Uteuzi Julai 31, 2024: Rais Samia aunda Tume ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi (Presidential Commission on Tax Reforms)

Uteuzi Julai 31, 2024: Rais Samia aunda Tume ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi (Presidential Commission on Tax Reforms)

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tarehe 29 Julai, 2024 wakati wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alitangaza uamuzi wa Serikali kuunda kamati ya kutathmini na kushauri kuhusu masuala ya kodi nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Mhe. Rais ameunda Tume ya Rais ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi (Presidential Commission on Tax Reforms) na kumteua Balozi Ombeni Yohana Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo. Aidha, wajumbe wa Tume walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

i. Prof. Florens Luoga - Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) na Profesa Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam;

ii. Prof. Mussa Juma Assad Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Profesa Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Bw. Leonard Mususa - Aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa PricewaterhouseCoopers (PwC) Tanzania;

iv. CPA. Aboubakar Mohamed Aboubakar Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU);

V. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar - Mshauri wa Masuala ya Sheria;

vi. Bw. David Tarimo - Mtaalam na Mshauri wa Masuala ya Kodi na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushauri wa Kodi, PwC;

vii. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi - Katibu Mkuu Mstaafu; na

viii. Bw. Rished Bade Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

1722445411860.png

PIA SOMA
- Rais Samia amteua Mkuu wa Jeshi la Magereza
 
Bure kabisa!!!

When you run out of ideas, when you’ve hit a dead-end, when you don’t know what else to do, when you don’t have anything to fall back on, you just appoint, appoint, and appoint some more and hope that will solve whatever problems you wish to solve.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tarehe 29 Julai, 2024 wakati wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alitangaza uamuzi wa Serikali kuunda kamati ya kutathmini na kushauri kuhusu masuala ya kodi nchini...
wastage of time and money. Zimeundwa ngapi and what has been achieved?
 
Fursa zaidi zimetolewa kwa waliokuwa na fursa tayari.

Teuzi tunaambiwa ila budget ya hiyo tume ni siri. Ila ikija kujulikana utasikia mabilioni.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tarehe 29 Julai, 2024 wakati wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alitangaza uamuzi wa Serikali kuunda kamati ya kutathmini na kushauri kuhusu masuala ya kodi nchini...
Hana cha maana, ni muda wao wa kula na chakula kimeshaiva, acha waendelee kupeana hizo dinner invitations cards ambazo wamezipa jina la UTEUZI
 
Bure kabisa!!!

When you run out of ideas, when you’ve hit a dead-end, when you don’t know what else to do, when you don’t have anything to fall back on, you just appoint, appoint, and appoint some more and hope that will solve whatever problems you wish to solve.
Nilikuona asubuhi pale kaburini, umelia sana
 
Bure kabisa!!!

When you run out of ideas, when you’ve hit a dead-end, when you don’t know what else to do, when you don’t have anything to fall back on, you just appoint, appoint, and appoint some more and hope that will solve whatever problems you wish to solve.
Bro umenifanya nicheke aisee.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tarehe 29 Julai, 2024 wakati wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alitangaza uamuzi wa Serikali kuunda kamati ya kutathmini na kushauri kuhusu masuala ya kodi nchini...
Namuona mtu serious prof assad back at it again. hii imekaa poa kabisa.

But hii inatoa picha nyingine wazir wa wizara husika ame lost control or hatoshei
 
Back
Top Bottom