Huu ndiyo uzuri wa waTZ, hasa wapinzani, wape jambo moja tu linalomchafua mtu wanayemchukia wa CCM, then wanasahau mengine yote!! Kwa sasa masuala ya gari la magereza kushindwa kumpeleka Ustaadhi mahakamani, mabalozi mahakamani na Taasisi kubwa kuingilia mahakama yatasahaulika kwa muda!! Jumatatu watu watakuwa seat ya mbele, sikio likiwa limetegwa Arusha kusikiliza Sabaya atamtaja nani tena. Wakitaka wawatoe kwenye reli zaidi awataje Samia na Majaliwa, hapo Bwana ustaadhi atasahaulika hadi October!! Na vyombo vyetu vya habari kwao sasa hii ndiyo itakuwa habari ya kuuza.