Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kesi Hii tunakoelekea utasikia watuhumiwa walikuwa na pingu mikononi wameruka kwenye gari wakipeleka mahabusu na wamefafiki wote.Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya leo Ijumaa Agosti 13, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha amewataja Hayati John Magufuli, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na Gavana wa Benki Kuu kuwa walikuwa wanajua operesheni aliyokuwa akiifanya Arusha.
Sabaya amesema hayo wakati akitoa utetezi mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi Odira Amworo kuwa alichokuwa anakifanya Arusha Februari 9, 2021 haikuwa operesheni yake ya kwanza kuagizwa na hayati Rais Magufuli.
Akiongozwa na wakili anayemtetea Mosses Mahuna, wakati alipoanza kujitetea mahakamani hapo amesema kesi hiyo ni ya kutengeneza na yeye hajaiba wala kumtishia mtu yoyote kwa silaha.
Sabaya alisema siku ya tukio Februari 9, 2021 alipomaliza kuongoza kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Hai, alipokea simu ya Dk Magufuli aliyemwelekeza kazi ya kufanya katika mkoa wa Arusha ambapo pia alipaswa kuwapitia watu wengine wanne katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo watu hao walikuwa na maelekezo juu ya kazi hiyo wanayoenda kufanya.
"Hiyo haikuwa kazi ya kwanza kwa sababu miezi michache iliyopita tulipewa zoezi la kukamata mitambo inayotengeneza noti bandia na tulifanikiwa kukamata mitambo na fedha Sh 800 Milioni bandia eneo la Chanika wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam ,Gavana wa BoT anajua na aliyekuwa Waziri wa Fedha kwa wakati huo Dk Philip Mpango, Makamu wa Rais wa sasa pia anafahamu," alisema Sabaya.
Chanzo: Mwananchi
lazma achukue 15 kwenda mbeleHuyo dogo ni mshirikina sana.... mganga wake mmasai flani hivi!! Hiyo kesi itaisha kimiujiza labda lile lipete lake lipelekwe kwa baba paroko!
Eh no snitching around., sabAya is waaack!!!Hahaha umekuwa Riley "say no to snitching".
Wewe unaamini wako serious!!!!
Jaji wa nini?mmeanza kurudi tena jukwaani! jiulizeni kwa nini jaji katoka mkoa mwingine! kwa nini PCCB ina yule aliyewekwa hapo mtajua
Umesikia utetezi wake? mtu kama amekiri mwenyewe unategemea nini?Chadema wana chuki binafsi na huyu bwana mdogo!
KutekaKakiri kuhusika na nn?
ataanzwa muda siyo mrefuAsubiri kupigwa mande, sasa hivi hajawa mfungwa, akiwa mfungwa ndipo atakapoona anapigwa mande
Je, wana CHADEMA Wenzangu hapa Mitandaoni JamiiForums kwa jinsi huyu aliyekuwa Adui yetu Ole Sabaya sasa anavyoupiga mwingi Kiutetezi kwa Kuwataja Hayati Rais Dkt. Magufuli, Makamu wa Rais Dkt. Mpango na Gavana wa BOT tutabadilika na kuanza Kumpenda na Kumpamba Mitandaoni au tutaendelea tu Kumkazia na watajuana wenyewe kwa wenyewe?
Kusema alikuwa kwenye " kazi maalumu " ndio kukiri?!Umesikia utetezi wake? mtu kama amekiri mwenyewe unategemea nini?
Eti Jiwe alinituma!!!😃😃😃😃😃😎😎😎😎
Fyuuuuu
Kazi maalum kuvamia watu?Kusema alikuwa kwenye " kazi maalumu " ndio kukiri?!
Aiseee ni kweliDuh!! Mungu anamuona lakini!
Amejitetea kiume sana
Makamu wa Rais Dr Mpango na DC mstaafu Dr Kihongosi watakuwa mashahidi wake muhimu kama katiba inaruhusu.
Rais mstaafu Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kumtetea Prof Mahalu pale Kisutu!
Unawajua polis tu u umeambiwa Kaz maalum maana yake na polis walijuimukaMajukumu ya polisi ni yapi!.na majukumu ya mkuu wa wilaya ni yapi!
Hapa kimeumana tunataka katiba mpya