Toka Hiyo kesi inaanza nilijua lazima Sabaya atatoa utetezi huu, maana ni kweli kuna mambo mengi kinyume na sheria Magu alikuwa anawaagiza hawa waovu wenzake. Na Sabaya anataja hayo maagizo ya kupewa na rais, maana anajua kuna wengi sana walikuwa wakiagizwa na Magu kufanya kinyume na sheria, na walikubali maana walikuwa wanafaidika na huo uovu, wao binafsi, na pia walikuwa wanalinda ajira zao kwa kumnufaisha huyo mtu muovu.
Mfano ule uporaji wa fedha za kwenye mabureau de change, shambulizi la Lisu huko kwenye makazi ya wabunge Dodoma, huku polisi wakiwa wameondolewa eneo la tukio. Hakuna kiongozi mwingine yoyote anayeweza kutoa amri zile zaidi ya rais. Hata haya mashitaka ya ugaidi dhidi ya Mbowe, ni maagizo ya rais Samia ili katiba mpya isidaiwe. Tunaposema tunataka katiba mpya, sehemu mojawapo ni haya madaraka ya rais kuendesha mambo ya uovu, huku katiba ikimpa kinga ya kutoshtakiwa.