwa pale mbele kama Wakili na Rafiki, yalianza kusomwa makosa moja baada ya jingine na mwisho wa siku ikaonekana jamaa alikuwa hana hatia.

Sijui huyu DPP amejiandaaje ila kwa kufahamu ufanyaji kazi wetu hapa Tanzania ulivyo, lolote laweza kufanyika. Wapo jela watu kibao waliobambikiwa kesi na wakafungwa. Kwa ufupi mahakama zetu si huru na zinategemea sana Wakubwa wameamua nini au TAJIRI kaamua nini. Ndiyo maana aliyemsukuma mtu anashitakiwa kwa MAUWAJI na aliyetowa bastola na kumlima driver risasi (Ditopile) anashitakiwa kwa kuuwa bila kukusudia. Hapa sasa ndipo DPP watu wanaanza kumuwekea mashaka sana.

Niliongea na Kanumba mwaka jana kwa simu na nikawa na mipango fulani naye huko mbeleni. Nimesikitika sana kifo chake na hasa ukichukulia alikuwa Ngosha mwenzangu (ndiyo maana namwita homeboy). Ila kwenye hii kesi, naona BAHATI MBAYA iliyotokea, watu wanataka kumbebesha huyu binti. Kitabia, hawa wasanii wetu wengi wao wanatisha na hiyo bahati mbaya angeliweza kuwa hata Lulu leo hii akawa Marehemu.

Naomba tusome maoni/maswali ya Kintinku ambayo ukiyasoma, unaona kuwa ndiyo maswali ya msingi ya Mkuu wa Mashtaka anapoanza kupeleleza. Kuna watu wengi sana wanatakiwa kujibu hiki kifo na mwisho wa siku, jamaa nzima ianze kufundishwa jinsi ya nini cha kufanya mtu akiumia au kupoteza fahamu. Inaonekana Kanumba aliachwa kwa muda mrefu bila ya kupata huduma kwa sababu moja au nyingine jambo ambalo unashindwa kuelewa lilifanywa kwa makusudi au lilifanywa kwa bahati mbaya. Ni sawa na wengine wanaosema kuwa "Mkapa alijua NYERERE ni Mgonjwa na akamuacha huko kijijini kwake hadi alipoona hali imekuwa mbaya kabisa ndipo akaja kutoa msaada. Ila alijua kuwa imeshatoka." Hapa kosa la Mkapa linakuwa ni huo Uzembe wake ila nao unagawanyika - Uzembe alijua au hakujua anafanya uzembe. Wanaosema Mkapa kamuuwa Nyerere, wanasema hivyo kwa sababu alifanya uzembe kwa makusudi. Na bado walipomfikisha London, hakupelekewa hotelini moja kwa moja hadi alipozidiwa.

Sasa kwa Kanumba, kwa nini walipoona mtu anatoka povu, wakaganda dakika kibao bila ya kumpeleka hospital? Na kwanza wakampitisha POLISI, duhh..... eti kuchukua PF3 sijui? Kaazi kweli kweli. Nafikiri wote tusibishane tu na haya mawazo ya Ruta ila tuende zaidi kwenye maswali ya Kintiku ambayo ndiyo maswali ya msingi. RIP Kanumba.
 
1.Hebu rejea criminal responsibility kuhusiana na age.......nasikitika kuona unashadadia eti "hana kesi ya kujibu kwasababu ana miaka 18"

2. hawezi kufanikiwa na issue ya malicious prosecution kwa vile alikuwa na marehemu wakati wa tukio
 
Je kuna ripoti yyt ya daktari inayoonyesha kuwa Kanumba alikua na ugonjwa wa Kuanguka,Moyo,presha na magonjwa mengine ambayo yalikua yanamfanya aanguke? Km hakuna basi lulu anahusika
 
unless the woman is his wife who is fifteen or more years of age and is not separated from the man.[SUP][SUP][2][/SUP][/SUP]

kwa hiyo wataka kusema lulu alikuw mke wa mwendazake wajamani.............hii sasa mpya.............na walikuwa wakiishi wote ili kumwondolea mwendazake tuhuma za kubaka?....................inanichekesha kwa hii mitazamo feki ambayo hata DPp hatakubali aende mkichwamkichwa hivyo............
 
