UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka...


Aluta continue..............
 
Wewe ndiyo unajua hilo leo? Tuache wanasheria wafanye kazi yao, tusianze kuhukumu kabla, AKUTWE NA HATIA AU ASIKUTWE NA HATIA, AWE AMA ASIWE MTOTO, LULU ANA MAMBO YA KIUTU UZIMA...KALE SIYO "KATOTO LUTASHUBANYUMA KANABEBA WAZEE KUZIDI WEWE"

ni kweli malezi ni mabovu lakini kinda nikinda tu hana makosa.............anahitaji kulelewa siyokusingiziwa kesiya mauaji ambayo ni hewa.......................kama ni kumsaidia zipo njia mbadala nyingi lakini huu ni uonevu usio na kipimo..........tumwogope Mungu asije akatulaani kwa hii dhuluma........
 
Kishoka_Zumbu wewe ni kishoka kweli.maelezo yako yana migongano...........hiyo nyekunde umejihami kuwa unadhani............basi mwenzetu endelea kudhani................mimi sina muda wa kudhani ila ninaongelea uzoefu wa kesi za namna hii duniani................defence ya provocation.......is always available in murder case...............na attempted rape is wholly provocation..........
 
mwalimu wake na mlezi wake katika sanaa

mbakaji ni mbakaji tu........tuikemee wabakaji wanadhalilisha jamii nakuturudisha enzi za stone age........
 

DOTTO MUNGO........commonsense is the best of senses..........
 
Kwa maoni yangu ni kwamba Elizabeth Michael "Lulu" ameshatoka/yupo huru kabla ya Kesi kuanza kusikilizwa. Nitafafanua

Kesi aliyofunguliwa Lulu ni ya mauaji (yaani anashitakiwa kwa kosa namba moja la kumuua Mwendazake Steven Kanumba)

Kwa kosa hilo Mahakama itahitaji kumtia hatiani Lulu kwa ushahidi usio na mashaka ya namna yoyote (beyond any reasonable doubt) kwamba ni kweli Lulu alimuua Steven Kanumba.

Kitu ambacho nina uhakika, shahidi/mashahidi ama mahakama haitoweza kulithibisha hilo kwa ushahidi wa kimazingira na kitabibu ambao wanao mpaka muda huu mahakama.

Ushahidi wa Kimazingira kama ilivyoripotiwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni CSP Charles Kenyela.

1. Ni kwamba marehemu hakuwa na jeraha lolote mwilini lakini pia haukukutwa na sumu yoyote (labda kama mkemia mkuu atakuja na matokeo tofauti ya uchunguzi), hii taarifa ni kwa mujibu wa maelezo ya madaktari waliouchunguza mwili wa marehemu kabla ya kuruhusu kuzikwa.

2. Chumba ambacho marehemu alikutwa amekufa kilikutwa na vinywaji, kilevi aina ya Jack Daniel na soda Sprite.

3. Kama hivi vinywaji vitaonekana na sumu iliyopelekea kudhuru/kumuua mwendazake Steven Kanumba, mahakama kupitia mashahidi na ushahidi usio na mashaka inakazi ya kuthibisha kuwa ni Lulu ndiye aliyeweka sumu hiyo.

4. Pia chumba hicho kilikutwa na panga lakini marehemu hakuwa na jeraha la namna yeyote, isipokuwa mshtakiwa Lulu amekutwa na majeraha, hapa napo mahakama ina kazi ya ziada kumtia hatiani Lulu.

5. Lakini pia huyo Lulu mwenyewe amekutwa akiwa na majeraha (hapa mahakama inakazi ya kuthibitsha kuwa haya majeraha hayakusababishwa na marehemu Steven Kanumba)

6. Kwa Mazingira hayo, achia mbali swala la umri na tabia binafsi za Lulu, kumtia hatiani Lulu kwa shitaka la Mauaji/kumuua marehemu Steven Kanumba kwa ushahidi wa mtu aliye nje ya chumba lilipotokea tukio ni ngumu sana. Labda kidogo kama kesi inayomkabili ingekua ni kuua bila kukusudia (manslaughter)

Mwisho napenda niwakumbushe hukumu iliyotolewa mwaka juzi iliyokua ikimkabili Abdalah Zombe kwa shitaka namba moja la kuwaua wafanyabiashara watatu wa madini wanaotokea mahenge morogoro.
akiwemo na dereva teksi wa sinza Ndugu Juma. Hukumu ilitolewa na Abdalah Zombe aliachiwa huru (yaani mahakama ilishindwa kumtia hatiani kwa kosa lililokuwa likimkabili la mauaji)

Hapo juu naomba niseme kwamba ama mahakama ilifungua kesi kwa kujua kwamba haitoweza kumtia hatiani ama walijua kuwa ni lazima watathibisha kuwa aliua lakini ukweli ni kwamba mwisho wa siku hakuna shahidi aliyethibitisha kuwa Zombe aliua.

