Uteuzi Julai 31, 2024: Rais Samia aunda Tume ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi (Presidential Commission on Tax Reforms)

Uteuzi Julai 31, 2024: Rais Samia aunda Tume ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi (Presidential Commission on Tax Reforms)

Fursa zaidi zimetolewa kwa waliokuwa na fursa tayari.

Teuzi tunaambiwa ila budget ya hiyo tume ni siri. Ila ikija kujulikana utasikia mabilioni.
Bajeti si utasoma report ya cag ww kijana punguzwa nongwa kwa hiyo unataka miprofesa hii ilipwe pesa ndogo? Ni lazima wale mabilion elimu yao sio ya serikali
 
Nashangaa Waziri wa mahela hayumo
Ingawa ni kama wamekumbukwa tu kwenye mlo
Ukistaafu ipo siku utaitwa tu
Wamekuwa kama wajeda walio standby mda wowote 😄
 
Kwa dhati ya moyo wangu

Nakushukuru kwa kauli zako, Matamanio,uthubutu,nia,sababu na uthubutu wa kufanya mapitio, maboresho, yamkini uundaji upya wa mfumo,taasisi na sheria za kodi.

Hili ni chachu kubwa katika mapinduzi ya uwekezaji,biashara na ujasiliamali ktk nchi yetu.

Kila jema lina gharama ila faida ni kubwa kuliko hasara.
 
Kwa dhati ya moyo wangu
Nakushukuru kwa kauli zako,Matamanio,uthubutu,nia,sababu na uthubutu wa kufanya mapitio,maboresho,yamkini uundaji upya wa mfumo,taasisi na sheria za kodi.

Hili ni chachu kubwa ktk mapinduzi ya uwekezaji,biashara na ujasiliamali ktk nchi yetu.

Kila jema lina gharama ila faida ni kubwa kuliko hasara.
Maboresho gani yamefanyika mkuu? Unaongeza kitu kisicho kuwepo? Hivi inahitaji tume kujua kodi hizi zinahitajika au lah?😂😂😂😂😂😂
 
Sera za Kodi zinatakiwa ziangalie pia Mazingira salama kiafya ya kuhojiana maswala ya Kodi na Ulipaji

Yaani Mfumo wa Customer care uwe kiafya zaidi Ili walipakodi wanawiri

Janabi anajua mambo mengi

Mlale Unono 😀
Waanze na PAYE kwa watumishi, ni kandamizi sanaaa hii na inawaumiza mno mno na Mungu analiona hili
 
hawa wazee ndio waliotufikisha hapa wakiwa vijana, sasa wanatembelea mikongojo watatushauri nn? hivi kweli tumeshindwa kuwaomba WB watufanyie hii analysis kweli? hivi hatuna wachumi kwenye balozi zetu wakatuambia wenzetu wanafanyaje kweli? mbona ali hassan mwinyi aliwatumia akina Hassan Diria kutoka ujerumani, Nyerere alimtumia Amir Jamal kutoka canada. tumeshinwa kweli kuwatumia akina Mariam Salim kweli, hadi utuletee hivi vibabu
 
juzi tulimteua balozi Ammy Mpugwe kuwa mshauri wa raisi, akaishia kutupiga mkwara kuwa yeye ni mtoto wa simba
 
hawa wazee ndio waliotufikisha hapa wakiwa vijana, sasa wanatembelea mikongojo watatushauri nn? hivi kweli tumeshindwa kuwaomba WB watufanyie hii analysis kweli? hivi hatuna wachumi kwenye balozi zetu wakatuambia wenzetu wanafanyaje kweli? mbona ali hassan mwinyi aliwatumia akina Hassan Diria kutoka ujerumani, Nyerere alimtumia Amir Jamal kutoka canada. tumeshinwa kweli kuwatumia akina Mariam Salim kweli, hadi utuletee hivi vibabu
Hakuna nia wala dhamira kurekebisha mapungufu ya kikodi yaliyopo..tume haki jinai ilichukua zaidi ya mwaka kutoa ripoti..toka mapokezi ya ripoti na kamati ile ile akiwemo sefue kufanya ufuatiliaji wa mapendekezo..kuna kitu kimebadilika??
 
Good move, ngoja tuone, lakini ningeshauri expert walau wawili toka UK wahusike hapa!, nawashauri mfumo wa cashless upewe kipaumbele kikubwa, kwani hili ni kama chujio la kila coins!
watembelee kujifunza kutoka nchi zenye mafanikio upande wa kodi ie Mauritius,Singapore
 
Back
Top Bottom