Pre GE2025 Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Pre GE2025 Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa mwendazake wengi tulifurahi maana alikuwa anakwenda kuingiza nchi kwenye machafuko nyang'au yule kama si Mungu kuingilia kati
Jiwe awe hai nani asubutu kuleta machafuko ? Kitu ambacho hujui machafuko yatatokea sasa wakati huu. Maandamano ya Kenya na UG yatakuwa kama arab spring yatamtoa kizimkazi

Jiwe na mabaya yake yote lakini alitufaa sana. Mfumo ndio ulikuwa mbovu ndio maana unaona sasa hayupo ila wimbi la kutekana na kuuana limezidi yeye aliteka watu wake kina Mo hakuwa ana deal na watu wa chini. Kizimkazi watoto wanauliwa yeye anaita Drama
 
Jiwe awe hai nani asubutu kuleta machafuko ? Kitu ambacho hujui machafuko yatatokea sasa wakati huu. Maandamano ya Kenya na UG yatakuwa kama arab spring yatamtoa kizimkazi

Jiwe na mabaya yake yote lakini alitufaa sana. Mfumo ndio ulikuwa mbovu ndio maana unaona sasa hayupo ila wimbi la kutekana na kuuana limezidi yeye aliteka watu wake kina Mo hakuwa ana deal na watu wa chini. Kizimkazi watoto wanauliwa yeye anaita Drama
Dkt Samia hata hahusiki kabisa
 
Hii tunaweza kusema rais Samia Suluhu Hassan amemkata mtama mbunge wa Mtama Nape Moses Nnauye baada ya kutengua uteuzi wake wa waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari

Kuna uwezekano mkubwa Nape amekatwa mtama huo na rais kwenye nafasi yake hiyo kutokana na kauli yake ya hivi karibuni aliposema kuwa "kupatikana kwa mshindi kwenye uchaguzi inategemea nani anayetangaza matokeo"
 
Hii tunaweza kusema rais Samia Suluhu Hassan amemkata mtama mbunge wa Mtama Nape Moses Nnauye baada ya kutengua uteuzi wake wa waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari

Kuna uwezekano mkubwa Nape amekatwa mtama huo na rais kwenye nafasi yake hiyo kutokana na kauli yake ya hivi karibuni aliposema kuwa "kupatikana kwa mshindi kwenye uchaguzi inategemea nani anayetangaza matokeo"
Ndo akome aache kuropoka ropoka
 
Ya Ruto yametoa darasa huku.

Ila huyu nguli wa uchumi ashukuru sana
Hana unguli wowote, ni vile tu mambo ya...

"Kijana kwenye hizo trillion 2 zilizoingizwa, moja ielekeze kwenye account ile ya Dubai" Wewe utachukua ile ile kama last time zingine zibakie kwenye kibubu chetu tusukumie miradi ya kitaifa.
 
Makamba mutoto wa mama vipi tena?
Ila Nape kanyea kambi.
Hivi hamkumwelewa RC wa Arusha kwenye hotuba yake pale Monduli kwenye kumbukumbu ya Waziri Mkuu, Hayati Edward Sokoine!!? Eti zee la Kisomali likaamua kumwita kwenye Kamati ya Nidhamu ya CCM na kumwambia awataje hao Mawaziri wanaopeleka taarifa za kidaku kwa Dada huko USA akifikiri RC hakupikwa na kupikika/kuiva kisawasawa!! RC akakataa kutoa siri kwa huyo Msomali akijui siri itavuja. Leo ndio siku imetimia na bado!! 🤣🤣
 
Itabidi akina Dina marios wamuonee huruma tuu aisee 😂 kwanza hapo nape atajifanya amesahau kama alitoa hy ahadi 😂
Alishapiga hesabu za mgao wa Tigo, Zantel, Vodacom,Halotel na Airtel kila mmoja akimpa million 10 kil mwezi hakosi za kuhonga. Ndio maana alidai 300M ni hela ndogo sana kwake 🤣
 
My Take
Cheo ni dhamana, maisha yaendelee 🙏🙏👇👇

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt, Moses Kasiluka, viongozi hao ni kama ifuatavyo;-

  1. Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Silaa alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anachukua nafasi ya Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  2. Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu);
  3. Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huu Mhe. Kikwete alikuwa Naibu Waziri, Odisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  4. Balozi Mahmoud ThabitKombo ameteuliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Balozi Kombo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy, anachukua nafasi ya Mhe. January Makamba (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
  5. Mhe. Cosato Dvid Chumi (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiki. Mhe. Chumi anachukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye atapangiwa kituo cha kazi;
  6. Mhe. Deus Clement Sangu (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
  7. Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Mhe. Londo anachukua nafasi ya Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
  8. Bw. Eliakim Chacha Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Kabla ya uteuzi huu Bw. Maswi alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA);
  9. Bi Mary Gasper Makondo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Makondo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Bi. Makondo anachukua nafasi ya Bi. Rehema Sefu ambaye amestaafu.
  10. Bw. Kiseo Yusuph Nzowa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huu Bw. Nzowa alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikuli;
  11. Bw. Musa Haji Ali ameteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Ali alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;
  12. Bw. Louis Peter Bura ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Bw. Bura anachukua nafasi ya Bw. Said Juma Nkumba ambaye amepangiwa majukumu mengine;
  13. Bi. Kemirembe Rose Lwota amehamishwa kutoka Wilaya ya Manyoni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti;
  14. Dkt. Vincent Biyegela Mashinji amehamishwa kutoka Wilaya ya Serengeti kuwa Mkuu wa Wilaya Manyoni;
  15. Dkt. Maulid Sleiman Madeni ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti;
  16. Bw. Afraha Nassoro Hassan amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Seringeti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Bw. Hassan anachukua nafasi ya Bw. William Anyitike Mwakalambile ambaye uteuzi wake umetenguliwa na;
  17. Bw. Dennis Kwame Simba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Kabla ya uteuzi huu Bw. Simba alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Serikali kumbe sometmes haina dhamira ya dhati,au tuseme uchawi upo, Jery silaa unamtoaje wizara ya ardhi wakati alikuwa anafanya vizuri zaidi!!? Au ndio matapeli wameenda kuroga ahamishwe wizara au atenguliwe!!! Kweli uchawi upooooo
 
Back
Top Bottom