Uteuzi Juni 15, 2024: Mobhare Matinyi, aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali apangiwa majukumu mengine, nafasi yake yachukuliwa na Thobias Makoba

Uteuzi Juni 15, 2024: Mobhare Matinyi, aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali apangiwa majukumu mengine, nafasi yake yachukuliwa na Thobias Makoba

Baada ya kuona alivyokuwa composed kwenye ile event ya kutoa gawio nilijua tu yule jamaa ndo the next Mkurugenzi Habari Ikulu au Msemaji wa Serikali.

Simjui vizuri ila as long as anafanya kazi na Nehemia Mchechu naamizi hawezi kuwa kilaza. Hadi Nehemia Mchechu akuamini na kukuweka front kwenye event ya namna ile basi wewe lazima utakuwa uko vizuri sana.

Nchi hii wanaojua kugundua uwezo wa watu na kuwakuza namba moja ni Nehemia Mchechu
Nehemia na kafulila itakuwa wamemwaga hela nyingi sana kwa PR team zao. Kwa kweli chawa kazi mnayoifanya tunaiona.
 
Umeanza utoto wako mdogo wangu.
Niambie tija ya hizi teuzi za mara kwa mara? Matinye aliteuliwa kuwa DC baada ya mwezi mmoja akateuliwa kuwa msemaji mkuu baada ya miezi 10 ametolewa, hivi utampima mtu kwa muda mfupi hivyo? teuzi hizi ni gharama kubwa sn kwa walipa kodi, kumteua mtu kuanzia DED/DAS/DC na kwenda juu siyo chini ya milioni 40, je ni sawa na dawati ngapi? tuache uchawa tuongee ukweli.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Habari ndio hiyo wenye kupata wamepata na wenye kuhamishwa wamehamishwa.

Ila tu fahamu ya kuwa msemaji wa serikali wa sasa ameondolewa kwenye nafasi yake na atapangiwa kazi nyingine.

Kazi iendelee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti

Lucas Hebel Mwashambwa.mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa piliView attachment 3018202View attachment 3018205
Asante kwa Taarifa
 
Niambie tija ya hizi teuzi za mara kwa mara? Matinye aliteuliwa kuwa DC baada ya mwezi mmoja akateuliwa kuwa msemaji mkuu baada ya miezi 10 ametolewa, hivi utampima mtu kwa muda mfupi hivyo? teuzi hizi ni gharama kubwa sn kwa walipa kodi, kumteua mtu kuanzia DED/DAS/DC na kwenda juu siyo chini ya milioni 40, je ni sawa na dawati ngapi? tuache uchawa tuongee ukweli.
Kaa kwa kutulia dogo.kinachoangaliwa ni kuleta tija na ufanisi mahali pa kazi.pia Watanzania ni lazima tujuwe kuwa ukipewa kazi basi fanya kwa bidii na siyo kuleta mazoea kazini.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

i Amemteua Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi, Balozi Dkt. Simbachawene alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.

ii. Amemteua Bw. Nkoba Eliezer Mabula kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Maliasili na Utalii anayeshughulikia utalii. Kabla ya uteuzi, Bw. Mabula alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.

Aidha, CP. Benedict Wakulyamba atakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia maliasili.

iii. Amemteua Dkt. Habib Gallus Kambanga kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi, Dkt. Kambanga alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.

iv. Amemteua Bw. Thobias Makoba kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi, Bw. Makoba alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Bw. Makoba anachukua nafasi ya Bw. Mabhare Matinyi ambaye amepangiwa majukumu mengine.

V. Amemteua Bw. Ally Rajab Mketo kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe. Kabla ya uteuzi, Bw. Mketo alikuwa Afisa Tawala Mwandamizi, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukombe. Bw. Mketo anachukua nafasi ya Bw. Onesmo Kisoka ambaye amestaafu.

vi. Amemteua Jaji Dkt. Mary Caroline Levira kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. Jaji Dkt. Levira ni Jaji wa Mahakama ya Rufani. Jaji Dkt. Levira anachukua nafasi ya Jaji Dkt. Gerald Ndika ambaye amemaliza muda wake.

vii. Amemteua Dkt. Leonard Douglas Akwilapo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Dkt. Akwilapo ni Katibu Mkuu Mstaafu na Mhadhiri Mwandamizi, Kikuu Kikuu cha Dodoma. Dkt. Akwilapo anachukua nafasi ya Prof. Maurice Mbago ambaye amemaliza muda wake. Amemteua Dkt. Noel Eusebius Mbonde kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala.

viii. ya Chuo cha Ufundi Arusha. Dkt. Mbonde ni Mkurugenzi Mstafu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

WASIFU WA THOBIAS MAKOBA

Naomba mwenye wasifu wa Bw. Thobias Makoba aliyeteuliwa leo kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali
 

Attachments

  • IMG_20240615_211729_151.jpg
    IMG_20240615_211729_151.jpg
    160.3 KB · Views: 3
Consistency kwenye utendaji inatoka wapi sasa kama kila siku tunateua na kutengua.

Matarijio unayotoa wapi wakati unarotate watu wale wale kutoka huku unapeleka kule.

Incompetency ni Incompetency tu hakuna namna nyingine.
Kama wewe ni mchapa kazi na mbunifu na mwenye mipango mizuri ya kazi,hata ukikaa tu siku moja ofisini watu watajuwa tu kuwa hapa alipita kiongozi mchapa kazi aliyeacha alama.
 
Back
Top Bottom