Jinai haina muda maalum wa kukamatwa!Sasa kwanini hakukamatwa mara baada ya tukio?!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jinai haina muda maalum wa kukamatwa!Sasa kwanini hakukamatwa mara baada ya tukio?!
Hakuna huyu muhuni tu, mwizi, tapeli...kwani hata ingekuwa kweli Rais akikutuma ukaibe ndio dhambi inaondoka, hakutumwa na mtu shenzi hili totoMazingira yanaonyesha huenda kweli Sabaya alitumwa na Jiwe.Wakati uharamia huu unafanyika mchana kweupe,Jiwe ambaye ni Amri Jeshi Mkuu,Mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi&Usalama na mwenye jukumu la kulinda wananchi wake alipiga kimya.Kitu Cha kufanya Sabaya ni Kwenda kampuni ya simu kupata ushahidi wa mazungumzo Yao!
Tusubiri tuone utetezi wako.Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad.
Akiongozwa na wakili Mosses Mahuna wakati akitoa utetezi wake mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Sabaya alidai yeye bado ni mtumishi wa Serikali ila alisikia tangazo la kusimamishwa kazi kutoka Kwa Rais Samia Suluhu.
Alidai kuwa siku ya tukio Februari 9 mwaka huu majira ya saa 9 kasoro alasiri alipigiwa simu na Mamlaka iliyomteua na kumpatia maelekezo ya kwenda kufanya kazi maalumu Arusha na kumtaka aongozane na watu wanne waliokuwa wakimsubiri uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro KIA.
Sabaya alidai kuwa walipofika Arusha wakiwa na wale watu wanne ambao ndio wenye taarifa zote walielekea eneo husika waliokuwa wameelekezwa na Mamlaka husika katika eneo la duka la Shaahid store lililopo mtaa wa Soko kuu jijini Arusha.
Akihojiwa na Wakili Mahuna kuhusu kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya tarehe 9.2.2021 ,Sabaya alidai alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani kilimanjaro na aliteuliwa na Rais Hayati Dkt John Pombe Magufuli tarehe 29.7.2018.
Lengai Ole Sabaya anaeleza mahakama kuwa alitumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 2 na miezi 10 na alikoma kuhudumu wadhifa huo tarehe 13.5.2021 baada ya Rais Samia Suluhu kutengua nafasi yake kupisha uchuguzi .
Sabaya ameieleza Mahakama kwamba baada ya kufikia katika duka hilo walimkosa Mmiliki wa duka na ndipo alipowasiliana na mamlaka iliyomtuma kazi hiyo, ambayo ilimjibu kwamba imeshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongozi na imeelekeza watu waliokutwa eneo la tukio wapelekwe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi ili kusaidia kupatikana Kwa mhusika wa duka aliyekuwa akitafutwa.
Anaeleza kuwa suala la yeye kupatiwa maelekezo na Mamlaka ya uteuzi ni Jambo la kawaida kwani miezi mitatu kabla ya siku ya tukio 9.2.2021 alipewa maelekezo ya kufanyakazi maalum na kubaini mtambo wa kutengeneza fedha bandia na kukamata fedha bandia sh,milioni 800 jijini Dar es salaam.
Sabaya anaeleza kuwa katika zoezi hilo alikuwa msimamizi mkuu ambapo Hata Gavana wa Fedha Prof Florian Luoga pamoja na aliye kuwa waziri wa Fedha hapa Nchini Dkt Philp Mpango ambaye kwasasa ndiye Makamu wa Rais wanalijua.
Sabaya amedai kuwa hajawahi kufikia katika duka la Shaahid Store na kupora kiasi cha sh, milioni 2,769,000 na kisha kumpiga human Jasim , Bakari Msangi, Salim hasani na Ally shabani na kuwatisha Kwa silaha na kwamba hamfahamu mshtakiwa mwenzake anayetajwa Kwa jina la Daniel Mbura na pia Silvester Nyegu hakuwa naye siku ya tukio.
Sabaya anaendelea kujitetea....
Jiwe simjui kwa kesi hii mporaji Ni Sabaya sio Jiwe nisiemjua Ni sawa na kusema Chadema chama Cha Magaidi wakati gaidi Ni Mbowe
Huu upuuzi wa eti rais hapangiwi ndiyo maana wananzengo wanapiga kelele za katiba mpya, hata rais kisheria hayuko juu ya sheria.Magufuli aliamini Sabaya ndio anaweza fanya kazi hiyo kwa ufanisi ,na Rais hapangiwi
Hivi huu utetezi waliwashirikisha mawakili kweli?Huwezi kutii amri haramu ya kiongozi yeyote hata kama ni rais.
