Uteuzi Julai 31, 2024: Rais Samia aunda Tume ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi (Presidential Commission on Tax Reforms)

Rais Samia anaendelea kuonesha kwamba yeye ni Kiongozi na reformist leader.

Next budget tutarajie VAT kushuka kutoka wastani wa 18% Hadi 15-16%.

Naposema hakuna Kiongozi wa miaka ya Karibuni kumfikia Kizimkazi muwe mnaelewa

 
Wafanyabiashara wanaolalamikia mfumo wa kodi kili uchwao hawana mwakilishi. Teuzi nyingine naweza kusema ni funika kombe mwanaharamu apite.
 
Walalamikaji wa kodi na tozo walioko field hawapo.Hawa maprofesa wa theory watasaidia nini.Hakuna tofauti na TRA akiona umefungua biashara anaona unapata sana kazi kukubandikia kodi kubwa
 
Sio wa kuvizia mlo wala hawana njaa hao na pia wana elimu zao kubwa tu na watu wazito sana
Ila unatarajia kodi itashuka?
Wewe ndio umekuwa mtoto kwa hasira
Tujadili tu humu kwani ukiwa na jazba utatoka kila mada umefura
kumbe nachati na mwehu nani kakwambia tanzania tunashida ya kodi kubwa? Kariakoo wameandamana sababu ya kodi kubwa ? Mijitu ambayo haijasoma bwana.Tatizo la kodi tanzania ni mfumo ndo maana hii ni tax reform yaan kuweka mfumo unaoeleweka (predictable and clear) mfumo wa sasa haueleweki na wamakisio sana ndo maana unatoa mwanya wa maafisa wa tra kujitajirikia kijinga,mama anataka auweke ili hata la saba ajue kodi yake kirahisi na kutokuwa na document mfano za vat on imports kusiwe na shida .hata wafanyabiashara kariakoo walikiri tra inatoza kodi ndogo sana
 
Sawa sawa umefafanua vizuri
Ila punguza munkar
Unataka kuelezea jambo ila mpaka ufoke
Unamfokea nani sasa, najua unatafuta matusi ila sio tabia yangu hiyo
Ita kila jina ila unaweza kuandika unayojua bila kuitana majina
Nakutakia siku njema na uwe na amani
Ukiwa hivyo utakufa na pressure aisee
Au ndio makuzi hayo
 
Munauzi sana kushutumu huku hamjui napata munkar sababu naona unarudisha nyuma juhudi njema ,ukiona jambo hujui uliza uzuri wa jf wako wataalamu wa kila aina ,sawa na ww mtu akuzushie shoga utapuuza,je mwehu atae amua kutangaza huku hana uhakika hutapata bmunkar?
kuwa na siku njema
 
Someni kuhusu human herding and ostracism, mtanishukuru sana, mimi nimeiboresha definition ya human herding kama itawapendeza nitakupeni
 
Kweli kuna watu wa kila aina ila unaelezea bila dharau na hasira
Wala usijali, nimeyaona mengi zaidi ya haya humu
Always be calm
I will never retaliate boss
Again, have a pleasant day
 
wanyonge wanachanga paadiem kwaajili ya kutathiminiwa furushi walilolibeba, hii siyo furushi tena ni lumbesa ova😎
 
Tumezoea kusoma mavitabu makubwa kama Sarkar na Mulla, cha Luoga nadhani ni moja ya vitabu vya kwanza kabisa vya Tax Law, with time nadhani ataanza kutoa editions, na kitakuwa kikubwa zaidi
Hakika msomi,

Lakini hawa kina Luoga wana jipya kweli maana kila mjumbe pale ni mstaafu! Walikuwepo kwenye kila kamati za kitaalam.

Tusubiri tuone.
 
Matumizi mabaya ya kodi
Unatengeneza tatizo kuunda tatizo
Huyo waziri wa faranga apumzishwe
Wasomi uchw
 
Hizi tume, task force, uoembuzi wa kina yakinifu vyote vina gharama kubwa. Tume ya katiba watu walipewa mpaka ma v8 na madereva juu ni gharama kwa common mwananchi
 
Tume ni nzuri, Mamlaka ziwe tayari kuchukuwa hatua stahiki maana mapendekezo ya tume yanaweza kupelekea kuliwa vichwa vya baadhi ya viongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…