Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya leo Ijumaa Agosti 13, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha amewataja Hayati John Magufuli, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na Gavana wa Benki Kuu kuwa walikuwa wanajua operesheni aliyokuwa akiifanya Arusha.

Chanzo: mwananchi_official
Muda Ni Mwalimu mzuri na msema kweli'

Ipo cku Siro atasema kesi ya ugaidi aliyopewa mboye Ni Maagizo kutoka juu!
 
Haina ugumu wowote. Ameanza vibaya. Mkuu wa Wilaya na kazi maalum za kukamata kamata wahalifu wapi na wapi. Na amejichanganya zaidi kudai alikuwa pia akitekeleza mission hizo nje ya eneo lake la kazi. Atahitaji kithihitisha kisheria kama hicho kikosi alichokuwa akikiongoza kiliundwa kweli, kiliundwaje na kea sheria ipi.
Hata OCD wa Hai na police ilifaa waunganishwe kwenye kesi ya hii ya kuvamia duka sabaya alitoa wapi silaha za kivita kufanyia uhalifu?.
 
Ole Sabaaya ameshapotoshwa na wanasheria wake,

1) Amri Kutoka Kwa Wakuu Wake (Order From Higher Personnel) sio Criminal Defence. Ni Heri hata angejitetea alikua amelewa kwasababu Intoxication inaweza kutumika kama Criminal Defence.
hii ipo katika defence! lakin alichofanya ni uhuni mtupu

maagizo kutoka juu yalitakiwa kuishia kuwakamata na kuwapeleka polisi kama kweli criminals
 
Mkuu wa wilaya ya Ya Hai anatumwa na Raisi akafanye operation wilaya isio yake ya Arusha? Raisi Hana operative wakuu wa wilaya ya Arusha au mkuu wa mkoa wa Arusha hidden operative wa kufanya hiyo Operation...
Si mlimtuma kwenda kumsambaratisha Mbowe
 
Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang’anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad...
watuletee CCTV ambayo haijapikwa na washahid waitambue tumalize mchezo
 
Sabaya ameona ngoja atumie mlango wa dharura ( Emergency exit) kujinasua. Jamaa anaakili sana. Kunakoendelea hana kesi . Hapo suluhisho ni Katiba mpya amasivyo hata mpango hatoweza kuitwa kutoa utetezi wake mahakamini kisa katiba na sheria zilizopo haziruhusu Raisi wala makamu wala spika wala Jaji mkuu kushitakiwa
 
Logically tu haiwezekani Rais wa nchi ajue Oparesheni fulani halafu Makamu wake nae asijue.

Naona sasa Ole Sabaya kaamua Kujilipua tu na kwamba liwalo na liwe.
Wasije mdunga sindano huko kisongo wasingizie corona, wasitufanye sisi wajinga, serikali ilijua fika alichokuwa anafanya Lengai acha awataje
 
Magufuli aliamini Sabaya ndio anaweza fanya kazi hiyo kwa ufanisi ,na Rais hapangiwi

Ndio maana tunasema Magu alikuwa rais muovu. Haya madai yetu ya katiba mpya, ni pamoja na kumdhibiti rais kuwa na madaraka yaliyopita mipaka. Kinga ya rais kutoshtakiwa ilitegemewa tutakuwa na marais waadilifu, lakini ukimuacha Nyerere kwa mbali, marais wengine wote hawajawahi kuwa waadilifu, na Magufuli ndio alikuwa muovu wa wazi.
 
Back
Top Bottom