Huyu ni mjinga pamoja na mawakili wake wote.
SAWA.Sabaya zigo lako Hilo uliwezaje kwenda kufanya military operation nje ya your judistriction? Hiyo Operation alitakiwa afanye Mama Mgwira au mkuu wa wilaya ya Arusha au polisi wilaya ya Arusha au mkoa etc etc but from Arusha.Raisi hawezi ishiwa operatives wa any mission Hana haja ya kutafuta mtu wa Hai kwenda Arusha!!!
Navoona Saa mbaya alitenda makosa na anajua hivyo kuwa hakuna namna anaweza kujitoa kwenye makosa moja kwa moja; Kwa sababu hiyo sasa anaona kilichobaki ni kuonesha kuwa, pamoja na kuwa ni kweli alitenda makosa lakin alitegemea wale waliomtuma wangemtetea badala yake wamemtekekeza ajijue mwenyewe na yeye sasa kaamua kama ni mbwai acha iwe mbwa tu; ni kama ana hoji "hivi mimi sabaya, katika mazingira ya utawala wa wakati ule, ningeliweza vip kukataa maelekezo (soma AMRI) ya Mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama wa nchi, na tena mkuu huyo ni Jiwe himself?!!!Huwezi kutii amri haramu ya kiongozi yeyote hata kama ni rais.
Huyu ni mjinga pamoja na mawakili wake wote.
Hata Yale Makonda alikua anafanya atakua alikua anatumwa na Magu.Kesi ujambazi wako unasingizia ulitumwa na magu, eti gavana na waziri anajua ujambazi wako, so what? Utetezi dhaifu sijawahi sikia. Wanajua kwa utaratibu upi? Shenzi kweli hili toto kumbe sabaya kichwani popompo kabisa. Alitumia ushikaji na marehemu vibaya, akawa anazunguka kupiga pesa. Kwa hiyo nchi ilikuwa ukiwa mshikaji wa Rais basi unafanya chochote kibaya bila kujali sheria na taratibu
Wewe ndio umechafua kabisa uzi kwa kububujikwa na mimatemate, angekuwepo jiwe unadhani hii kesi isingekuwepo.Kwahiyo kupiga simu polisi ndio unahitimisha hakufanya unyang'anyi? Je polisi unajuaje kama na wenyewe hawakua sehemu ya mpango au walipewa maagizo.Japo akili yako unaitumia tu kwenye kupanua mdomo na kutumbukiza kijiko cha chakula jaribu uiboost ikusaidie katika mambo menginehii kesi haina tofauti na ya Prof. Mahalu naye wakati alipo shitakiwa alidai alitumwa na aliye kuwa Rais wa awamu ya 3 Mkapa, kweli Mkapa walikuja na kumtetea Mahalau na Mahalu aliachiwa huru.
Sabaya hana makosa kama alikuwa anatekeleza maelekezo ya aliye mteua, naamini kama Magufuli angekuwa hai angemtetea Sabaya bila kigugumizi, lkn pia kama Mama Anna Mgwira ange kuwa hai ange mtetea Sabaya bila kigugumizi.
sijaona unyang'anyi uliotendwa!
mnyang'anyi angechukua receipts machine ya nn?!!
mnyang'anyi angepiga simu kituo cha polisi?!
huo ni unyang'anyi wa wapi?
Utajuaje kama aliamriwa..."wewe fanya rorote almradi utekereze kazi ninayokutuma"...Ana mashtaka ya kubaka, kujeruhi na kupora. Hayo ndio alitumwa?
Ndiyo sababu ya kuwa jeuri vile. Alijua hashikiki.Gavana ametajwa, Makamu ametajwa, Magu ametajwa
Hilo swali kwa sheria ipi" hakuna jibu hapo. Kumsave huyu kijana labda iwe amri toka juu.Haina ugumu wowote. Ameanza vibaya. Mkuu wa Wilaya na kazi maalum za kukamata kamata wahalifu wapi na wapi. Na amejichanganya zaidi kudai alikuwa pia akitekeleza mission hizo nje ya eneo lake la kazi. Atahitaji kuthihitisha kisheria kama hicho kikosi alichokuwa akikiongoza kiliundwa kweli, kiliundwaje na kwa sheria ipi.