Je kuna ripoti yyt ya daktari inayoonyesha kuwa Kanumba alikua na ugonjwa wa Kuanguka,Moyo,presha na magonjwa mengine ambayo yalikua yanamfanya aanguke? Km hakuna basi lulu anahusika

hivi kuanguka lazima iwe ni kabla ya tukio au hata siku ya tukio ikiwa ya kwanza kwani ipo shida gani...........kuanguka mtu si anaanguka tu kwa sababu zake..............hivi Lulu anahusika kwa vipi.......kugoma kubakwa ndiyo kosa lake kama lipo na mwendazake alipata mshtuko mkubwa baada ya kuona kakatiwa laini aliyozoea.............na kuona kumbe binti anao wengineo..............akajidondokea mwenyewe........
 
mwisho wa siku KOSA LA MAREHEMU BABA .......
 
uliposema tu DPP anafanya kazi kwa mashinikizo ya mob justice ndipo umeniondolea hamu ya kusoma post yako. Si angefanya hivyo kwa kesi mliyoishabikia sana ya Zombe?
kwangu mimi hata asipofungwa kwa murder basi angalau kwa manslaughter kwa ushahidi wa kimazingira
kwanza ndiye mtu pekee aliyekuwa nae chumbani wakati hayo yanatokea.
Pili hata kama waligombana, kiasi cha ugomvi wa marehemu kitakuwa less and less kwavile alifariki na kifo chaweza kuwa kilitokana na execessive provocation au kusukumwa hadi chini kutokana na kutokuwa na nguvu kwavile alikunywa etc. Hayo ya simu messages na mengine yatasadia tu kuthibitisha lakini the gal ana hatia bwana. Tusikimbie ukweli
 
haka KADEMU mi sikaiti katoto mana kameshakubuhu, haka kademu kana kesi 2 ya 1. Kujihusisha na ngono "uasherati" kakiwa na umri mdogo 2. Kumuua mpenzi wake. HATA MKIKAFUNDISHA KASEME UONGO HUKUMU YAKE ITAKUWA HAPAHAPA DUNIANI na wala hakatafika mbali.
 
1.Hebu rejea criminal responsibility kuhusiana na age.......nasikitika kuona unashadadia eti "hana kesi ya kujibu kwasababu ana miaka 18"

2. hawezi kufanikiwa na issue ya malicious prosecution kwa vile alikuwa na marehemu wakati wa tukio

hizi khoja umeziokota wapi? utetezi wake ni kuwa yuko chini ya miaka 18................kwa hiyo mwendazake alikuwa ni mbakaji tu naye alikuwa anajilinda asibakwe...........swala ala malicious prosecution linakuja ya kuwa anapokufa mtu siyo lazima kila aliyekuwepo anahusika na kifo chake...................watu hufa kila siku mbele ya ushuhuda wa wengi na hili ni moja wapo..........malaicious prosecuition inakuja DPP pale anapoaamua kumtia ndani wakati hana ushahidi wowote wa ya kuwa kuna mauaji na hata kumfungulia kesi hata kabla ya taarifa za kitaalamu cha kilichomwuua mwendazake hakijulikani...........hapo DPp inakula kwake kuwa aliyafanya haya yote akijua na kuzififilisha haki za Lulu za kuwa huru na kumwoongezea karaha nyingi ikiwemo ya kushushiwa hadhi mbele ya jamii kuwa ni muuaji wakati DPP hajafanya uchunguzi wa kina................kuwepo au kutokuwepo siyo khoja bali khoja ni je DPP alikuwa ana taarifa za kutosha za kumtia nguvuni na kumfungulia kesi ya mauaji................jibu hakuwa na ushahidi wowote ule naye amekaririwa akisema ahivyo ya kuwa anasubiri taarifa mbalimbali zikiwemo za mkemia mkuu, kampuni za simu, post-mortem ripoti..........sasa DPP anajuaje hata kama kuna mauaji kwenye mazingira ya namna hii??????????
 
mwendawake kivipi ??hiyo si ndio anachomokea unawezaje kumweka mtoto chini ya miaka 18 kama mwendani wako kwanza wewe ulieandka huna adabu kabisa ...sheria ipi inaruhusu kuweka ndani chini ya miaka 18...labda sheria za nchi zinasemaje

1..mtu akikaa naa mwenzake zaidi ya miaka miwili anahesabika kama mkeewe
kanumba ajafikisha hata mwaka akiwa na lulu
2..kanumba akupata kufunga ndoa na luulu so mahusiano hayo ayajulikani kisheria
3..kanumba atashtakiwa kwa kesi si tu ya kubaka bali ni pamoja na uzinzi kama wale makahaba wanokamatwa pale sinza na kuishia kwenye ma landrover ....
4..nafikiri muda mufaka saasa familia ya kanumba kuingilia kati nakutoa tamko else yanakuja ya ajabu ambayo lulu akipewa funguo la mdomo afungue naamini akuna atakaeamini..sitaki kuingilia sheria wacha tuiache ifwate mkondo wake.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…