Uteuzi Juni 15, 2024: Mobhare Matinyi, aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali apangiwa majukumu mengine, nafasi yake yachukuliwa na Thobias Makoba

Uteuzi Juni 15, 2024: Mobhare Matinyi, aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali apangiwa majukumu mengine, nafasi yake yachukuliwa na Thobias Makoba

Ndugu zangu Watanzania,

Habari ndio hiyo wenye kupata wamepata na wenye kuhamishwa wamehamishwa.

Ila tu fahamu ya kuwa msemaji wa serikali wa sasa ameondolewa kwenye nafasi yake na atapangiwa kazi nyingine.

Kazi iendelee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti

Lucas Hebel Mwashambwa.mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa piliView attachment 3018202View attachment 3018205
Acha kusifiasifia kipumbavu we chalii
 
View attachment 3018303
Rais Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

i Amemteua Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi, Balozi Dkt. Simbachawene alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.

ii. Amemteua Bw. Nkoba Eliezer Mabula kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia utalii. Kabla ya uteuzi, Bw. Mabula alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.

Aidha, CP. Benedict Wakulyamba atakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia maliasili.

iii. Amemteua Dkt. Habib Gallus Kambanga kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi, Dkt. Kambanga alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.

iv. Amemteua Bw. Thobias Makoba kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi, Bw. Makoba alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Bw. Makoba anachukua nafasi ya Bw. Mabhare Matinyi ambaye amepangiwa majukumu mengine.

V. Amemteua Bw. Ally Rajab Mketo kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe. Kabla ya uteuzi, Bw. Mketo alikuwa Afisa Tawala Mwandamizi, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukombe. Bw. Mketo anachukua nafasi ya Bw. Onesmo Kisoka ambaye amestaafu.

vi. Amemteua Jaji Dkt. Mary Caroline Levira kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. Jaji Dkt. Levira ni Jaji wa Mahakama ya Rufani. Jaji Dkt. Levira anachukua nafasi ya Jaji Dkt. Gerald Ndika ambaye amemaliza muda wake.

vii. Amemteua Dkt. Leonard Douglas Akwilapo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Dkt. Akwilapo ni Katibu Mkuu Mstaafu na Mhadhiri Mwandamizi, Kikuu Kikuu cha Dodoma. Dkt. Akwilapo anachukua nafasi ya Prof. Maurice Mbago ambaye amemaliza muda wake. Amemteua Dkt. Noel Eusebius Mbonde kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala.

viii. ya Chuo cha Ufundi Arusha. Dkt. Mbonde ni Mkurugenzi Mstafu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.


Mbona Ikulu imesafishwa, kulikoni?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Habari ndio hiyo wenye kupata wamepata na wenye kuhamishwa wamehamishwa.

Ila tu fahamu ya kuwa msemaji wa serikali wa sasa ameondolewa kwenye nafasi yake na atapangiwa kazi nyingine.

Kazi iendelee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti

Lucas Hebel Mwashambwa.mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa piliView attachment 3018202View attachment 3018205
Wananchi tutampangia huyo mama Yako majukumu mengine mnamo 2025.
 
Kabisa mkuu.

Kwa mfano yule aliyepelekwa kisarawe alikuwa lumumba baadae jumba jeupe kabla fagio la juzi.

Mtu wa mfumo ana kadi ya chama pendwa na wanajua katiba mpya ndio mwisho wa hizi sarakasi zao, unahisi mkuu watakubali?
Hawatakubali lakini inabidi tuwalazimishe nchi siyo mali ya CCM ni mali ya watanzania
 
Huyo Dr Akwilapo ndiye aliyemtengenezea Magufuli PhD ya Chemistry pale Mlimani wakati huo tukiwa pale naona bado anaendelea kula fadhila, na atakuwa keshasahau organic chemistry yote.
Una uhakika na hilo uliloandika? Au umesimuliwa tuu!!!
 
Wamesoma Sana unapendaga kitabu gani cha uongozi na Usimamizi!?

download (3).jpg

download.png
 
Kila Mtu na "Maisha Yake"

Kila enzi na "Mambo yake"

"Akili za Watu hizo"

Mtachomoka hata kwenye UTEUZI kitabu gani cha Uongozi tukitumie

download (3).jpg

download.png
 
Back
Top Bottom