tutamkumbukamagu
JF-Expert Member
- Jul 3, 2021
- 317
- 270
unamlaumu sabaya au mto comment?......amejitetea kiume?
Subiri siku atakapopelekwa kupakatwa kwa muda wa miaka 7 ndo akili itakukaa sawa.....
sio kila mtu anamchukia sabaya ndugu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
unamlaumu sabaya au mto comment?......amejitetea kiume?
Subiri siku atakapopelekwa kupakatwa kwa muda wa miaka 7 ndo akili itakukaa sawa.....
kabla haujaandika yote hayaAipate wapi hiyo proof?!
Hata kama alitumwa, usitarajie eti alipata official letter kumtaka akafanye huo uhalifu!! Hiyo official letter ingekuwa ndo ushahidi!!
Hapo itakuwa alitumwa kwa kupigiwa simu tu!!!
Lakini hata kama angekuwa na hiyo barua, bado alitakiwa kujua kama maagizo aliyopewa ni halali kisheria, au la!! Na iwe anajua au hapana bado haiwezi kusaidia kwa sababu kutojua sheria haihalalishi kuvunja sheria!!
Hujawahi kufanya kazi hata kwenye taasisi ndogo? Hakunaga watu wanatumwa kazi maalum kutoka DSM kwenda Mwanza, Mwanza kwenda Mbeya, Mbeya kwenda Moro, Moro Kwenda Arusha, Dodoma kwenda Babati? Huko kote kunawaga hakuna wanaojua hiyo kazi?Mkuu wa wilaya ya Ya Hai anatumwa na Raisi akafanye operation wilaya isio yake ya Arusha? Raisi Hana operative wakuu wa wilaya ya Arusha au mkuu wa mkoa wa Arusha hidden operative wa kufanya hiyo Operation?
Sabaya zigo lako Hilo uliwezaje kwenda kufanya military operation nje ya your judistriction? Hiyo Operation alitakiwa afanye Mama Mgwira au mkuu wa wilaya ya Arusha au polisi wilaya ya Arusha au mkoa etc etc but from Arusha.Raisi hawezi ishiwa operatives wa any mission Hana haja ya kutafuta mtu wa Hai kwenda Arusha!!!
Sabaya jambazi wewe kesi Hilo lako usisingizie Marehemu wewe hukujua kuwa Arusha sio eneo lako la judistriction? Kuwa wewe ni
mkuu wa wilaya ya hai? Ungekuwa huna area ya uteuzi utetezi wako unge matter. Lakini mmmmmm .una kesi ya kujibu
tatizo wewe ni layman kweliYawezekana Sabaya hana qualified advocate au yuko kwenye extreme stage ya desparation. Hata mimi lay person siwezi kumfanyia examination client wangu kwa swali kama hilo.
Ni weitten documents tu zenye sahihi rasmi za kutoka kwa Magufuli zinazomuamuru kwenda kufanya hiyo operesheni ndizo zinaweza kumuokoa. Otherwise hiyo siyo defence bali maongezi ya kijiweni tu.
Tangu umezeshwe kitu inaitwa katiba wewe kila kitu katiba! Katiba iliyopo umewahi kuisoma?Vyote vinaendana, wewe huoni ajabu mwenyekiti wa chama kinachounda serikali, na ambaye ndiye Rais, anatajwa kuwaagiza wasaidizi wake wakawafanyie ujambazi wananchi waliompigia kura?!! Aibu tupu.
Unafikiri kama si katiba mbovu haya yangetokea? Na ujue hapo saa mbaya kafikishwa mahakaman ni kwa kutaka mama, mama asingetaka saa mbaya asingefikishwa popote...yote hayo ni katiba mbovu
Moses Mahuna ni incompetent au ni Afisa KipenyoHumjui Moses Mahuna?
Mimi ni layman kweli kwa vile siyo mwanasheria. Ila wewe ni la 7Btatizo wewe ni layman kweli
unachanganya chuki zako kwa sabaya na sheria
Mpango hajashtakiwa. Kwanini tunakuwa wadhaifu kwenyw kuconsume taarifa kiasi hiki? Mpango kufahamu juu ya haimaanishi kushtakiwa. Na operation haimaanishi kufanya ujambazi au kuua ai hata kupiga. Lakini Sabaya amehalalisha uwepo wa operation aliohusika jijini Arusha. Ametoa na mfano wa operation aliofanya Temeke.Hapo Mpango kashatiwa doa la kugombea urais dah.Au hii movie imetengenezwa
Jihusishe na mada ilioko mezani.Moses Mahuna ni incompetent au ni Afisa Kipenyo
Someni utetezi. Acheni conclusions ambazo hazina maana. Hii nchi ina upungufu wa intelectuals sana. Sabaya ameelezea uhalali wa operation. Matendo ya kwenye operation yanabaki kuwa ya kwake na wale alioambatana nao na amekana kufanya uporaji wa kutumia silaha unaotajwa kwenye mashtaka.Sabaya Magufuli hayupo juu ya Sheria hapo ni sawa na kukiri kosa jiandae tu uchomoki
Mpango hajashtakiwa. Kwanini tunakuwa wadhaifu kwenyw kuconsume taarifa kiasi hiki? Mpango kufahamu juu ya haimaanishi kushtakiwa. Na operation haimaanishi kufanya ujambazi au kuua ai hata kupiga. Lakini Sabaya amehalalisha uwepo wa operation aliohusika jijini Arusha. Ametoa na mfano wa operation aliofanya Temeke.