Pia katika kesi ile mara baada ya watu kulalamikia hukumu, Jaji alisema kwa shitaka lililofunguliwa huwezi kumtia hatiani Zombe labda kama kosa lililokua linamkabili lingekuwa ni kosa la kutoa order hao wafanyabiashara wauawe, kwahiyo mwisho wa siku mawakili upande wa serikali walishindwa kesi.

Kwa mazingira hayohayo pia inawezekana Mahakama wakawa wamemfungulia kesi ya Mauaji Lulu wakijua kwamba kwa mazingira ya tukio hakuna mahala ama shahidi/ushahidi utakaothibisha kuwa Elizabeth Michael "Lulu" kuwa ameua na hivyo kuona hana hatia na jaji kuamua kumuachia huru.

Sometimes these prosecutions are being handled techniacally to save the accused person before the case begin.

R.I.P Steven Charles Kanumba
 

DOTTO MUNGO........commonsense is the best of senses..........
 

unadai kuna dili kati ya polisi na mtuhumiwa.....................If you believe this then you will believe anything.....
 
Bila ya kuleta blah blah, LULU anakabiliwa na matatizo makuu mawili

1. Tatizo la kisheria la kuhakikisha kuwa hatiwi hatiani kwa tuhuma zinazomkabili kisheria

2. Tatizo la pili ni kuhakikisha jamii haimuoni kama manipulator na muuaji anayeweza kufanya chochote ili kujinasua na mkono wa sheria na hivyo kuifanya jamii imhukumu. Katika hili la pili LULU anaweza kulikabili kwa kuwa tayari kuongea ukweli katika lile la kwanza bila kuonesha kuwa anambebesha marehemu mzigo wa kubaka, kudhalilisha au hata kumuonesha kuwa alikuwa ni sex predator. Kwa sasa jamii inamuona marehemu kuwa ni victim kwa sababu tu amepoteza maisha na LULU na wanasheria wake wanatakiwa kujua kuwa hawatakiwi kutumia hila yoyote kumbadilishia kibao marehemu ili tu LULU a walk freely.

Kwa kweli inahitajika balance ya hali ya juu kwenye hili katika kumrudishia LULU maisha yake ya kawaida. Otherwise awe tayari kwenda kuishi nje ya Tanzania nako itakuwa ngumu kwa tuhuma zilizowahi kumkabili. Binafsi nisingependa LULU awe guilty kwanza katika sakata hili yeye ni muathirika wa kwanza wa kifo cha Kanumba kwani alikuwa ni mwandani wake na mengi yanaongewa nyuma ya pazia kuhusu future plan ya wawili hao.

Kwa kuwa LULU amewahi kutamka kwenye public kuwa yeye ni 18 years old, anaweza kukubali kosa kuwa alidanganya ili kupata advantages za adults na ndicho kilichomfanya marehemu kumuomba kuwa wapenzi ila kwa kuwa alikuwa anaongea kwenye vyombo vya habari bila kuwa under oath basi akiwa under oath anaongea ukweli kuwa yeye si 18 bali ni 17 years old. All in all LULU na timu yake ya utetezi watakuwa wanaharibu sana kama kwa njia yoyote ile wataanza kupeleka lawama kwa mtu asiyekuwa na uwezo wa kujitetea mahamani, marehemu.

Ninachokiona hapa ni LULU kutiwa hatiani kwa makosa ya kudanganya umri na kuua bila ya kukusudia ambapo kwa umri wake anaweza wekwa chini ya jela ya watoto kwa miaka miwili au mitatu na kisha kuachiwa na kuja kujiunga na jamii akiwa mtu mpya na mwenye kujutia kumpoteza mpenzi wake.
 
Lulu ana mwili mdogo sana ukilinganisha na Kanumba. Je alitumia nguvu gani kuweza kumsukuma Kanumba hadi aanguke?
Kwa sababu walikuwa wawili chumbani basi mtu pekee ambaye anaweza kusema kilichompata Kanumba ni Lulu mwenyewe hata kama kitakuwa cha uongo na hakutakuwa na mtu wa kuthibitisha kuwa ni uongo. Kanumba angekutwa amejeruhiwa kwa kutumia silaha, hapo Lulu angekuwa hana la kujitetea.
Tuiachie mahakama ifanye kazi yake.
 
nimejifunza mengi,uongo saa nyengine huponza.unaweza ukaongopa,na siku utakayokuwa mkweli,utaonekana muongo tu.hiki kitoto kiongo.ila simuombei mabaya,kwani yaliyotokea ni yeye mwenyewe ndie anaejua
 
