Uteuzi June 22, 2024: Rais samia ameteua na kutengua viongozi mbalimbali

Uteuzi June 22, 2024: Rais samia ameteua na kutengua viongozi mbalimbali

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
TAARIFA KWA VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

1. Amemteua Dkt. Ashura Abdul Katunzi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi, Dkt. Katunzi alikuwa Afisa Udhibiti Ubora Mkuu, Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Dkt. Katunzi anachukua nafasi ya Dkt. Athuman Yusuf Ngenya ambaye amemaliza muda wake.

2. Amemteua Bw. Hassan Juma Mnyika kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo. Kabla ya uteuzi, Bw. Mnyika alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu. Bw. Mnyika anachukua nafasi ya Bw. Lain Ephraim Kamendu ambaye amestaafu.

3. Amemteua Bw. Addo Missama kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi. Kabla ya uteuzi, Bw. Missama alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu. Bw. Missama anachukua nafasi ya Bw.Joseph Constantine Mafuru ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

20240622_202516.jpg
 
Bi Ashura atafanya uchunguzi kibaini ubora wa sukari Toka Brazil inayodaiwa kuwa fake, ijulikanayo kama GMO?
Hakuna namna ya kujua kama sukari ni GMO labda mtengenezaji aseme hivyo.

BTW, miwa au mimia mingine inayotumika kutengeneza sukari ndio inaweza kuwa GMO, sukari ni final product.

Pia mtu anayesema GMO maana yake ni feki basi hajui hata GMO ni kitu gani.
 
Back
Top Bottom