Unajua kuna watu humu wamesoma Bsc (civil) Eng; na M.A (Public Admin) na ni watu wazima sana halafu wao ndo wanajiona Wanasheria waliofuzu kumbe wanapotosha umma.
Sheria ya mwenendo wa kesi ya kubaka ni tofauti sana na sheria ya mwenendo wa kesi ya mauaji.
Hebu twende taratibu, Lulu kashtakiwa kwa kosa la mauaji na wala si Kanumba kashitakiwa kwa "Tuhuma za Kusadikika" za Kubaka.
Sheria ya Tanzania inatambua umri tofauti kwa makosa tofauti. Mfano, katika kesi za kubaka ni offence kama ukimbaka mtu mwenye umri chini ya miaka 18.
Wakati huo huo sheria ya ndoa inatoa haki kwa huyu mtoto wa miaka 18 kuolewa kwa ruksa ya wazazi. Wakati Lulu na Kanumba enzi zao walikuwa wanapika na kupakua mama Lulu alikuwa anajua na kuwapa baraka zote. may be kwa kuwa naye aliona matunda yake. Nia ya Kanumba ilikuwa njema kabisa ni Kumwoa Lulu. Mama yake Mlezi Dotnata na Kanumba alifahamishwa hivyo na hata alipomwuliza Lulu kama ataacha Ukicheche aliahidi kuwa atatulia. Kanumba alikuwa anataka kum-transform abadilike. Lulu alikuwa ameiaminisha Dunia kwa matendo na maneno kuwa yeye ni mtu mzima above 18 (Achana na cheti, cheti ni nini bana), ushahidi wa watu wachache wakimshudia kuwa amekuwa akikiri kuwa na umri wa 18 na hivyo kumwaminisha kanumba na watu wengine kuwa yeye ni mtu mzima unatosha kumtia hatiani kama ni binti mwongo na asiyeaminika na hivyo ni mtu mzima ajibu mashtaka. Unajua kusema uongo ni kosa.
Sasa tuangalie umri katika kesi za mauaj: angalia kiambatanishi pia:
"mtu mzima" maana yake ni mtu mwenye umri wa au zaidi ya miaka kumi na sita;
"mtoto" maana yake ni mtu ambaye hajatimiza umri wa miaka kumi na sita;
"Kijana mdogo" maana yake ni mtu aliye chini ya umri wa miaka kumi na sita;
CHAPTER XIXA inazungumzia Murder and Manslaughter
195. Any person who by an unlawful act or omission causes the death of another person is guilty of the felony termed "manslaughter" An unlawful omission is an omission amounting to culpable negligence to discharge a duty tending to the preservation of life or health, whether such omission is or is not accompanied by an intention to cause death or bodily harm.
196. 'Any person who of malice aforethought causes the death of another person by an unlawful act or omission is guilty of murder.
197. Any person convicted of murder shall be. sentenced to death: (of course kuna exceptions)
Nimeongea na Kiongizi mmoja Police Force wa Kitengo cha Crime na haya ndiyo yaliyojili:
1. Ushahidi walionao wa awali unatosha kumshitaki Lulu kwa Murder kwa kuwa ni above 16
2. Bado kuna ushahidi mzito katika simu yake na SMS for last few weeks na huenda kesi hii ikawavuta wengi.
3. Report ya daktari inayoonyesha SK alikufa kwa Brain Concussion imepelekea Police kupata ushahidi wa kitu kilichomgonga, mpiga, au mwangusha wakati muda mfupi tu alikuwa mzima. Report inashuhudia SK hakuwa na maradhi mengine na alikuwa ni mtu wa Gym.
4. Report ya Mkemia Mkuu ambayo inasubiriwa inaweza kuwa na dondoo zingine.
5. Jukumu la mwendesha mashtaka ni kumshtaki mtuhumiwa kwa Murder (ambalo ni kosa la juu) ingawa mahakama kutegemea na uzito inaweza kumpunguzia adhabu ikawa Manslaughter (kosa dogo).
6. Elizabeth alikuwa Mlevi (Only over 18 unaruhusiwa kununua kilevi, alikuwa na mabwana kama alivyowahi kukubali mwenyewe kuwa hakuwa Bikra (na hao nao walikuwa wanambaka?). Yote haya yanahakikisha kuwa binti ni mtu mzima na anaweza kujibu tuhuma za mauaji.
7. Jamuhuri ikishamtia katika hatia kuwa Lulu ni Mwongo mbele ya jamii na kuwa kadanganya miaka na kuwaaminisha watu kuwa yeye ni mtu mzima, basi mziki mnene unamsubiri, maana mahakama tayari inaushahidi kuwa ni Mwongo na anatumia uongo kutake advantage. hapo Wanasheria wazuri au waendesha mashitaka watakuwa na kazi ya kumbomoa kwa kila analosema. Aombe tu yote atakayoongea hayatakinzana na aliyotenda na kufanya na ambayo yatakuwa na ushahidi.
8. Bra bra zingine kuwa Kanumba kabaka bila ushahidi wowote na hayupo kujitetea in nothing other than wishful thinking lakini sheria iko wazi.
Ni vema tuache kupotosha watu na tuiachie mahakama ifanye kazi yake.