Kama Maelezo ya seth ni sahihi kwamba Mlango Ulifungwa na funguo wakati walipoanza kutofautiana na kelele kusikika kwa muda ni dhahiri kwamba ALIEFUNGA MLANGO NI MWENYE CHUMBA ITAKUWA VIGUMU SANA KA BINTI MGENI NDANI YA CHUMBA KUCHUKUA MAMLAKA YA KUMFUNGIA NDANI MWENYE CHUMBA (USHAHIDI WA KIMAZINGIRA) NI KAMA KISA CHA NABII YUSUFU KWA WAISLAMU. JERAHA LIPO MBELE AU NYUMA, MBELE NI LA KUSHAMBULIWA, NYUMA NI LA KUANGUKA/KUSUKUMWA/KUPEPESUKA NA HATIMAYE KUANGUKA
 
Jamani tuwe na busara kidogo, huu umoja wa wasanii mimi binfsi ninashangaa sana, msanii mwenzao Lulu amepata matatizo wapo kimya hata kumsaidia hawataki sijui kwa nini.
Kwa mtizamo wangu ninaona Lulu kuna uwezakano mkubwa akaachiwa huru, kwani mpaka sasa sioni kama kuna ushahidi wowote wa kuweza kuthibitisha tuhuma zinazomkabili

  1. Ripoti ya madaktari, kimsingi ripoti hii inamjenga zaidi Lulu kuliko upande wa mashitaka “Prosecution” kwa sababu ripoti hii inaeleza kwamba Mwendazake (Kanumba) kifo chake kimesababishwa na Brain Concussion ambayo inasababishwa na kugongwa na kitu kichwani, majeraha pamoja na kuanguka. This is undisputed facts all we do concur after having read the named report. Lakini haisemi kama Lulu ndio aliyemsukuma ama gonga kichwani marehemu, bado haiweza kuinganisha name alimgonga au mwangusha marehemu, uchunguzi inabidi uende mbali zaidi kuweza kupata ushahidi pasipo shaka/zaidi ya ukomo wa mashaka “ to prove beyond any reasonable doubt” wa kwamba Lulu ndiye aliyemsukuma au mwangusha Kanumba kwa tunakubaliana ripoti ya polisi haiwezi kusisima peke yake kwa hiyo tunaipiga chini/tupa huko!.
  2. Ripoti ya madaktari haikwenda mbali kuweza kubaini kumbukumbu ya marehemu kama kuna magonjwa mengine yalikuwa yanamsumbua marehemu kabla ya kumkuta mauti, kwani hayo ndio yanaweza kuwa ndio sababu ya kifo chake tunapiga tena chini ripoti ya madaktari.
  3. Ripoti ya mkemia mkuu, hata ikisema kulikuwa na sumu, lazima atafuta nani aliiweka hiyo sumu na sio kumsingizia Lulu, vile vile lazima iseme ni sumu ya aina gani na ina uwezo gani wa kuua, je ni kwa muda mfupi namna ile, lakini Kanumba kuwa na sumu sio sababu ya kumfunga lulu kwa sababu inategemeana na sampuli ya machozi au aina yeyote (specimen), imechuliwaje kwa sababu yawezekana hiyo sampuli imechanganyikana na vipondozi anavyotumia marehemu kama mafuta, lotion n.k kwani wazi vipondozi hivi vina sumu kwani kuna wakati TFDA walitangaza vipodozi vyenye sumu, huenda watanzania wengi wana sumu mwilini mwao ndio maana leo kuna dawa za kutoa sumu mwilini, yawezekana hata wewe au mimi tuna sumu.Nayo ripoti tunapiga chini.
  4. Tunakuja kwa polisi hapo ndipo tuna “rise doubt” mpaka mheshimiwa hakimu ashangae kwanza kwa nini mdogo wake na Kanumba hakuwekwa chini ya ulinzi, kwani best practice tunao kwamba mtu akifa watu wote kwenye tukio mnakuwa watuhumiwa, na kama haukuhusika ni baadaye huko mwishoni ndio unatoka, lakini leo tumeona from day one mdogo wake Kanumba yote nje na ana mislead investigation kwenye media. Je hivyo vinywaji ambavyo vinaweza kutumika kama vielelezo vilichukuliwa kwa utaratibu yaani shihidi ni nani(independent witness/shahidi huru) ie mwenyekiti wa serikali za mitaa, mjumbe kama hakuwepo tunavipiga chini. Kwani mdogo wake haiwezekani amuwekee sumu kaka mtu tumeona matukio kibao ndungu wanauana. Kumbuka vinywaji hivyo Kanumba alikuwa anavnywa kabla possible mtu mwingine akawa amemuwekea. Vile vile polisi hawakumkamata Lulu alienda mwenyewe polisi hii ni ushahidi tosha kwamba alikuwa hana nia ya kuua, vile vile yeye ndiye toa taarifa kwa mdogo wa marehemu na kutoa ushirikiano.
  5. Caution or plain statement ya polisi tunaipiga chini, regardless imechukuliwa chini ya kiapo kama kuna vitu amekiri (confess) basi tunaamsha taratibu za kukiri lazima awepo mlinzi wa amani tofauti na hapo tunapiga chini.
  6. Ni nani alimwita mwenziye kati ya Kanumba au Lulu kama ni Kanumba alimwita aende nia ya kuua tunaitilia shaka, siku zote mwenye nia ya kuua haitwi anakuja mwenyewe na kutekeleza azma yake.
  7. Kuna ushahidi gani kwamba Lulu alikuwepo chumbani kwa Kanumba, ushahidi wa mdogo wa kunumba unapigwa chini kwa sababu kimsingi nay eye anatakiwa awe mtuhumiwa na vile vile ana maslahi kwa marehemu(bias/interested).
  8. Mwili wa marehemu umezunguka sana kabla ya polisi kuanza uchunguzi kiasi kwamba umebadili mwelekeo wa uchunguzi makini, kwanini polisi hawakuweza kufika eneo la tukio na kuzuia kwa ajili ya uchunguzi na kuchukua taarifa mbalimbali ie finger prints za maeneo mbalimbali kama vitasa, glass, chupa za vinywaji n.k
  9. Baada ya hapo tunakuja na defence ya kwamba Marehemu alitaka kubaka mpendwa wetu Lulu kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 132 (Penal code contray to Sect 132.)
    1. 132. Attempted rape Act No. 4 of 1998 s. 8
(1) Any person who attempts to commit rape commits the offence of attempted rape, and except for the cases specified in subsection (3) is liable upon conviction to imprisonment for life, and in any case shall be liable to imprisonment for not less than thirty years with or without corporal punishment.
(2) A person attempts to commit rape if, with the intent to procure prohibited sexual intercourse with any girl or woman, he manifests his intention by–
(a) threatening the girl or woman for sexual purposes;
(b) being a person of authority or influence in relation to the girl or woman, applying any act of intimidation over her for sexual purposes;
(c) making any false representations for her for the purposes of obtaining her consent;
(d) representing himself as the husband of the girl or woman, and the girl or woman is put in a position where, but for the occurrence of anything independent of that person's will, she would be involuntarily carnally known.
(3) Where a person commits the offence of attempted rape by virtue of manifesting his intention in the manner specified in paragraph (c) or (d), he shall be liable to imprisonment for life and in any case for imprisonment of not less than ten years.