Wakimtupa baharini sio mbaya,Kwa hiyo kipi kikifanyika Ni Bora kwa mahakama wamfunge au wamwachie
Wapi nimeandika Mpango kashitakiwa?umepanick bro bila shaka una udugu na mpango ila urais hampati.Mpango hajashtakiwa. Kwanini tunakuwa wadhaifu kwenyw kuconsume taarifa kiasi hiki? Mpango kufahamu juu ya haimaanishi kushtakiwa. Na operation haimaanishi kufanya ujambazi au kuua ai hata kupiga. Lakini Sabaya amehalalisha uwepo wa operation aliohusika jijini Arusha. Ametoa na mfano wa operation aliofanya Temeke.
Kwa nini nisiisome na hata kama ningekuwa sijaisoma hiyo haiondoi umuhimu wa kuondoa mapungufu yaliyopo. Kamwe Hatuwezi kuendelea kuwa na katiba inamruhusu mtu mmoja kuwafanyie wenzaye atakavyo hata kama ni kuwakata masikio bila kuchukuliwa hatua..huo ni utumwa na ukatili uliopitiliza. Ni lazima tuwe na katiba inayolinda haki na maslahi ya kila mtanzania na kila kundi katika jamii ya watanzania wakiwemo ccm. Kama ccm itaendelea kutawala tunataka wapate madaraka kwa haki si ghilba na wakishayapata waongoze nchi na wananchi kwa haki na kuwa mujibu wa sheria. Hakuna mtu wa kufanywa mtumwa na dhalili hapa kwa maslah ya wachache, karne ya 21 hii.Tangu umezeshwe kitu inaitwa katiba wewe kila kitu katiba! Katiba iliyopo umewahi kuisoma?
Tulishajua akina Mpango, Luoga, Majaliwa na huyo Samia wote si wakweli na ni wahusika wakuu katika kuteka, kuua na kunyang'anya watu mali zao. Hata wakisema hawahusiki ni uongo, wanajua wazi alichokuwa akifanya Sabaya. Shame on them.Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad.
Akiongozwa na wakili Mosses Mahuna wakati akitoa utetezi wake mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Sabaya alidai yeye bado ni mtumishi wa Serikali ila alisikia tangazo la kusimamishwa kazi kutoka Kwa Rais Samia Suluhu.
Alidai kuwa siku ya tukio Februari 9 mwaka huu majira ya saa 9 kasoro alasiri alipigiwa simu na Mamlaka iliyomteua na kumpatia maelekezo ya kwenda kufanya kazi maalumu Arusha na kumtaka aongozane na watu wanne waliokuwa wakimsubiri uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro KIA.
Sabaya alidai kuwa walipofika Arusha wakiwa na wale watu wanne ambao ndio wenye taarifa zote walielekea eneo husika waliokuwa wameelekezwa na Mamlaka husika katika eneo la duka la Shaahid store lililopo mtaa wa Soko kuu jijini Arusha.
Akihojiwa na Wakili Mahuna kuhusu kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya tarehe 9.2.2021 ,Sabaya alidai alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani kilimanjaro na aliteuliwa na Rais Hayati Dkt John Pombe Magufuli tarehe 29.7.2018.
Lengai Ole Sabaya anaeleza mahakama kuwa alitumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 2 na miezi 10 na alikoma kuhudumu wadhifa huo tarehe 13.5.2021 baada ya Rais Samia Suluhu kutengua nafasi yake kupisha uchuguzi .
Sabaya ameieleza Mahakama kwamba baada ya kufikia katika duka hilo walimkosa Mmiliki wa duka na ndipo alipowasiliana na mamlaka iliyomtuma kazi hiyo, ambayo ilimjibu kwamba imeshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongozi na imeelekeza watu waliokutwa eneo la tukio wapelekwe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi ili kusaidia kupatikana Kwa mhusika wa duka aliyekuwa akitafutwa.
Anaeleza kuwa suala la yeye kupatiwa maelekezo na Mamlaka ya uteuzi ni Jambo la kawaida kwani miezi mitatu kabla ya siku ya tukio 9.2.2021 alipewa maelekezo ya kufanyakazi maalum na kubaini mtambo wa kutengeneza fedha bandia na kukamata fedha bandia sh,milioni 800 jijini Dar es salaam.
Sabaya anaeleza kuwa katika zoezi hilo alikuwa msimamizi mkuu ambapo Hata Gavana wa Fedha Prof Florian Luoga pamoja na aliye kuwa waziri wa Fedha hapa Nchini Dkt Philp Mpango ambaye kwasasa ndiye Makamu wa Rais wanalijua.
Sabaya amedai kuwa hajawahi kufikia katika duka la Shaahid Store na kupora kiasi cha sh, milioni 2,769,000 na kisha kumpiga human Jasim , Bakari Msangi, Salim hasani na Ally shabani na kuwatisha Kwa silaha na kwamba hamfahamu mshtakiwa mwenzake anayetajwa Kwa jina la Daniel Mbura na pia Silvester Nyegu hakuwa naye siku ya tukio.
Sabaya anaendelea kujitetea....
So kwani operation tza huwa anafanya yeye pekee mbona wengi tu ufanya operation na awafanyi uhalifu.Someni utetezi. Acheni conclusions ambazo hazina maana. Hii nchi ina upungufu wa intelectuals sana. Sabaya ameelezea uhalali wa operation. Matendo ya kwenye operation yanabaki kuwa ya kwake na wale alioambatana nao na amekana kufanya uporaji wa kutumia silaha unaotajwa kwenye mashtaka.
Mijadala ijadiliwe kwa akili ili ukweli ujitenge na uongo.