Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya

Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi
Taratibu unabii lzm utimie
Hii trela
 
Timu Magufuli ni Timu ya wananchi, ni Timu ya Tanzania ijayo ya haki.

Timu Mbowe na Makamba na Nape na Kinana ni Timu Mafisadi, Timu maslahi binafisi Timu wanafiki.

..nyinyi mnachezewa akili tu.

..Kabudi na Johari watafanyaje kazi pamoja?

..Hamza Johari ndiye aliyeandaa mswada wa Dp World,uliotengua sheria ya ulinzi wa rasilimali, iliyoandikwa na Prof.Kabudi.

..Mama amechanganyikiwa, anatapatapa.
 
Kwahiyo Kabudi na Lukuvi wamekuwa vijana tena maana alivyowaondoa aliwashukuru Kwa kazi nzuri ila wataendelea kuwa karibu nae katika kumpa ushauri na akawaahidi atakuwa anawatumia kwenye majukumu mbalimbali.
 
Hakuna wengine wanaofaa? Mna recycle wale wale tu, tatizo nini mbona watanzania tupo wengi sana? Kama wameshindwa waondolewe wateuliwe wengine wapya, hii michezo haitatusaidia kama taifa.

Vyuo vya serikali kila siku tuna graduate, hamtuoni?

Manasema vyuo vyetu vizuri lakini hamtaki kutuajiri, achaneni na hao wazee, ajiri vijana tujenge taifa letu.
 
Nilipoona tu Wiki iliyopita Rais anamsifia katika Ukumbi fulani nikajua kuna Bomu alishaliandaa na alikuwa Anamzuga tu Kinafiki na leo kamaliza Shughuli. Ogopa sana Rais akikusifia kwani huwa ni Kinyume chake.
Hii kawaida tu, si unaona wote anawasifia wanafanya kazi nzuri lakini anatengua. Aache woga aite mbwai mbwai. Wewe tumekuweka hapa hakuna ulichofanya ama umeharibu 1,2,3….
 
Back
Top Bottom