Jamani tuwe na busara kidogo, huu umoja wa wasanii mimi binfsi ninashangaa sana, msanii mwenzao Lulu amepata matatizo wapo kimya hata kumsaidia hawataki sijui kwa nini.
Kwa mtizamo wangu ninaona Lulu kuna uwezakano mkubwa akaachiwa huru, kwani mpaka sasa sioni kama kuna ushahidi wowote wa kuweza kuthibitisha tuhuma zinazomkabili
- Ripoti ya madaktari, kimsingi ripoti hii inamjenga zaidi Lulu kuliko upande wa mashitaka Prosecution kwa sababu ripoti hii inaeleza kwamba Mwendazake (Kanumba) kifo chake kimesababishwa na Brain Concussion ambayo inasababishwa na kugongwa na kitu kichwani, majeraha pamoja na kuanguka. This is undisputed facts all we do concur after having read the named report. Lakini haisemi kama Lulu ndio aliyemsukuma ama gonga kichwani marehemu, bado haiweza kuinganisha name alimgonga au mwangusha marehemu, uchunguzi inabidi uende mbali zaidi kuweza kupata ushahidi pasipo shaka/zaidi ya ukomo wa mashaka to prove beyond any reasonable doubt wa kwamba Lulu ndiye aliyemsukuma au mwangusha Kanumba kwa tunakubaliana ripoti ya polisi haiwezi kusisima peke yake kwa hiyo tunaipiga chini/tupa huko!.
- Ripoti ya madaktari haikwenda mbali kuweza kubaini kumbukumbu ya marehemu kama kuna magonjwa mengine yalikuwa yanamsumbua marehemu kabla ya kumkuta mauti, kwani hayo ndio yanaweza kuwa ndio sababu ya kifo chake tunapiga tena chini ripoti ya madaktari.
- Ripoti ya mkemia mkuu, hata ikisema kulikuwa na sumu, lazima atafuta nani aliiweka hiyo sumu na sio kumsingizia Lulu, vile vile lazima iseme ni sumu ya aina gani na ina uwezo gani wa kuua, je ni kwa muda mfupi namna ile, lakini Kanumba kuwa na sumu sio sababu ya kumfunga lulu kwa sababu inategemeana na sampuli ya machozi au aina yeyote (specimen), imechuliwaje kwa sababu yawezekana hiyo sampuli imechanganyikana na vipondozi anavyotumia marehemu kama mafuta, lotion n.k kwani wazi vipondozi hivi vina sumu kwani kuna wakati TFDA walitangaza vipodozi vyenye sumu, huenda watanzania wengi wana sumu mwilini mwao ndio maana leo kuna dawa za kutoa sumu mwilini, yawezekana hata wewe au mimi tuna sumu.Nayo ripoti tunapiga chini.
- Tunakuja kwa polisi hapo ndipo tuna rise doubt mpaka mheshimiwa hakimu ashangae kwanza kwa nini mdogo wake na Kanumba hakuwekwa chini ya ulinzi, kwani best practice tunao kwamba mtu akifa watu wote kwenye tukio mnakuwa watuhumiwa, na kama haukuhusika ni baadaye huko mwishoni ndio unatoka, lakini leo tumeona from day one mdogo wake Kanumba yote nje na ana mislead investigation kwenye media. Je hivyo vinywaji ambavyo vinaweza kutumika kama vielelezo vilichukuliwa kwa utaratibu yaani shihidi ni nani(independent witness/shahidi huru) ie mwenyekiti wa serikali za mitaa, mjumbe kama hakuwepo tunavipiga chini. Kwani mdogo wake haiwezekani amuwekee sumu kaka mtu tumeona matukio kibao ndungu wanauana. Kumbuka vinywaji hivyo Kanumba alikuwa anavnywa kabla possible mtu mwingine akawa amemuwekea. Vile vile polisi hawakumkamata Lulu alienda mwenyewe polisi hii ni ushahidi tosha kwamba alikuwa hana nia ya kuua, vile vile yeye ndiye toa taarifa kwa mdogo wa marehemu na kutoa ushirikiano.
- Caution or plain statement ya polisi tunaipiga chini, regardless imechukuliwa chini ya kiapo kama kuna vitu amekiri (confess) basi tunaamsha taratibu za kukiri lazima awepo mlinzi wa amani tofauti na hapo tunapiga chini.
- Ni nani alimwita mwenziye kati ya Kanumba au Lulu kama ni Kanumba alimwita aende nia ya kuua tunaitilia shaka, siku zote mwenye nia ya kuua haitwi anakuja mwenyewe na kutekeleza azma yake.
- Kuna ushahidi gani kwamba Lulu alikuwepo chumbani kwa Kanumba, ushahidi wa mdogo wa kunumba unapigwa chini kwa sababu kimsingi nay eye anatakiwa awe mtuhumiwa na vile vile ana maslahi kwa marehemu(bias/interested).
- Mwili wa marehemu umezunguka sana kabla ya polisi kuanza uchunguzi kiasi kwamba umebadili mwelekeo wa uchunguzi makini, kwanini polisi hawakuweza kufika eneo la tukio na kuzuia kwa ajili ya uchunguzi na kuchukua taarifa mbalimbali ie finger prints za maeneo mbalimbali kama vitasa, glass, chupa za vinywaji n.k
- Baada ya hapo tunakuja na defence ya kwamba Marehemu alitaka kubaka mpendwa wetu Lulu kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 132 (Penal code contray to Sect 132.)
- 132. Attempted rape Act No. 4 of 1998 s. 8
(1) Any person who attempts to commit rape commits the offence of attempted rape, and except for the cases specified in subsection (3) is liable upon conviction to imprisonment for life, and in any case shall be liable to imprisonment for not less than thirty years with or without corporal punishment.
(2) A person attempts to commit rape if, with the intent to procure prohibited sexual intercourse with any girl or woman, he manifests his intention by
(a) threatening the girl or woman for sexual purposes;
(b) being a person of authority or influence in relation to the girl or woman, applying any act of intimidation over her for sexual purposes;
(c) making any false representations for her for the purposes of obtaining her consent;
(d) representing himself as the husband of the girl or woman, and the girl or woman is put in a position where, but for the occurrence of anything independent of that person's will, she would be involuntarily carnally known.
(3) Where a person commits the offence of attempted rape by virtue of manifesting his intention in the manner specified in paragraph (c) or (d), he shall be liable to imprisonment for life and in any case for imprisonment of not less than ten years.
- Lulu ni girl or woman na tafsiri inapatikana katika sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 129A. Definition of woman
In this Chapter "woman" means any female person and, unless the context requires otherwise or it is otherwise expressly provided, irrespective of age.
- Mwisho, na ikumbukwe kwamba kazi ya mtuhumiwa ni kutia shaka juu ya hoja zinazotolewa na upande wa mashitaka, upande wa mashitaka una jukumu la kuthibitisha tuhuma pasipo acha shaka tuhuma inayo mkabili mtuhumiwa. Lulu hana hatia ila tu kwa mfumo wetu wa uendeshaji wa mashitaka huwa unachukua muda mrefu ndio ambayo itamgharimu. Na nyinyi maaskari wa kike ambao mnamsindikiza Lulu mahakamani naomba muwe mnampa ushauri na kumtia moyo msimtenge sana ni mwanamke mwenzenu.