Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya leo Ijumaa Agosti 13, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha amewataja Hayati John Magufuli, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na Gavana wa Benki Kuu kuwa walikuwa wanajua operesheni aliyokuwa akiifanya Arusha.

Sabaya amesema hayo wakati akitoa utetezi mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi Odira Amworo kuwa alichokuwa anakifanya Arusha Februari 9, 2021 haikuwa operesheni yake ya kwanza kuagizwa na hayati Rais Magufuli.

Akiongozwa na wakili anayemtetea Mosses Mahuna, wakati alipoanza kujitetea mahakamani hapo amesema kesi hiyo ni ya kutengeneza na yeye hajaiba wala kumtishia mtu yoyote kwa silaha.

Sabaya alisema siku ya tukio Februari 9, 2021 alipomaliza kuongoza kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Hai, alipokea simu ya Dk Magufuli aliyemwelekeza kazi ya kufanya katika mkoa wa Arusha ambapo pia alipaswa kuwapitia watu wengine wanne katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo watu hao walikuwa na maelekezo juu ya kazi hiyo wanayoenda kufanya.

"Hiyo haikuwa kazi ya kwanza kwa sababu miezi michache iliyopita tulipewa zoezi la kukamata mitambo inayotengeneza noti bandia na tulifanikiwa kukamata mitambo na fedha Sh 800 Milioni bandia eneo la Chanika wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam ,Gavana wa BoT anajua na aliyekuwa Waziri wa Fedha kwa wakati huo Dk Philip Mpango, Makamu wa Rais wa sasa pia anafahamu," alisema Sabaya.

Chanzo: Mwananchi
Kesi Hii tunakoelekea utasikia watuhumiwa walikuwa na pingu mikononi wameruka kwenye gari wakipeleka mahabusu na wamefafiki wote.
 
Wewe unaamini wako serious!!!!

..mashitaka ni mabaya / serious.

..na sidhani kama Sabaya ameyapangua hayo mashtaka.

..kusema kwamba alitumwa na Raisi siyo utetezi wa kutosha.

..Mramba na Yona walitoa utetezi wa aina hiyohiyo lakini walifungwa.

..Pia Raisi anaweza kukutuma lakini ukitekeleza hovyo-hovyo anaweza kukushtaki na hatimaye ukafungwa.
 
Je, wana CHADEMA Wenzangu hapa Mitandaoni JamiiForums kwa jinsi huyu aliyekuwa Adui yetu Ole Sabaya sasa anavyoupiga mwingi Kiutetezi kwa Kuwataja Hayati Rais Dkt. Magufuli, Makamu wa Rais Dkt. Mpango na Gavana wa BOT tutabadilika na kuanza Kumpenda na Kumpamba Mitandaoni au tutaendelea tu Kumkazia na watajuana wenyewe kwa wenyewe?

Tumpende mtu muovu? Alichokifanya ni kudhibitisha yale madai yetu kuwa Magufuli alikuwa rais muovu, na aliiendesha nchi hii kwa maagizo ya uovu. Ushahidi huu unazidi kuyapa nguvu madai yetu ya katiba mpya, huku kipengele cha madaraka ya urais yakipunguzwa, ikiwemo rais kushitakiwa akiwa madarakani, au akiwa ametoka.
 
Eti Jiwe alinituma!!!😃😃😃😃😃😎😎😎😎
Fyuuuuu
msiba.png

Na huyu je? Kweli mwendakuzimu alikuwa dhalimu!
Baada ya haya matamshi, mahakama kimyaaa, Wizara ya sheria kimyaaa na Jaji Mkuu kimyaaaa!​
 
Kusema alitumwa ndio ushahidi?waliomtuma walimwambia afanye ujambazi?,na kama aliambiwa afanye ujambazi je ilikuwa amri halali?

Ngoja waitwe hao waliomtuma kama wapo uone kama watakiri walimwambia afanye jinai
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] aisee anamchafua marehemu
 
Back
Top Bottom