Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #101
Kama umepata kazi ya upishi, inapita miezi na hata miaka kadhaa hujapika chakula chochote na bado unapata mshahara, inabidi ujiulize kama bado unastahili hiyo nafasi. Ngereja anastahili kuwajibika yeye mwenyewe kwa kushindwa kufikia matazamio ya nafasi aliyopewa.
Kutangaza hali ya hatari ni prerogative ya Rais. Halazimishwi na yeyote, na hashauriwi na yeyote. Bunge kama wawakilishi wa watu wanaweza kutoa tamko la kumtaka Rais kufanya hivyo. Rais akitangaza hali ya hatari anaweza hata kumteua Waziri wa Nishati wakati wa Dharura na kumwacha Ngeleja ashughulikie mambo mengine.
Watu tuna kumbukumbu fupi sana na ukweli huu umejidhihirisha hivi sasa kwenye haya matatizo ya umeme. Waziri Ngeleja anaoneka ndiye kama vile amesababisha matatizo yote haya wakati ukweli wa mambo umeme wa uhakika umekuwa tatizo sugu Tanzania.
Sasa iweje Ngeleja leo abebeshwe msalaba wa lawama na shutuma wakati mawaziri wa nishati na serikali zilizopita zimemrithisha tatizo? Hiyo si haki hata kidogo. Jaribuni tu kurudi nyuma miaka 20 iliyopita muone ni kina nani waliweza kupata fursa ya kuongoza wizara hiyo na walifanya nini kuhakikisha tatizo linakuwa historia.
I cut him some slack!!
Bw Mwanakijiji,
Japo ninaamini ni mfuatiliaji mzuri wa masuala yanayohusu hii nchi kuna kitu kimoja nataka kukufahamisha, japokuwa huyu Ngeleja amekuta hayo matatizo wizara ya Madini na nishati ukijumuisha na Tanesco; huyu bwana hawezi kukwepa fagio la chuma! sababu kubwa ni ameshindwa kuja na jawabu la kuondoa hali hiyo na zaidi ya hilo matatizo tuliyo nayo sasa yamesababishwa (kwa kiasi kikubwa) na uzembe (negligence) yaani kuna mitambo miwili imekosa mafuta mmoja wa IPTL na mwingine ni Symbion (tunavyoongea sasa)!
Gamba la Nyoka... unafikiri Rais anajua uzito wa tatizo la upungufu wa nishati au anahitaji kupewa ushauri na watu wengine juu ya uzito huo?
Unajua tukianza kukimbilia collective responsibilities tutaanza kuondoa dhana nzima ya uwajibikaji tusisahau wizara ni organ yenye sub-organs (departments et al) zenye systematical hirearchical divisions of responsibilities zenye specific individuals that oversee the organ smooth functioning! Sasa unapoanza mambo ya sera ina maana unaanza kuongelea the whole system that is party+government (chama Magamba (NEC) + serikali (including the whole ministries) + bunge)! Sasa nikuulize kwanini Magufuli under his ministry of Works awe accountable na kukosekana umeme? Tuache cheap politics na ku-victimize kila mtu kwa uzembe wa watu waliokuwa costitutional bestowed power ila waka-misuse!Nani anayetengeneza sera ya Nishati nchini? Kuna ubaya gani kwa Rais kutangaza hali ya dharura hata kesho na kutumia madarka aliyonayo kutatua tatizo la umeme?
Sera ya nishati 1992,ililetwa chini ya Jakaya Mrisho Kikwete,ikafanyiwa marekebisho chini ya Yona nadhani.Juzijuzi nilisikia kwamba wawekezaji hawaifagilii tanzania kwenye nishati kwa sababu ya masharti magumu,wengine wakasema bei ya umeme hairidhishi.Nani anayetengeneza sera ya Nishati nchini? Kuna ubaya gani kwa Rais kutangaza hali ya dharura hata kesho na kutumia madarka aliyonayo kutatua tatizo la umeme?
Mwanakijiji unaongea kana kwamba Rais wa Tanzania (kama taasisi) ni mnyonge asiyeweza kuagiza umeme wa upepo utengenezwe kula Singida na pale kwetu Makambako; wa maji utengenezwe kule kwetu milimani Upare na hapo kwenye Stiegler's Gorge. Au anaogopa Wanaharakati wa Mazingira waliombana kwenye suala la barabaraba ya Serengeti? Hivi kweli kabisa Sheria zetu za kusimika madaraka katika Dola ndio chanzo cha kuwa na taasisi dhaifu ya Urais hivyo kupelekea hitaji la kutangaza hali ya hatari? Basi na atangaze na hali ya dharura kuhusu njaa. Na kuhusu elimu. Pia na kuhusu vifo vya wajawazito mahospitalini. Kwa ujumla atangaze Marshal Law kisha atangaze Marshal Law kisha nchi iendeshwe ki-benovelent dictatorship; kulala saa 4 usiku hakuna kutembea giza likishaingia, amri (decree) ndio ziwe sheria za nchi, mijadala ya kidemokrasia ikome mara moja, lengo liwe moja tu: kuitumikia dola tuendelee!
Una ushahidi gani kuwa Rais wa Tanzania, kwa madaraka aliyonayo leo hii angeweza "kuagiza umeme wa upepo utengenezwe kula Singida na pale kwetu Makambako; wa maji utengenezwe kule kwetu milimani Upare na hapo kwenye Stiegler's Gorge."? Je, hii sii ni tayari sawa na mfano wa "nchi iendeshwe ki-benovelent dictatorship"? Kwa hiyo kutakuwa na haja gani basi ya Rais kuchukua extra measures za kutangaza "Marshall law" wakati tayari kikatiba yuko empowered with requisite Dictatorial powers?
Kwani anatumia madaraka gani anapoenda kuwaalika wawekezaji huko Sauzi na kwingineko?
Hivi kama nchi ikiingia Vitani mngetaka Rais aoneshe uongozi kwa kuchukua madaraka aliyonayo kisheria. Ninavyowasikiliza ni kana kwamba Idi Amin alipovamia Kagera Nyerere alitakiwa aende kukutana naye kumbeleza aondoe majeshi yake au aamue kumwachilia tu. Sijui kama Kikwete angekuwa Rais wakati ule tungefanya nini.
Ndio maana naamini aidha hii hali ya dharura siyo mbaya jinsi ambavyo tunaaminishwa na yawezekana haina athari kubwa kwa uchumi wetu na maisha yetu kulinganisha na Vita ya Uganda. Maana ya Vita ya Uganda iligusa sehemu ndogo ya nchi, lakini nchi nzima ikawa mobilized. Tatizo la Nishati nadhani linawagusa watu wachache zaidi na halina athari kama kuvamiwa ardhi yetu. Ndio maana watu wanataka kukaa kamati, mijadala, mazungumzo ya siku 21! gademu!!!
Ndio maana wengine tunasema Uongozi ni uwezo! Si ujana, si elimu, na si sura!
Kulingana na hoja zako za awali, hilo swali lako siyo la msingi hata kidogo. Unachotakiwa ni kutoa ushahidi kadiri uwezavyo kutetea kauli na madai yako kama ulivyoakinisha hapo juu.