  1. Lulu ni girl or woman na tafsiri inapatikana katika sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 129A. Definition of woman
In this Chapter "woman" means any female person and, unless the context requires otherwise or it is otherwise expressly provided, irrespective of age.

  1. Mwisho, na ikumbukwe kwamba kazi ya mtuhumiwa ni kutia shaka juu ya hoja zinazotolewa na upande wa mashitaka, upande wa mashitaka una jukumu la kuthibitisha tuhuma pasipo acha shaka tuhuma inayo mkabili mtuhumiwa. Lulu hana hatia ila tu kwa mfumo wetu wa uendeshaji wa mashitaka huwa unachukua muda mrefu ndio ambayo itamgharimu. Na nyinyi maaskari wa kike ambao mnamsindikiza Lulu mahakamani naomba muwe mnampa ushauri na kumtia moyo msimtenge sana ni mwanamke mwenzenu.
 
Jamani inshu iko mahakamani mbona mmekuwa na jazba
kuweni wapole punguzeni jazba au nendeni mahakamani mkatoe utetezi wenu
 
Wanasema si rahisi kuwa mtaalamu wa kila kitu...ila kila mtu anaweza kuwa informed lakini asijue technical know how. Mtoa hoja hii - @Ruta anashindwa kuelewa kuwa hakuna uhusiano kati ya umri na kosa nanalotuhumiwa kwalo.

Ni vigumu kutaka watu waamini kuwa ukiwa under 17 huwezi kutuhumiwa kufanya kosa katika nchi hii. Niseme swala si kuwa anapashwa kuwa huru au la...tumeona kesi ambazo ni damaging (Zombe, Vijana waliouawa na Polisi Arusha etc) kuliko hii ya Lulu. Ukweli ni kwamba Lulu anayotuhuma ya kujibu period.
 

Soma tena ulichokiandika labda utagundua kitu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…