Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Mkuu wa wilaya ya Ya Hai anatumwa na Raisi akafanye operation wilaya isio yake ya Arusha? Raisi Hana operative wakuu wa wilaya ya Arusha au mkuu wa mkoa wa Arusha hidden operative wa kufanya hiyo Operation?

Sabaya zigo lako Hilo uliwezaje kwenda kufanya military operation nje ya your judistriction? Hiyo Operation alitakiwa afanye Mama Mgwira au mkuu wa wilaya ya Arusha au polisi wilaya ya Arusha au mkoa etc etc but from Arusha.Raisi hawezi ishiwa operatives wa any mission Hana haja ya kutafuta mtu wa Hai kwenda Arusha!!!

Sabaya jambazi wewe kesi Hilo lako usisingizie Marehemu wewe hukujua kuwa Arusha sio eneo lako la judistriction? Kuwa wewe ni
mkuu wa wilaya ya hai? Ungekuwa huna area ya uteuzi utetezi wako unge matter. Lakini mmmmmm .una kesi ya kujibu
Kwenye system ilo swala la kawaida sana .Rais anamtuma mtu anaeona anaweza kuitekeleza kazi Ile kwa ufanisi
 
Kumbuka utetezi wa Luoga na Philip Mpango ambao anautaja Sabaya ni kuhusu yeye kushiriki kusaka na kukamata mtambo wa kuchapisha pesa bandai baada ya kuwakamata wahalifu waliokua wakiuza pesa bandia huko Hai.

Amewataja hao kina Luoga na Mpango akiamini anatengeneza uhalali kuwa yeye ni kawaida kufanya kazi za kipolisi nje ya wilaya yake 🤣

Haihusiani na hii ya kuvamia duka la muarabu, Sabaya anawachanganyia maneno.
Kwanini uongozi wote wa mkoa wa Arusha ulimuacha DC Ole sabaya afanye kazi hiyo ndani ya mkoa wao?
 
Kwanini alikuwa hakamatwi?
Anakamatwa vipi wakati alikua akifika popote anajata jina la Rais na anajulikana ni DC, Rudi kwenye kesi kasome ushahidi wa Askari Gwakisa aliyewahoji hao waliokamatwa na Sabaya, anasema wazi kabisa kuwa Sabaya alikua amefanya makosa kwa hao watuhumiwa feki aliowatesa ila hawakuwa na cha kufanya kwa mteule wa Rais aliyewaambia kuwa ametumwa na Rais na mwisho wa siku Askari Gwakisa aliona kesi haina mashiko akaifutilia mbali na Sabaya alishiriki kumuomba mmoja ya wateswaji akubali kesi ifutwe.
 
Anakamatwa vipi wakati alikua akifika popote anajata jina la Rais na anajulikana ni DC, Rudi kwenye kesi kasome ushahidi wa Askari Gwakisa aliyewahoji hao waliokamatwa na Sabaya, anasema wazi kabisa kuwa Sabaya alikua amefanya makosa kwa hao watuhumiwa feki aliowatesa ila hawakuwa na cha kufanya kwa mteule wa Rais aliyewaambia kuwa ametumwa na Rais na mwisho wa siku Askari Gwakisa aliona kesi haina mashiko akaifutilia mbali na Sabaya alishiriki kumuomba mmoja ya wateswaji akubali kesi ifutwe.
Kwanini Gwakisa hakuripoti kwa RPC kwa ushauri zaidi?
 
Shida huyo jamaa Lengai Sabaya hiyo kesi akishindwa kinachofuata sio kifungo bali lipa pesa inayoendana na kifungo chake kazi kwisha ingawa wengi wanapenda akanyee debe kwa ninavyojua mm hakim atapata maelekezo kutoa option ktk kesi hii! Ilaa angekuwa wa upande wa pili hapo option isingetolewa!
Ungemjua hakimu ameletwa maalum kutoka Geita kwa hio kazi maalum,usingebonga Sana.
 
Bwashee tofautisha Kazi maalumu na Ujambazi!

