Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Mazingira yanaonyesha huenda kweli Sabaya alitumwa na Jiwe.Wakati uharamia huu unafanyika mchana kweupe,Jiwe ambaye ni Amri Jeshi Mkuu,Mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi&Usalama na mwenye jukumu la kulinda wananchi wake alipiga kimya.Kitu Cha kufanya Sabaya ni Kwenda kampuni ya simu kupata ushahidi wa mazungumzo Yao!
 
Kwani mitambo ya kutengeneza fedha fake aliikamata kweli?
Wapi? Kwa order gani? Ya mdomo au waraka?
Kama ni kweli, kwanini hawakutumwa walioko Dar?

Hana hatia. ATACHOMOKA

Wala Luoga hajamtaja kuwa alimtuma ila amesem ANAJUA
 
Kesi ujambazi wako unasingizia ulitumwa na magu, eti gavana na waziri anajua ujambazi wako, so what? Utetezi dhaifu sijawahi sikia. Wanajua kwa utaratibu upi? Shenzi kweli hili toto kumbe sabaya kichwani popompo kabisa. Alitumia ushikaji na marehemu vibaya, akawa anazunguka kupiga pesa. Kwa hiyo nchi ilikuwa ukiwa mshikaji wa Rais basi unafanya chochote kibaya bila kujali sheria na taratibu
 
Hakuna huyu muhuni tu, mwizi, tapeli...kwani hata ingekuwa kweli Rais akikutuma ukaibe ndio dhambi inaondoka, hakutumwa na mtu shenzi hili toto
 
Tusubiri tuone utetezi wako.
 
Kesi imeisha hiyo! Sabaya soon utakuwa uraiani na ingependeza urudi Jimbo la hai ili udili vzr na magaidi
 
Tatizo sio kuagizwa ni je ulifanya makosa wakati wa utekelezaji wa maagizo!? Kumbuka kesi ya Zombe. Mwenye kosa hubeba kosa sio alieagiza.
 
Magufuli aliamini Sabaya ndio anaweza fanya kazi hiyo kwa ufanisi ,na Rais hapangiwi
Huu upuuzi wa eti rais hapangiwi ndiyo maana wananzengo wanapiga kelele za katiba mpya, hata rais kisheria hayuko juu ya sheria.
 
Huwezi kutii amri haramu ya kiongozi yeyote hata kama ni rais.
Huyu ni mjinga pamoja na mawakili wake wote.
 
SAWA.

Sasa tueleze wewe, hawa wote walishindwa kitu gani kulikamata jambazi lililovamia kwenye himaya yao, badala yake wakaliacha tu lifanye uhalifu! Hili ni jambo la kawaida?
 
Huwezi kutii amri haramu ya kiongozi yeyote hata kama ni rais.
Huyu ni mjinga pamoja na mawakili wake wote.
Navoona Saa mbaya alitenda makosa na anajua hivyo kuwa hakuna namna anaweza kujitoa kwenye makosa moja kwa moja; Kwa sababu hiyo sasa anaona kilichobaki ni kuonesha kuwa, pamoja na kuwa ni kweli alitenda makosa lakin alitegemea wale waliomtuma wangemtetea badala yake wamemtekekeza ajijue mwenyewe na yeye sasa kaamua kama ni mbwai acha iwe mbwa tu; ni kama ana hoji "hivi mimi sabaya, katika mazingira ya utawala wa wakati ule, ningeliweza vip kukataa maelekezo (soma AMRI) ya Mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama wa nchi, na tena mkuu huyo ni Jiwe himself?!!!
 
Reactions: Qwy
Hata Yale Makonda alikua anafanya atakua alikua anatumwa na Magu.
 
Reactions: Qwy
Wewe ndio umechafua kabisa uzi kwa kububujikwa na mimatemate, angekuwepo jiwe unadhani hii kesi isingekuwepo.Kwahiyo kupiga simu polisi ndio unahitimisha hakufanya unyang'anyi? Je polisi unajuaje kama na wenyewe hawakua sehemu ya mpango au walipewa maagizo.Japo akili yako unaitumia tu kwenye kupanua mdomo na kutumbukiza kijiko cha chakula jaribu uiboost ikusaidie katika mambo mengine
 
Ana mashtaka ya kubaka, kujeruhi na kupora. Hayo ndio alitumwa?
Utajuaje kama aliamriwa..."wewe fanya rorote almradi utekereze kazi ninayokutuma"...
Tuvute subira, pamoja na ujambaz wake lakin huenda huyu jamaa si mjinga kiasi cha kumtaja Mkuu wa nchi hivhiv tu bila kuwa na chembe yoyote ya ushahidi...na ujue naye ana mawakili wake na huenda pia wapo watu ndani ya hicho chama na ndani ya system wana sypathize naye..
Kuwa mpole mkuu tunywe mtori kwanza, nyama tutazifikia tu.
 
Huu ndiyo uzuri wa waTZ, hasa wapinzani, wape jambo moja tu linalomchafua mtu wanayemchukia wa CCM, then wanasahau mengine yote!! Kwa sasa masuala ya gari la magereza kushindwa kumpeleka Ustaadhi mahakamani, mabalozi mahakamani na Taasisi kubwa kuingilia mahakama yatasahaulika kwa muda!! Jumatatu watu watakuwa seat ya mbele, sikio likiwa limetegwa Arusha kusikiliza Sabaya atamtaja nani tena. Wakitaka wawatoe kwenye reli zaidi awataje Samia na Majaliwa, hapo Bwana ustaadhi atasahaulika hadi October!! Na vyombo vyetu vya habari kwao sasa hii ndiyo itakuwa habari ya kuuza.
 
Hilo swali kwa sheria ipi" hakuna jibu hapo. Kumsave huyu kijana labda iwe amri toka juu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…