Uteuzi Julai 31, 2024: Rais Samia aunda Tume ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi (Presidential Commission on Tax Reforms)

Uteuzi Julai 31, 2024: Rais Samia aunda Tume ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi (Presidential Commission on Tax Reforms)

Hahaha..

Hii nchi tuna safari ndefu kufika tunapohitaji kufika.

Ifike mahala tuwe serious ase kwamba masuala ya kodi hayatambuliki au hatufahamu changamoto na sehemu tulizo vizuri licha ya kuwa taasisi za kodi pamoja na tume mbalimbali.

Viongozi wakipunguza masihara huwenda nchi yetu ikapiga hatua.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tarehe 29 Julai, 2024 wakati wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alitangaza uamuzi wa Serikali kuunda kamati ya kutathmini na kushauri kuhusu masuala ya kodi nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Mhe. Rais ameunda Tume ya Rais ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi (Presidential Commission on Tax Reforms) na kumteua Balozi Ombeni Yohana Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo. Aidha, wajumbe wa Tume walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

i. Prof. Florens Luoga - Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) na Profesa Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam;

ii. Prof. Mussa Juma Assad Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Profesa Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Bw. Leonard Mususa - Aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa PricewaterhouseCoopers (PwC) Tanzania;

iv. CPA. Aboubakar Mohamed Aboubakar Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU);

V. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar - Mshauri wa Masuala ya Sheria;

vi. Bw. David Tarimo - Mtaalam na Mshauri wa Masuala ya Kodi na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushauri wa Kodi, PwC;

vii. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi - Katibu Mkuu Mstaafu; na

viii. Bw. Rished Bade Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).


View attachment 3057904
Hopeless. Hakuna hata mmoja amewahi uza nyanya hapo.


Watu wasiojua chochote kuhusu uhalisia
 
Luoga, mwalimu wa Tax Law, UDSM, na kile kijitabu chake, Assad akateme sumu mpaka ziishe, its a good team
Nchi ikiwa na watu aina hii, ambao pekee analofikiri ni kujikimu..na mbaya zaidi wameroga roga hadi kupata kanafasi ka utumishi wa umma..nchi haiwez kufika popote, kila kinachofanyika anzia uteuzi wanachoona kwanza ni kujikimu..teuzi zote ni fursa za kujikimu, hawaoni kingine zaidi ya hicho..na hawa nao wanajikimu kwa kusifia kila kitu na kujaribu kupoteza mwelekeo wa mada!
 
Bure kabisa!!!

When you run out of ideas, when you’ve hit a dead-end, when you don’t know what else to do, when you don’t have anything to fall back on, you just appoint, appoint, and appoint some more and hope that will solve whatever problems you wish to solve.
Nakumbuka uliwahi SEMA anaweza sana na kuipenda kazi ya kuteua na kutengua. Anatimiza hobby yake.
 
Janabi atasababisha wajumbe wa tume wasiwe wanakula kwasabb ya hamasa yake ya intermittent fasting.
 
Sera za Kodi zinatakiwa ziangalie pia Mazingira salama kiafya ya kuhojiana maswala ya Kodi na Ulipaji

Yaani Mfumo wa Customer care uwe kiafya zaidi Ili walipakodi wanawiri

Janabi anajua mambo mengi

Mlale Unono 😀
Ataanza na kitambi cha Pfof Assad
 
Rais weka na watu wa biashara wenyewe badala ya bureaucrats tu wastaafu. Baraza la Biashara la Taifa ndiyo waathirika namba wani wekeni hata wajumbe wawili mpate uhalisia wa madhaifu ya tax admin on the ground.
 
Sera za Kodi zinatakiwa ziangalie pia Mazingira salama kiafya ya kuhojiana maswala ya Kodi na Ulipaji

Yaani Mfumo wa Customer care uwe kiafya zaidi Ili walipakodi wanawiri

Janabi anajua mambo mengi

Mlale Unono 😀
ni kweli janabi anajua mambo mengi, kuna siku tutamtaiti atuelezee vizuri na sisi tuelewe. Lala unono pia
 
Back
Top Bottom