Usipanic.......hii kesi tangu mwanzo ilionyesha Sabaya anachomoka!
Mkuu kazi maalum serikali haikupi defense, you're on your own. Yaani mahakama imemkuta na kesi ya kujibu, halafu anajibu ujinga hivi.

Anyways tulipowaambia hawezi kuendelea na uDC wakati wa Mama, mlitubeza hapa. Ngoja tusubiri hukumu
 
hii kesi haina tofauti na ya Prof. Mahalu naye wakati alipo shitakiwa alidai alitumwa na aliye kuwa Rais wa awamu ya 3 Mkapa, kweli Mkapa walikuja na kumtetea Mahalau na Mahalu aliachiwa huru.
Sabaya hana makosa kama alikuwa anatekeleza maelekezo ya aliye mteua, naamini kama Magufuli angekuwa hai angemtetea Sabaya bila kigugumizi, lkn pia kama Mama Anna Mgwira ange kuwa hai ange mtetea Sabaya bila kigugumizi.
sijaona unyang'anyi uliotendwa!
mnyang'anyi angechukua receipts machine ya nn?!!
mnyang'anyi angepiga simu kituo cha polisi?!
huo ni unyang'anyi wa wapi?!
Haya wale waliokatwa masikio sabaya alitumwa nasikia
 
Kuweka kumbukumbu sawa Marehemu Mzee Pombe hakumpigia simu Sabaya na kumuambia eti aende Dar kufanya kazi maalum ya kusaka mtambo wa kuchapisha pesa feki, ni polisi wa Hai walikamata pesa feki hapo Hai wakamtaarifu Sabaya wakawabana watuhumiwa na kusafiri nao kwenda Dar mpaka wakaonyesha mtambo wao wa kuchapisha pesa bandia.

In short Sabaya jambo lolote linalohusu PESA liwe la halali au haramu ilikua lazima atahakikisha anashiriki kwenda phisical eneo husika hata kama sio eneo lake la kazi au hata kama ni jukumu la taasisi nyingine.
Jambazi kabisa huyu. Ingekuwa kwetu china wala kulikuwa hamna kesi,tayari angekuwa amechapwa risasi hadharani. Naiomba sana mahakama ya Arusha,hapo kama ni swala la haki ya kimaamuzi ya mahakama,huyu haki yake mvua 30
 
Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad.

Akiongozwa na wakili Mosses Mahuna wakati akitoa utetezi wake mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Sabaya alidai yeye bado ni mtumishi wa Serikali ila alisikia tangazo la kusimamishwa kazi kutoka Kwa Rais Samia Suluhu.

Alidai kuwa siku ya tukio Februari 9 mwaka huu majira ya saa 9 kasoro alasiri alipigiwa simu na Mamlaka iliyomteua na kumpatia maelekezo ya kwenda kufanya kazi maalumu Arusha na kumtaka aongozane na watu wanne waliokuwa wakimsubiri uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro KIA.

Sabaya alidai kuwa walipofika Arusha wakiwa na wale watu wanne ambao ndio wenye taarifa zote walielekea eneo husika waliokuwa wameelekezwa na Mamlaka husika katika eneo la duka la Shaahid store lililopo mtaa wa Soko kuu jijini Arusha.

Akihojiwa na Wakili Mahuna kuhusu kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya tarehe 9.2.2021 ,Sabaya alidai alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani kilimanjaro na aliteuliwa na Rais Hayati Dkt John Pombe Magufuli tarehe 29.7.2018.

Lengai Ole Sabaya anaeleza mahakama kuwa alitumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 2 na miezi 10 na alikoma kuhudumu wadhifa huo tarehe 13.5.2021 baada ya Rais Samia Suluhu kutengua nafasi yake kupisha uchuguzi .

Sabaya ameieleza Mahakama kwamba baada ya kufikia katika duka hilo walimkosa Mmiliki wa duka na ndipo alipowasiliana na mamlaka iliyomtuma kazi hiyo, ambayo ilimjibu kwamba imeshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongozi na imeelekeza watu waliokutwa eneo la tukio wapelekwe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi ili kusaidia kupatikana Kwa mhusika wa duka aliyekuwa akitafutwa.

Anaeleza kuwa suala la yeye kupatiwa maelekezo na Mamlaka ya uteuzi ni Jambo la kawaida kwani miezi mitatu kabla ya siku ya tukio 9.2.2021 alipewa maelekezo ya kufanyakazi maalum na kubaini mtambo wa kutengeneza fedha bandia na kukamata fedha bandia sh,milioni 800 jijini Dar es salaam.

Sabaya anaeleza kuwa katika zoezi hilo alikuwa msimamizi mkuu ambapo Hata Gavana wa Fedha Prof Florian Luoga pamoja na aliye kuwa waziri wa Fedha hapa Nchini Dkt Philp Mpango ambaye kwasasa ndiye Makamu wa Rais wanalijua.

Sabaya amedai kuwa hajawahi kufikia katika duka la Shaahid Store na kupora kiasi cha sh, milioni 2,769,000 na kisha kumpiga human Jasim , Bakari Msangi, Salim hasani na Ally shabani na kuwatisha Kwa silaha na kwamba hamfahamu mshtakiwa mwenzake anayetajwa Kwa jina la Daniel Mbura na pia Silvester Nyegu hakuwa naye siku ya tukio.

Sabaya anaendelea kujitetea....

Kwani Arusha hakua na mkuu wa Wilaya mpaka atoke yeye Hai aende kufanya kazi Wilaya Nyingne. Kihongozi alikuwa wap? Mkuu wa mkoa wa Arusha alikua wapi
 
Mkuu kazi maalum serikali haikupi defense, you're on your own. Yaani mahakama imemkuta na kesi ya kujibu, halafu anajibu ujinga hivi.

Anyways tulipowaambia hawezi kuendelea na uDC wakati wa Mama, mlitubeza hapa. Ngoja tusubiri hukumu
Wewe unaamini amejibu ujinga?
 
Ukipitia hukumu ya Zombe ( RPC mstaafu) kwenye ile kesi ya wale jamaa wa madini utagundua Sabaya ana nafasi kubwa ya kuachiwa huru!
Hiyo kesi ya zombe Marehemu walikuwa hawawez kujitetea Ni rahisi kutoka.

Kesi ya Sabaya wahanga wote wako hai, apambane.
 
Ole Sabaaya ameshapotoshwa na wanasheria wake, kifungo kinam nyemelea huyu jamaa;

1) Amri Kutoka Kwa Wakuu Wake (Order From Higher Personnel) sio utetezi wa jinai (Sio Criminal Defence). Ni Heri hata angejitetea alikua amelewa kupita kiasi kwasababu Ulevi (Intoxication) inaweza kutumika kama Criminal Defence.

Hakuna defence katika jinai ya Kutimiza Amri Ya Kiongozi Wa Juu (Order From Higher Personnel). Hii haipo kwenye Penal Code CAP 16 na hata kwa wanajeshi haipo kwenye Marshall Codes & Laws.

Ref: Nurenmberg Trials and Nuremberg Codes.

Wanajeshi wa Nazi walitumia utetezi huo kujitoa katika hatia ya makosa ya jinai waliotenda dhidi ya binaadamu, walisema wao walitenda hayo mauwaji ila kwa kufuata na kutii amri za wakubwa zao jeshini. Ila mahakama ya kijeshi ya Nurenmberg ilikataa utetezi huo kwa hoja moja kuu "UNAPOPEWA ORDER NA MKUU WAKO YA KUFANYA JAMBO LINALOKWENDA KINYUME NA SHERIA AU HAKI ZA BINAADAMU, UNA WAJIBU WA KUKATAA KUTII ORDER HIO".

2) Ushahidi wa kumtaja mtu kwamba amekupa maagizo fulani kisheria unahitaji "CORROBORATION" ya ushahidi wa ziada kutoka kwa huyo mtu alietajwa. Magufuli hawezi kupatikana kwaajili ya kutoa ushahidi wa ziada ku-support na ku-confirm ushahidi wa Ole Sabaaya.
Labda busara za majaji tuu kwa kuzingatia mazingira ya Tzn na utawala uliokuwepo hapo awali
 
Back
Top Bottom